mbingunikwetu
JF-Expert Member
- Feb 17, 2015
- 13,897
- 18,477
Aibu yake kubwa ni mbele ya Uhuru Kenyatta. Uhuru Kenyatta amembeba sana, serikali ya Kenyatta imembeba sana!! Ruto akapakwa matope hadharani na mkuu wa nchi kuwa hawezi na hana jipya maana alipewa nafasi ya kuwa makamu wa rais lakini hakufanya chochote!!. Ukizingatia kuwa Kenyatta yuko nyuma ya kabila kubwa kabisa kenya, ilitazamiwa kuwa wakikuyu watasikia maneno ya Kenyatta na watamnyima kura Ruto. Kinyume na matazamio hayo Raila kashindwa na hivyo bila shaka anaona aibu kubwa kwa Kenyatta kuwa alimbeba lakini hakubebeka.
Aibu nyingine ni kuwa uchaguzi ulikuwa huru na wa haki sana. Kulikuwa na uwazi mkubwa katika kuhesabu na kurekodi kura ya kila mmoja na mawakala walikuwa wanapata nakala ya matokeo kwenye kila kituo, na kila mkenya na asiye mkenya alikuwa anaweza kuyaona matokeo ya vituo vyote kupitia tovuti ya tume ya uchaguzi. Uwazi huo haumpi nafasi ya kusingizia kuibiwa kura au kudanganywa! Halafu hawezi kusingizia chochote maana matokeo yapo wazi kwa kila mmoja kujionea na kujijumlishia!!
Njia pekee iliyobakia ni kulazimisha kutengeneza mazingira yatakayompa nafasi ya kuona ameonewa! Kwa hiyo kupitia watu wake wa karibu kwenye tume ya uchaguzi (au kuwarubuni) ili wasusie zoezi la kutangaza matokeo (baada ya kuwa wameshiriki zoezi la kuhakiki matokeo kwa ukamilifu na matokeo wakiwa wanayajua). Wakazua jambo ambalo halipo kikatiba kuwa eti Raila apewe nafasi ya kuyaona na kuyahakiki matokeo-jukumu ambalo halimhusu kabisa.
Walizua jambo hilo huku wakijua kabisa kuwa hawawezi kukubaliwa. Walivyokataliwa bila shaka walifurahi sana kuwa angalau wamepata sababu wale wajumbe wa tume waliorubuniwa kudai hawajihushi na utangazwaji wa matokeo kwa "kukosekana uwazi. Raila naye akapata upenyo wa kuficha aibu ya uso wake ili asitokee kwenye utangazaji wa matokeo!! Hali kadhalika Uhuru Kenyatta naye hakuhudhuria! Naye ni aibu: angemtazamaje Ruto usoni? kampiga vita lakini ameshinda!! Kwa hiyo wakatafutwa watu waandae mazingira ili kuficha aibu ya Raila na Uhuru Kenyatta.