mngony
JF-Expert Member
- Jul 27, 2012
- 5,555
- 6,972
Japo ukweli unabaki wewe mwenyewe ndio unawajibika kwa afya yako, hivyo wewe ndio muamuzi wa jambo lolote kuhusiana na afya yako na wala mtu mwingine asikuchagulie linalohusiana na afya yako
Kufutia kuumwa kama tulivyoambiwa na familia ugonjwa wa changamoto ya kupumua, Mama yetu Mghwira Mungu alimpenda zaidi siku kadhaa nyuma, lakini tukumbuke mwaka jana mwezi wa nne wakati wa wimbi la pili alijitangaza kuumwa na hatimae kupona corona na hata kutoa wimbo kushukuru Mungu.
Lakini mwaku huu, wimbi la tatu la maambukizi ameumwa tena lakini Mungu alimpenda zaidi
Nitoe pole kwa familia, ndugu na wote walioguswa
Japo sio vizuri lakini tunajifunza kuwa kama umri umeenda sana, au una magonjwa ya muda mrefu kama vile Sukari na mengine yenye kudhoofisha mwili na kupunguza kinga ni vizuri ukachukua tahadhari kubwa kadri uwezavyo kwa sababu ukishakuwa katika hiyo hali ni rahisi kuumwa sana na hata ikatokea ukapona maana yake wimbi likija tena uwezekano wa kupata na kuumwa sana( kupata numonia ya corona) unakuwa uko palepale, tena inakuwa hatari zaidi kwa sababu athari za corona kufika kwenye mapafu huwa ni zinabaki muda mrefu hata baada ya kupona
Kama uko katika hayo makundi hatarishi, achana na hizi siasa chagua mwenyewe mustkabali wa afya yako chukua tahadhari mwenyewe, usije ukachukua ushauri wa mtu mwenye 20s to 40s ambaye shida yeyote kiafya ambaye akipata maambukizi anaishia na kifua na labda na homa siku 3 anapona ukafata wewe mwenye 40s na kuendelea huku ukiwa na magonjwa kama sukari n.k
Tukumbuke haya maambukizi yataendelea kuja wimbi baada ya wimbi, yanakuja yanasambaa kwa kasi na kuathiri wengi baadae hali inatulia na kuanza tena kwa hiyo ni suala muda mrefu
Wewe uliye kundi hatari chukua tahadhari zote hata ukiona kuchanja ni muhimu kwako chanja ukiona haina acha. Na wengine ambao hatuko kundi la hatari tuwalinde walio kundi hatari