Tuna la kujifunza kutokana na ajali ya ferry Likoni

ibanezafrica

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
7,261
Reaction score
6,553
Ni ajali ya kusikitisha iliyochukua roho ya mama na mtoto wa miaka minne kwa gari yao kuserereka katika pantoni waliokua wakivuka.

Gha kusikitisha zaidi gari ile ilielea kwa takriban dakika ishirini mwishowe kuzama taratibu na kufunikwa kabisa na maji huku hakuna jitihada zozote zilizochukuliwa na mamlaka husika huko.

Cha kujifunza hapa ni wajibu wa vikosi vya uokoaji huwa wanafanya nini au wanasubiri kuokoa nini?

Kwa ushauri wangu kwa watu wa port Dar na hata Mombasa wajenge rescue centre jirani na sehemu wanaposhukia na kupandishia abiria kwa pande zote.yaani mfano hapa Dar ijengwe upande wa kigamboni na nyingine upande wa inland soko la ferry.katika vituo hivyo kuwe na ma divers wa kutosha hata kama ni 50 kuwe na Powerful cranes,Chains na hook za urefu na ukubwa mbalimbali,wajenge mashine kubwa zenye kuweza kuvuta kitu kizito kwa kutumia strong chains au hata zile kamba nene za marine,Kuwepo Rescue boats hata 6 na ambulances,wawe na taa za kutosha zenye mwanga mkali,ambazo zaweza kuwa movable.

Kwa kuwa na vituo kama hivi ambavyo vitakuwa 24hrs/7days a week hakika vingeokoa maisha ya wengi.

Tatizo afrika huwa hatuko aware na masuala ya Safety sijui kwanini..wenzetu walioendelea huwa wapo makini mno na usalama.kwa muda fulani niliokaa nje huwa nayaona mapungufu mengi sana hasa ya kiusalama hupenda kutoa ushauri lkn cjui wapi pa kutoa ushauri.

Ben. 0716399767
 
Hapa suala kubwa ni kuwa na Rescue boat kubwa ya kisasa. Au kuwe na Coast Guard na wawe na vifaa vya kisasa kuweza kufanya uokoaji.
 
Mbele na nyuma ya ferry kuna ile milango (Ramp) wakati wa kuondoka nahodha huwa anaupandisha na kuna wakati mwingine unakuwa upo flat na ferry inaanza kutembea.

Ushauri wangu kwa manahodha na operators zile ramp inabidi isogezwe mpaka mwisho hivyo italeta muinuko hata gari ikirudi nyuma haitoweza kuingia moja kwa moja labda iwe inapata nguvu ya engine kurudi nyuma.

Na kwa baharia aliyezamu inabidi awe anahakikisha lile geti la chuma la kuruhusu gari kupita na watu awe anafunga vizuri safari ikianza.
 
Hapa suala kubwa ni kuwa na Rescue boat kubwa ya kisasa. Au kuwe na Coast Guard na wawe na vifaa vya kisasa kuweza kufanya uokoaji.


Inaweza kuwepo lakini watumishi wake ni wale wa kujivuuuuta kama vile hawakupitia mafinzo, unakumbuka ule uokoaji wa yule mtoto kwenye dimbwi pale Mlimani city miaka ya 2007 au 08?

Waikoaji walikwenda na gari la zimamoto, walipofika pale wakachukua mti wakaanza kukoroga sehemu ya dimbwi, ndipo raia mmoja alipoona hao walikuwa wababaishaji akaamua kuzama mwenyewe majini kumtafuta maiti wao waokoaji wameduwaa pembeni
 
Kuna kipindi lilizama gari apo feri sidhan kama miaka minne imepita ndio maana kwa sasa huruhusiwi kukaandani ya gari ukishaingia kwenye kivuko


Hiyo itakuwa ya pili, kuna mwaka huko nyuma ilizama nyingine ikiwa na mzigo wa mbao
 
Uzembe au kutokuchukua action ndio kilichopo
Hivi gari inazama vile halsfu msemaji wa port kenya anasema wacha kwanza tujaribu kwa juhudi zetu kuokoa tukishindwa tutaomba msaada south africa...hz ni jokes !
Pale nungwi meli ikazama wakajaribu kidogo kufanya uokozi usiku kiongozi mmoja akasikika akisema twendeni kulala tutakuja kuendelea kesho saa hizi ishakua giza !! This was a shame...watu bado wanahangaikia roho zao ndani ya chombo ati mnaenda kulala kwanza.
 
Rescue center ipo hapo ferry kwenye control tower
Pale ni Marine Rescue Coordination Centre (MRCC) ni kituo cha uokozi wao wanapokea taarifa ya ajali au hatari kwa kupitia Vifaa kama EPIRB,SART na Radio Communication kutoka kwenye meli na kutoa oda kwa waokoaji.

Hapo kwenye ilo gorofa hakuna diver wote wavaa suti.

Na hao wa Likoni ferry ilibidi wazamishe kile kifaa kinaitwa Emergency Position Indicating Radio Beacon (EPIRB) taarifa ingevikia vyombo vyote vya majini au kama ferry zao zina Radio wangepinga Distress Call ya Man Overboard meli na boat zote zingesogea kutoa msaada.
 
Sie waafrika sijui ni nini huwa nawaza huenda kuna baadhi ya chip kichwani mwa mwafrika mungu alizichomoa pamebaji empty slots tu
 
Hiyo itakuwa ya pili, kuna mwaka huko nyuma ilizama nyingine ikiwa na mzigo wa mbao
Kinachotakiwa abiria wasikae ndani ya magari kwenye ferry.Likoni Huwa nawashangaa hata ukiwa kwenye basi mnashushwa abiria wachache wengine wanabaki ndani ya basi.Wasafiri waenda Mombasa tunalijua hilo.Ninachowasifu wakenya ferry yao Likoni unapanda bure hulipii hata Mia tofauti na zetu.
 
Kutolipa hata shilingi hakumaanishi ajali haiwahusu
Ajali ya kujitakia kwa nini Mtu ukae kwenye gari ukiwa ndani ya ferry ni ujinga.Ndani ya gari hakuna maboya ya kujiokoa ndio maana watu hutakiwa watoke kwenye magari wakae kwenye ferry ikianza mfano kuzama unadaka boya unaelea unanusurika.Iwe bure au kulipia hutakiwi kukaa ndani ya gari ukiwa kwenye feri.
 
Pole yao sana...

Kwani hizo ferry hazina ukingo imara wa kuzuia vyombo vya moto kuserereka?


Cc: mahondaw
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…