Kuna mambo kadhaa ambayo tunaweza kujifunza kutoka eurozone. Ningependa zaidi kutumia matukio ya Cyprus kufafanua. Kwanza, ni muhimu tukaelewa kwamba kinachoendelea nchini Cyprus ni collapse ya mfumo wa fedha/banking system kutokana na fedha nyingi kutoweka katika mzunguko, hali ambayo imeathiri availability of credit/mitaji to finance businesses ambazo ni key katika kutengeneza ajira katika taifa, kuchangia kuongezeka kwa kwa mapato ya ndani taifa kupitia income and corporate taxes, na pia kuongeza pato la la taifa (GDP). Cyprus imeathirika katika maeneo yote haya matatu. Kuna mambo kadhaa ambayo tunaweza kujifunza lakini kwa sasa nitajadili machache:
Kwanza, hii ni wake up call na reminder kwamba hoja ya Zitto bungeni mwaka jana (2012) kuhusu fedha chafu ma madhara yake katika uchumi ilikuwa ni hoja muhimu sana kwa maana ya kwamba mzunguko mkubwa wa fedha nchini Tanzania ni aidha wa fedha chafu au fedha zisizo rasmi au vyote kwa pamoja. Fedha za namna hii ni vigumu kuzidhibiti na zina tabia ya umalaya kwa maana ya kwamba zina hama hama kutokana na tamaa na uwoga, kwa mfano leo hii tunaweza kuwa na fedha nyingi sana ambazo zinajenga magorofa na kutoa ajira kwa watu, lakini kesho, just out of speculation hata za kizushi, fedha hizi zinaweza kutoweka katika mzunguko na kupelekea kuanguka kwa mfumo mzima wa fedha ndani ya taifa;
Kwahiyo, kinachoendelea nchini Cyprus ni meltdown ya mfumo wa kifedha/kibenki; je nini kimechangia sana? Tufahamu kwamba Cyprus ni moja ya nchi maarufu za kutunza fedha za mafisadi, fedha nyingi haramu na matajiri wakwepa kodi kwa ujumla kutoka sehemu mbalimbali duniani offshore accounts, hivyo fedha zake nyingi zilizokuwa katika mzunguko zilitokana na fedha hizi Malaya; Nyingi ya fedha hizi zilikuwa zikiwekezwa katika Sokola Hisa - Stock Exchange ya Cyprus kama Portfolio Investments; Tukumbuke kwamba kuna aina mbili ya financial flows (investments) kutoka katika nchi moja kwenda nyingine Kwanza ni Foreign Direct Investments (FDI) ambapo wawekezaji uenda kuwekeza katika ujenzi wa viwanda, migodi, na makampuni mbalimbali ya kuzalisha bidhaa na kutoa huduma; aina ya pili ya foreign financial flows ni Foreign Portifolio Investments (FPI) ambapo matajiri halali, mafisadi, wauza madawa ya kulevya n.k na wakwepa kodi uingiza fedha zao katika uchumi husika na kujiingiza katika mchezo wa kutengeneza faida haraka hasa kwa kununua na kuuza hisa katika soko la hisa (stock exchange) ndani ya uchumi/taifa husika;
Foreign Portifolio Investments (FPI) ni fedha Malaya kama nilivyojadili, na ni fedha za mguu mmoja ndani, mguu mmoja nje kutokana na mazingira yake kutawaliwa na uwoga, tama na kila aina ya uchafu, kwahiyo speculation zozote hata ambazo hazina msingi kama vile tetesi kuhusu hatua za serikali husika kuja na masharti magumu ya kudhibiti feddha chafu, au tetesi kuhusu machafuko ya kisiasa n.k, hupelekea wenye fedha za namna hii kufanya maamuzi ya kuzihamisha over night hivyo kuzitoa kutoka katika mzunguko wa kifedha ndani ya uchumi husika na kuzipeleka kwingine; sasa kama uchumi wa nchi husika unategemea sana fedha za namna hii katika mzunguko wake wa fedha, kinachofuata ni disaster katika mfumo na mzunguko wa ndani wa fedha; Lesson nyingine hapa ni kwamba Financial inflows nzuri na zenye maana kwa uchumi legelege kama wetu au uchumi wa taifa kama Cyprus ni zile za FDIs- Foreign Direct Investments ambazo zinaenda kuwekeza katika uanzishwaji wa makampuni, biashara ambapo jobs get created, hivyo kuchangia ongezeko la makusanyo ya kodi na GDP ya nchi; Fedha zinazoingia kwa mtindo wa FDI hazibabaishwi na mere speculations kama fedha Malaya za FPI;
Suala jingine ambalo ambalo ningependa kulijadili linahusiana zaidi na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ambayo baadhi ya wadau humu wameijadili katika muktadha wa mada husika. Katika hili, pengine kutoka kwangu zaidi ni pendekezo kwamba tunapoongelea East Africa Monetary Union/Sarafu Moja katika jumuiya ya afrika mashariki, nadhani muhimu tukafanya hivyo kwa kulenga zaidi katika uchambuzi wa fursa na changamoto zilizopo katika muungano wa kiuchumi (economic integration) in a holistic manner (sio kivipande vipande), huku tukitambua kwamba muungano wa kiuchumi baina ya nchi wanachama husika popote pale hupitia hatua nyingi kuna hatua za mwanzo na hatuo za mwisho, huku kila hatua ikitoa fursa, faida, hasara zake na changamoto zake; Hivyo ndivyo tutaweza kuwa na mjadala wa maana juu ya wapi tunataka kwenda n.k; Tatizo lililopo ni kwamba kuna utamaduni wa watawala fulani fulani katika Jumuiya yetu wa aidha ya kuzuia a speedy process kutoka hatua moja ya economic integration kwenda hatua nyingine kwa sababu za kizalendo, lakini pia wapo wanaofanya hivyo kwa sababu za kisiasa; Vilevile wapo baadhi ya watawala ambao wana harakisha mchakato wa muungano wa kiuchumi kutoka hatua moja hadi nyingine kwa sababu za kizalendo, na pia wapo ambao wanafanya hivyo kwa sababu za kisiasa; Lakini mbaya zaidi ni kwamba tunarudi katika tatizi lile lile ambapo POLITICS IS SUPREME TO EVERY COMMON SENSE AND RATIONALITY, INCLUDING ECONOMICS;
Kama nilivyosema hapo awali, muungano wa kiuchumi hufuata hatua kadhaa, na hatua hizi zipo saba, huku kila moja ikiwa na fursa zake, faida zake, hasara zake na changamoto zake; Kwahiyo katika muktadha wa EAC huku tukizidi kujifunza kutoka Eurozeone experience, nadhani ni muhimu tukatumia framework ya mchakato wa muungano wa kiuchumi kujadili fursa, faida, hasara na changamoto za kila hatua za mchakato husika, kama vile Monetary Union n.k. Hatua za mchakato wa muungano wa kiuchumi ni kama ifuatavyo:
Awali kabisa ni Preferential Trade Area (PTA); PTA ni a trade block baina ya nchi wanachama ambapo nchi husika hupeana upendeleo katika eneo la kodi za bidhaa Fulani Fulani watazokubaliana (sio bidhaa zote), lengo hasa ikiwa ni kupunguziana viwango vya kodi katika bidhaa husika ili to stimulate trade, jo creation, GDP, n.k; Swali linalofuata ni je ni watanzania wangapi wenye uelewa juu ya jinsi gani PTA imekuwa in effect katika EAC na je inawapa fursa gani? Faida gani? Hasara gani? Changamoto gani? Pia je, Serikali ina mikakati gani ya kulinda uchumi wetu dhidi ya economic shocks zinazoweza kujitokeza?
Hatua ya Pili ni Free Trade Area (FTA) ambayo nayo ni a trade block baina ya nchi husika; FTA ina elements za PTA lakini FTA inaenda mbali zaidi kwani nchi wanachama hukubaliana kufuta kabisa kodi, import quotas katika bidhaa na huduma nyingi watazokubaliana (sio zote); Swali linalofuatia ni kwamba je - ni wananchi wangapi wenye uelewa juu jinsi gani FTA imekuwa in effect katika EAC na je inawapa fursa gani? Faida gani? Hasara gani? Changamoto gani? Pia je, Serikali ina mikakati gani ya kulinda uchumi wetu dhidi ya economic shocks zinazoweza kujitokeza?
Hatua ya tatu ya muungano wa kiuchumi ni Customs Union hapa nchi wanachama wanakubaliana kwa pamoja kuweka viwango sawa vya kodi kibiashara dhidi ya mataifa ambayo sio wanachama wa trade block yao; Hii hufanya mataifa nje ya trade block yenu yasibague wanachama wengine kutokana na wengine katika trade block yenu kuwa na viwango vikubwa vya kodi kwani kwa kawaida, nchi nje ya trade block yenu watakimbilia nchi zenye viwango vidogo vya kodi and vice versa holds; katika hili, iwapo Tanzania na nchi za SADC au EAC wangeamua kuwa na viwango sawa vya kodi, lakini hasa kukataa upuuzi wa tax exemptions kwa wawekezaji wanazopewa kwa miaka mitano (mfano rejea jinsi gani mahoteli makubwa yanavyobadili majina kila baada ya miaka mitano), tungekuwa katika nafasi bora zaidi kiuchumi. Swali linalofuata ni je watanzania wangapi wanaelewa fursa, hasara, faida na changamoto za mfumo huu katika jumuiya yetu ya Afrika Mashariki? Pia je, Serikali ina mikakati gani ya kulinda uchumi wetu dhidi ya economic shocks zinazoweza kujitokeza?
Hatua ya nne ni Common Market au Single Market katika hili, kunakuwa na common policies za uendeshaji biashara na regulations katika uendeshaji biashara, lakini hasa uzalishaji; Hapa pia kunakuwa na free movement ya factors of production (Labor, Capital, Services na Enterprises) baina ya wanachama wa trade block husika; Lengo kuu hapa ni kuondoa kila aina ya vikwazo vya kibiashara baina ya nchi wanachama vinavyotokana na jiografia (mipaka), kodi, technical /standards requirements n.k; Swali linalofuata ni je watanzania wangapi wanaelewa fursa, hasara, faida na changamoto za mfumo huu katika jumuiya yetu ya Afrika Mashariki? Pia je, Serikali ina mikakati gani ya kulinda uchumi wetu dhidi ya economic shocks zinazoweza kujitokeza?
Hatua ya Tano ni Economic & Monetary Union huu ni mchanganyiko wa hatua zote za awali hapo juu PLUS uanzishaji wa sarafu moja (common currency); Swali linalofuatia ni je - watanzania wangapi wanaelewa fursa, hasara, faida na changamoto za mfumo huu katika jumuiya yetu ya Afrika Mashariki? Pia je, Serikali ina mikakati gani ya kulinda uchumi wetu dhidi ya economic shocks zinazoweza kujitokeza? Monetary Union ni moja ya mijadala mikali hivi sasa ndani ya EAC
Hatua ya Sita ni Fiscal Union hatujafikia hatua hii lakini hapa maana yake ni muungano wa fiscal policies (kodi na matumizi ya mapato ya kodi) baina ya wanachama ambapo maamuzi kuhusu ukusanyaji kodi na matumizi ya fedha za walipa kodi yanakuwa centralized kupitia Benki Kuu moja that serves all members; mfano mzuri ni Federal System ya USA FRB; Swali linalofuatia ni je tukija fikia huko, watanzania wangapi wanaelewa fursa, hasara, faida na changamoto za mfumo huu katika jumuiya yetu ya Afrika Mashariki? Pia je, Serikali ina mikakati gani ya kulinda uchumi wetu dhidi ya economic shocks zinazoweza kujitokeza?
Hatua ya mwisho ni Full Integration ambayo inahusiana zaidi na Political Integration; Swali linalofuata ni je - watanzania wapo tayari kwa hili? Na ni wangapi wanaelewa fursa, hasara, faida na changamoto za hatua hii katika jumuiya yetu ya Afrika Mashariki?
Kwa mtazamo wangu, nadhani tukitumia framework hii kujadili lessons from EU kwa jumuiya yetu yaAfrika mashariki, tutakuwa katika nafasi nzuri zaidi ya kuelewa juu ya faida, hasara, changamoto na fursa mbalimbali za kiuchumi zinazotukabili sasa na zitazotukabili baadae katika muktadha huu wa EAC, hivyo kutupatia fursa nzuri zaidi ya kuja na mikakati mbalimbali ya kukabiliana na changamoto husika kwa ajili ya maendeleo yetu na ya vizazi vijavyo;