Tumzungumzie Dkt. Tulia Ackson baada ya kupata ubunge Mbeya Mjini

Tulia hakuchaguliwa na wana Mbeya Mjini bali ni Mbunge wa Magufuli.

Samia hawezi kutekeleza ahadi za Magufuli kwa Tulia Ackson, kwa hiyo sahauni kabisa kupata miradi kwa kumtegemea yule kijakazi

Wana Mbeya mjini kuweni wapole hadi mwaka 2025 mtakapochagua Mbunge wenu mnayemtaka.
 
Muda alio nao ungali bado mrefu zaidi ana nafasi ya kufanya makubwa zaidi iwapo tu ataamka na kutambua ushawishi alio nao kwenye uongozi wa taifa hili katika kuwaletea manufaa Wananchi wa Mbeya mjini pamoja na mkoa kwa ujumla Kama walivyo tarajia.
Sasa anakwenda kufanya makubwa as a Spika wetu mpya.
P
 
Tulia ataendelea kuwa Naibu Spika. Yeye naye ni Sukuma Gang na alikuwa anambeza sana Samia akiwa VP.

Hata hivyo Hana HAIBA ya kuwa Spika. Mbeya wana HASARA
 
Tulia ataendelea kuwa Naibu Spika. Yeye naye ni Sukuma Gang na alikuwa anambeza sana Samia akiwa VP.

Hata hivyo Hana HAIBA ya kuwa Spika. Mbeya wana HASARA

Well said, academically (paper) ziko safi ila ni bomu la mwisho tutaharibu kumpa u spika!
 
Wakubwa labda tuulizane,
SSH alikuwa VP wa JPM kwa miaka yote, yeye alikuwa team nani?
Kama JPM asingemwona na team yake, je 2020 wakati anachukua form mara pili, kama asingekuwa na imani nae, angeweza kumrejesha kama running mate?

CCM wamejijenga kuwa loyal kwa Mkiti ambae in most cases huwa ndie Rais wa nchi pia.

SSH kawarithi mawaziri na wabunge ambao mchakato wote wa kupitishwa kugombea ulifanywa chini ya JPM kama mkiti wa CCM.

Kama SSH atataka aje na team mpya ambayo iko "loyal" kwake basi itamlazimu agombee Urais 2025 ili pia apitishe wagombea wabunge kati ya hawa wa sasa au wapya ambao watakuwa "loyal" kwake.

Angalizo, hatuhitaji Bunge hasa Spika ambae ni loyal kwa Executive Branch. Spika ni vema kumheshi Rais kwa nafasi yake ya Ukuu wa nchi, ila ni vema awe na uwezo wa kuendesha bunge kama taasisi inayojitegemea ili kudhibiti serikali kwa maslahi ya wananchi hasa pale ambapo watu wachache serikalini wanakuwa off-truck.

Wakati wa JK, Spika wa bunge kawahi kuunda tume teule ya bunge kwa nyakati tofauti kuhoji serikali dhidi ya matumizi ya mabaya ya fedha wa mawaziri kadhaa.
Kama mtakumbuka mawaziri kama EL, Karamagi & Msabaha (Richmond Saga)
Nchimbi, Nahodha, Balozi Kagasheki (Saga la Twiga kuutoroshwa na ukikwaji wa haki za binadamu)... this list goes on.

Tujipe dhana, Ndugai alihoji kwanini 1.3Tril yet kulikuwa na tozo; hoja hii ingeweza kujibiwa kwa facts, say kama ni makusanyo ya tozo ingechukuwa mwaka kupata fedha za kujenga madarasa, ila kwa mkopo tumeweza kujenga madarasa kwa muda mfupi na tozo zitaendelea ku-serve kwe TARURA na maji vijijini.

Vip kama Job angeunda tume teule kuchunguza matumizi ya 1.3Tril ambayo pia ni mandate yake; nadhani hapo wangemwona kama "muasi" kumbe anafanya kazi yake.

Nadhani mtu anae-challenge hadharani akajibiwa kwa hoja sio mbaya, hoja ijibiwe kwa hoja, hii itatufanya tuwe stable kama taifa na afya kwa demokrasia ya kibunge hata CCM pia.

Kuhusu Job, maji yashamwagika. CCM na serikali ikijenga spirit ya uwoga sana, ipo siku baadhi ya viongozi kwa ubinadamu watakosea, wanaweza kupida madili na atakosekana mtu wa ku-challenge ya kuonesha udhaifu kama utatokea.

Sitta akiwa Rais wa serikali ya wanafunzi UDSM aliwahi kumpinga mwl. Nyerere akiwa Rais wa nchi, pamoja na kumfukuza chuo na baadae alimsamehe, yet akampa nafasi ya uwaziri.

Kama Job alikosa, na akaomba msamaha, je, kuna ya kujifunza kwa Nyerere aliepigwa, yet akafanya kazi na waliompinga.

Rai yangu, tujadiliana kwa hoja na staha, tuheshimiane hata kama tuna utofauti wa hoja na tusiraruane.

Kila la kheri spika mpya ajae.
 
Kwa kubashiri tu, Spika mpya anaweza kuwa Nani?
 
Atakubalika na wabunge wampe kiti hicho maana inasemekana nae Ni Sukuma Gang?
 
Atakubalika na wabunge wampe kiti hicho maana inasemekana nae Ni Sukuma Gang?
Sukuma Gang ni nini au ni nani?

Rais wa sasa alikuwa VP, baada ya kifo cha #1, kikatiba ameapishwa na kuwa #1; je na yeye ni Sukuma gang kwa kuwa alikuwa VP kwa miaka 5 ya kwanza, then JPM akamteua kuwa running mate kwa kipindi cha pili?

VP wa sasa alikuwa boss wa TRA kwa uteuzi wa JPM then waziri wa fedha, je, nae anaweza kuwa kuwa sukuma gang simply SSH alimkuta ni waziri wa fedha?

Chongolo ambae ni katibu mkuu CCM, ni JPM ndie alimpa u-DC. Je nae ni Sukuma Gang kwa kuwa SSH alimkuta akiwa DC

Naibu katibu Mkuu CCM bara alikuwa RC na SSH akamsogeza kwenye chama, nae aondolewe kwa hii dhana na sukuma gang?

Rais SSH amemrithi kila mtu aliekuwa kwenye serikali wa JPM na yeye akiwa VP ni sehemu ya serikali. Je avunje bunge lote na kuanza mchakato ili aepukane na Sukuma gang?

Kama kuna hoja ambayo inapwaya na inakosa logic na kuonekana fulani ni sukuma gang na fulani sio wakati watu walio kwenye mfumo wa utawala by 95% SSH kawakuta nae alikua sehemu ya mfumo huo huo.

Ni kama wakati wa JK kulikuwa na kundi linaitwa wanamtandao, yet baada ya tume teule ya bunge kuundwa na Spika Sitta (ambae nae wanasema alikuwa mwanamtandao) EL akalazimika kujiuzuru nafasi ya u-PM;

Kuna dhana huwa tunazijengea hoja ila zinakosa uzito na depth ikiwamo hii ya sukuma gang. Unless kama kuna criteria ziwekwe wazi ili kuwa na rejea kuliko kubaki na hisia.
 
Akiupata Uspika, atafanya Makubwa zaidi.
P
 
Uchuro huu, Mhimili mmoja unatosha kuongozwa na mwanamke.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…