Tumzungumzie Dkt. Tulia Ackson baada ya kupata ubunge Mbeya Mjini

Tumzungumzie Dkt. Tulia Ackson baada ya kupata ubunge Mbeya Mjini

Nguvu kubwa iliyotumika kuusaka ubunge kwa mbunge wa Mbeya mjini DK. Tulia Ackson iliwaaminisha wengi kuwa ndiyo itakua dhamira ya utendaji ofisini pindi atakapopata idhini hiyo.

Ndoto ya kuusaka ubunge ikatimia katika uchaguzi mkuu wa Mwezi Oktoba 2020 kwa kushinda ubunge wa Mbeya mjini pamoja na baraza la madiwani zaidi ya viti 30 vikienda chama cha mapinduzi.

Baada ya ushindi matarajio yakaanza kujaa miongoni mwa watu wa Mbeya kutokana na cheo alichonacho kitaifa kama Naibu Spika wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Imani hiyo ilikuwa zaidi na kuchochea mtazamo mpya kwa wakazi wa Mbeya kwa kuamini kuwa Tulia atafungua milango mipya ya maendeleo ndani ya mji wa Mbeya na mkoa kwa ujumla kwakuwa anashikilia cheo chenye ushawishi kitaifa.

Kwa muda mrefu yaelekea muongo mmoja sasa, mkoa wa Mbeya umetengwa kwenye ajenda za maendeleo kitaifa ingawaje sababu hazijulikani.

Aliyekuwa Rais wa Tanzania hayati John Magufuli aliwahi kunukuliwa akisema Uwepo wa mbunge wa upinzani jijini Mbeya kwa wakati ule ulikwamisha maendeleo.

Kauli hii ya hayati Magufuli iliwapa watu imani ya mabadiliko wakiamini kuwa baada ya kumchagua Tulia ambae ni wa chama Tawala basi mambo yangebadilika waanze kushuhudia ajenda za maendeleo zikimiminika mkoani Mbeya.

Kwanini Tumzungumzie Tulia kwenye hili?
Kama ilivyoelezwa kwenye utangulizi ni kwamba Tulia alipewa Imani akiwa mbunge wa kuteuliwa na Sasa ni mbunge wa kuchaguliwa hivyo anategemewa kufanya makubwa zaidi.

Jiji la Mbeya ndilo funguo ya mkoa na Ukanda wa nyanda za juu kusini, hivyo maendeleo yake yanainua sehemu nyingine za mkoa Kama Tukuyu, Chunya, Kyela, Mbarali Na nyingine nyingi.

Uwepo wa Tulia uliaminiwa kuwa nuru ya kuvutia wawekezaji kwenye mambo mbalimbali kama vile viwanda, Kilimo, biashara na michezo.

Uwekezaji wa Serikali katika miundombinu na uchukuzi kama vile Barabara, reli na Usafiri wa anga mambo ambayo yanaweza kuchochea maendeleo ya watu na mkoa kwa ujumla.

Prince Mwaihojo ambaye ni msomi na mdau wa maendeleo mkoani Mbeya anasema ndani ya mwaka mmoja kwenye madaraka kama mbunge wa kuchaguliwa Tulia amewekeza kwenye vitu laini ambavyo havina manufaa makubwa kwa maendeleo ya Mbeya kwa miaka ijayo bali kwa manufaa ya kisiasa tu.

Mwaihojo anavitaja vitu hivyo kuwa "Vitu laini" Kama vile ujenzi wa vituo vya mabasi na machinga pamoja na kuendesha matamasha ya utamaduni.

Msomi huyu wa chuo kikuu Cha Oxford Uingereza anasema Wakati wa utawala wa Rais kikwete aliesema kuwa baada ya kuhamisha uwanja wa ndege kutoka mbeya mjini kwenda Songwe basi uwanja huo ungetumika kama chuo Cha kimataifa Cha masuala ya anga.

Anasema ujenzi wa chuo hicho ungevutia uwekezaji mkubwa wa Wageni ambao wangekuja kusoma na ingekua fursa kubwa kwa mkoa kujitangaza kimataifa.

Pia kikwete 2012 alipokuwa akihutubia mkutano wa Wafanyakazi siku ya Mei mosi katika Viwanja vya Sokoine jijini Mbeya alinukuliwa akisema uwanja mpya wa Songwe utakuwa ni uwanja wa kimataifa na usaidie wakulima watoke na matunda Mbeya wakauze uholanzi.

Lakini uongozi wa Tulia hujaweka mkazo kwenye suala hilo na kupelekea eneo uwanja wa zamani kugawiwa kwa wamachinga na ule mpya kubaki kwa matumizi ya ndege za ndani ya nchi na sio kimataifa zaidi kama ulivyo tarajiwa na kikwete.

Pia suala la barabara kuu ya kimataifa ya Tanzania-Zambia ambayo inapita katikati ya mji inaonekana kutokidhi matumizi kwa kusababisha msongamano katikati ya mji na kuwa kero ya mda mrefu kwa watumiaji.

Jambo hili lilifikishwa mbele ya ofisi ya bunge kwa muda mrefu lakini bado hakuna jitihada zilizochukuliwa katika kujenga barabara mpya yenye upana wa kukidhi matumizi.

Mwaka mmoja wa Tulia madarakani bado una deni la kulipa matarajio ya wananchi wengi ambao waliamini kuwa utakuwa suluhisho la mengi.

Licha ya jitihada alizozifanya katika kuwezesha akina mama, Vijana, wazee na walemavu kwa kuwapa mikopo na bajaji mambo haya yanatakiwa kuendelea huku sera mpya za maendeleo ya Mbeya zikisukwa.

Wana Mbeya wanataka kuona Viwanda vinafufuliwa Kama Kiwanda Cha zana za kilimo mbeya, Kiwanda cha Kahawa, Viwanda vya bidhaa mbalimbali vinaanzishwa mkoani Mbeya kupitia Msaada wa SIDO.

Kwa nyakati tofauti Tulia mwenyewe amewahi kulalamikia kutengwa kwa mkoa wa Mbeya katika ajenda za miundombinu kitaifa huku mikoa mingine ikitengewa bajeti kubwa kila mwaka jambo ambalo linavunja hamasa kwa wananchi ambao nao wanalipa kodi.

Muda alio nao ungali bado mrefu zaidi ana nafasi ya kufanya makubwa zaidi iwapo tu ataamka na kutambua ushawishi alio nao kwenye uongozi wa taifa hili katika kuwaletea manufaa Wananchi wa Mbeya mjini pamoja na mkoa kwa ujumla Kama walivyo tarajia.

Peter Mwaihola kitaaluma ni mwandishi wa habari na mchambuzi wa masuala ya siasa na jamii.
Tulia hakuchaguliwa na wana Mbeya Mjini bali ni Mbunge wa Magufuli.

Samia hawezi kutekeleza ahadi za Magufuli kwa Tulia Ackson, kwa hiyo sahauni kabisa kupata miradi kwa kumtegemea yule kijakazi

Wana Mbeya mjini kuweni wapole hadi mwaka 2025 mtakapochagua Mbunge wenu mnayemtaka.
 
Muda alio nao ungali bado mrefu zaidi ana nafasi ya kufanya makubwa zaidi iwapo tu ataamka na kutambua ushawishi alio nao kwenye uongozi wa taifa hili katika kuwaletea manufaa Wananchi wa Mbeya mjini pamoja na mkoa kwa ujumla Kama walivyo tarajia.
Sasa anakwenda kufanya makubwa as a Spika wetu mpya.
P
 
Sasa anakwenda kufanya makubwa as a Spika wetu mpya.
P
Tulia ataendelea kuwa Naibu Spika. Yeye naye ni Sukuma Gang na alikuwa anambeza sana Samia akiwa VP.

Hata hivyo Hana HAIBA ya kuwa Spika. Mbeya wana HASARA
 
Tulia ataendelea kuwa Naibu Spika. Yeye naye ni Sukuma Gang na alikuwa anambeza sana Samia akiwa VP.

Hata hivyo Hana HAIBA ya kuwa Spika. Mbeya wana HASARA

Well said, academically (paper) ziko safi ila ni bomu la mwisho tutaharibu kumpa u spika!
 
Upande alokuwa Tulia ndio upande wa Ndugai sasa anawezaje kuaminiwa na mwenyekiti
Hii ndoto imeishia hapa labda tusubiri wakati ujao
Si umemsikia Gwajima akisema alimtumia sms Spika kumpongeza baadae kaja kumponda
Sawa kwenye kundi wako wengi na Tulia akiwemo
Wakubwa labda tuulizane,
SSH alikuwa VP wa JPM kwa miaka yote, yeye alikuwa team nani?
Kama JPM asingemwona na team yake, je 2020 wakati anachukua form mara pili, kama asingekuwa na imani nae, angeweza kumrejesha kama running mate?

CCM wamejijenga kuwa loyal kwa Mkiti ambae in most cases huwa ndie Rais wa nchi pia.

SSH kawarithi mawaziri na wabunge ambao mchakato wote wa kupitishwa kugombea ulifanywa chini ya JPM kama mkiti wa CCM.

Kama SSH atataka aje na team mpya ambayo iko "loyal" kwake basi itamlazimu agombee Urais 2025 ili pia apitishe wagombea wabunge kati ya hawa wa sasa au wapya ambao watakuwa "loyal" kwake.

Angalizo, hatuhitaji Bunge hasa Spika ambae ni loyal kwa Executive Branch. Spika ni vema kumheshi Rais kwa nafasi yake ya Ukuu wa nchi, ila ni vema awe na uwezo wa kuendesha bunge kama taasisi inayojitegemea ili kudhibiti serikali kwa maslahi ya wananchi hasa pale ambapo watu wachache serikalini wanakuwa off-truck.

Wakati wa JK, Spika wa bunge kawahi kuunda tume teule ya bunge kwa nyakati tofauti kuhoji serikali dhidi ya matumizi ya mabaya ya fedha wa mawaziri kadhaa.
Kama mtakumbuka mawaziri kama EL, Karamagi & Msabaha (Richmond Saga)
Nchimbi, Nahodha, Balozi Kagasheki (Saga la Twiga kuutoroshwa na ukikwaji wa haki za binadamu)... this list goes on.

Tujipe dhana, Ndugai alihoji kwanini 1.3Tril yet kulikuwa na tozo; hoja hii ingeweza kujibiwa kwa facts, say kama ni makusanyo ya tozo ingechukuwa mwaka kupata fedha za kujenga madarasa, ila kwa mkopo tumeweza kujenga madarasa kwa muda mfupi na tozo zitaendelea ku-serve kwe TARURA na maji vijijini.

Vip kama Job angeunda tume teule kuchunguza matumizi ya 1.3Tril ambayo pia ni mandate yake; nadhani hapo wangemwona kama "muasi" kumbe anafanya kazi yake.

Nadhani mtu anae-challenge hadharani akajibiwa kwa hoja sio mbaya, hoja ijibiwe kwa hoja, hii itatufanya tuwe stable kama taifa na afya kwa demokrasia ya kibunge hata CCM pia.

Kuhusu Job, maji yashamwagika. CCM na serikali ikijenga spirit ya uwoga sana, ipo siku baadhi ya viongozi kwa ubinadamu watakosea, wanaweza kupida madili na atakosekana mtu wa ku-challenge ya kuonesha udhaifu kama utatokea.

Sitta akiwa Rais wa serikali ya wanafunzi UDSM aliwahi kumpinga mwl. Nyerere akiwa Rais wa nchi, pamoja na kumfukuza chuo na baadae alimsamehe, yet akampa nafasi ya uwaziri.

Kama Job alikosa, na akaomba msamaha, je, kuna ya kujifunza kwa Nyerere aliepigwa, yet akafanya kazi na waliompinga.

Rai yangu, tujadiliana kwa hoja na staha, tuheshimiane hata kama tuna utofauti wa hoja na tusiraruane.

Kila la kheri spika mpya ajae.
 
Kwa kubashiri tu, Spika mpya anaweza kuwa Nani?
 
Sasa anakwenda kufanya makubwa as a Spika wetu mpya.
P
Atakubalika na wabunge wampe kiti hicho maana inasemekana nae Ni Sukuma Gang?
 
Atakubalika na wabunge wampe kiti hicho maana inasemekana nae Ni Sukuma Gang?
Sukuma Gang ni nini au ni nani?

Rais wa sasa alikuwa VP, baada ya kifo cha #1, kikatiba ameapishwa na kuwa #1; je na yeye ni Sukuma gang kwa kuwa alikuwa VP kwa miaka 5 ya kwanza, then JPM akamteua kuwa running mate kwa kipindi cha pili?

VP wa sasa alikuwa boss wa TRA kwa uteuzi wa JPM then waziri wa fedha, je, nae anaweza kuwa kuwa sukuma gang simply SSH alimkuta ni waziri wa fedha?

Chongolo ambae ni katibu mkuu CCM, ni JPM ndie alimpa u-DC. Je nae ni Sukuma Gang kwa kuwa SSH alimkuta akiwa DC

Naibu katibu Mkuu CCM bara alikuwa RC na SSH akamsogeza kwenye chama, nae aondolewe kwa hii dhana na sukuma gang?

Rais SSH amemrithi kila mtu aliekuwa kwenye serikali wa JPM na yeye akiwa VP ni sehemu ya serikali. Je avunje bunge lote na kuanza mchakato ili aepukane na Sukuma gang?

Kama kuna hoja ambayo inapwaya na inakosa logic na kuonekana fulani ni sukuma gang na fulani sio wakati watu walio kwenye mfumo wa utawala by 95% SSH kawakuta nae alikua sehemu ya mfumo huo huo.

Ni kama wakati wa JK kulikuwa na kundi linaitwa wanamtandao, yet baada ya tume teule ya bunge kuundwa na Spika Sitta (ambae nae wanasema alikuwa mwanamtandao) EL akalazimika kujiuzuru nafasi ya u-PM;

Kuna dhana huwa tunazijengea hoja ila zinakosa uzito na depth ikiwamo hii ya sukuma gang. Unless kama kuna criteria ziwekwe wazi ili kuwa na rejea kuliko kubaki na hisia.
 
Kwanini Tumzungumzie Tulia kwenye hili?
Kama ilivyoelezwa kwenye utangulizi ni kwamba Tulia alipewa Imani akiwa mbunge wa kuteuliwa na Sasa ni mbunge wa kuchaguliwa hivyo anategemewa kufanya makubwa zaidi.

Muda alio nao ungali bado mrefu zaidi ana nafasi ya kufanya makubwa zaidi kwa ushawishi alio nao kwenye uongozi wa taifa hili katika kuwaletea manufaa Wananchi wa Mbeya mjini pamoja na mkoa kwa ujumla Kama walivyo tarajia.

Peter Mwaihola kitaaluma ni mwandishi wa habari na mchambuzi wa masuala ya siasa na jamii.
Akiupata Uspika, atafanya Makubwa zaidi.
P
 
Sasa anakwenda kufanya makubwa as a Spika wetu mpya.
P
Uchuro huu, Mhimili mmoja unatosha kuongozwa na mwanamke.
 
Back
Top Bottom