Umesahau kuna wabunge wa vitu maalum na kwa watu maalum! Kuna wale wanyonyaji/kupe kutoka Zanzibar! Kuna wabunge 10 wanaoteuliwa kwa matakwa ya mtu mmoja! Yaani unajisikia tu na kwa utashi wako kuteua watu 10 kwenda kulipwa mamilioni ya shilingi kila mwezi!!
Na bado mwaka huu kuna majimbo mapya yameongezwa ili tu kuwafurahisha/kuwabeba watu fulani fulani!
Hii nchi inaihitaji ile Katiba ya Wananchi ili kuondoa haya mauza uza ya kuigeuza nchi kuwa shamba la bibi.
Hii nchi kwa umaskini wetu huu tulitakiwa kuwa na wabunge wasiozidi 150.
Tungeokoa mabillion ya pesa yakaenda kwenye kilimo na viwanda hasa kuwashirikisha vijana wetu.