Tuna Miti kila Mkoa! Kwanini Wateja wa TANESCO wakose nguzo na kutakiwa kusubiri siku 60?!

BOB LUSE

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2014
Posts
3,813
Reaction score
3,430
Nimelipia nguzo ili niwekewe Mita,mita pia nimelipa, nimekwamishwa na nguzo hakuna!
Mita zinazalishwa na kuagizwa toka nje,zipo za kutosha,shida nguzo,naambiwa Material hakuna,nina muda wa kusubiri mpaka siku Sitini!

Kama TANESCO hamna ufanisi katika kujua mahitaji yenu kwanini muendeleze Monopoly ya Supply ya nguzo, Kwanini msishughulike na Quality,tuwe na supply wengi wa nguzo moja kwa moja kwa Wateja?

Mteja akae gizani siku zote hizo kwa kushindwa ku project mahitaji yenu? Tunaomba elimu tulizopata na vyeo vitoe ufumbuzi wa shida za wananchi.

Mnakawaida ya kuja na majibu ya jumlajumla humu .hii ni real life experience niliyoshare
 
Nchi yetu inachangamoto sana.
Sisi ambao tumenyooka Kidogo huwa tunaumizwa sana na haya Mambo.
Mtu unatamani usingezaliwa Tanzania.

"Tusiseme hatuna matatizo kwa kuyaficha matatizo yetu wenyewe. Ujasiri wa taifa hauko katika kuficha kasoro zake, bali katika kuzikubali na kuzitatua." Mwalimu J K Nyerere.
 
Cha ajabu miaka iliyopita eti walikua wanatoa nguzo SA tunalipishwa karibu nguzo moja Tsh 637,000 aisee wahuni sio watu nguzo zetu hizo hizo walikua wanatuuzia kwa bei ya kutoka nje na hakuna hata mmoja aliewajibika kwa huo wizi wa miaka yote.
 
Habari ya muda huu wakuu,
Kwa uelewa wangu ni kwamba kila ofisi ya Tanesco inakua na stoo yake kuu ya kutunzia Nguzo na kila bada ya muda idara ya Luku huandika mahitaji ya Nguzo zinazohitajika kutokana na mahitaji ya maombi na vipimo hasa kwa wateja wanaohitaji Nguzo mpya kuwekewa Umeme.
Kutokana na Hilo hapo juu bado kunakua na muendelezo wa wateja wapya kuomba kuwekewa Umeme na pia ndani ya hizo siku bado Kuna utaratibu wa kiofisi hufanyika mpaka mteja husika kufikiwa.
 
Nimelipia nguzo ili niwekewe Mita,mita pia nimelipa, nimekwamishwa na nguzo hakuna!
Mita zinazalishwa na kuagizwa toka nje,zipo za kutosha,shida nguzo,naambiwa Material hakuna,nina muda wa kusubiri mpaka siku Sitini!

Kama TANESCO hamna ufanisi katika kujua mahitaji yenu kwanini muendeleze Monopoly ya Supply ya nguzo, Kwanini msishughulike na Quality,tuwe na supply wengi wa nguzo moja kwa moja kwa Wateja?

Mteja akae gizani siku zote hizo kwa kushindwa ku project mahitaji yenu? Tunaomba elimu tulizopata na vyeo vitoe ufumbuzi wa shida za wananchi.

Mnakawaida ya kuja na majibu ya jumlajumla humu .hii ni real life experience niliyoshare
Habari ndugu mteja, asante kwa kuwasiliana nasi,

Pole kwa changamoto hiyo, tunaomba mawasiliano yako au namba ya ombi lako tuweze kujua sababu ya mkwamo huo na kuwezesha huduma kukufikia.

Dhamira yetu ni kuwahudumia wateja wetu kwa wakati, lakini kuna wakati inaweza kutokea changamoto tunapaswa kukufahamisha kuhusu huduma uliyolipia.

Asante.^FL
 
Habari ya muda huu wakuu,
Kwa uelewa wangu ni kwamba kila ofisi ya Tanesco inakua na stoo yake kuu ya kutunzia Nguzo na kila bada ya muda idara ya Luku huandika mahitaji ya Nguzo zinazohitajika kutokana na mahitaji ya maombi na vipimo hasa kwa wateja wanaohitaji Nguzo mpya kuwekewa Umeme.
Kutokana na Hilo hapo juu bado kunakua na muendelezo wa wateja wapya kuomba kuwekewa Umeme na pia ndani ya hizo siku bado Kuna utaratibu wa kiofisi hufanyika mpaka mteja husika kufikiwa.
Habari, ndugu mteja.

Tunashukuru kwa maelezo na uelewa wako kuhusu utaratibu wa utoaji huduma ya kuunganisha umeme kwa wateja wapya.

TANESCO ina utaratibu wa kupanga na kusimamia mahitaji ya vifaa vya kuunganishia umeme, ikiwemo nguzo, kwa kuzingatia mahitaji ya wateja, matokeo ya upimaji wa maeneo husika na upatikanaji wa vifaa.

Ni kweli kwamba maombi ya kuunganishiwa umeme yanaendelea kupokelewa wakati taratibu za kiutendaji, kiufundi na ugawaji wa vifaa zikiendelea kutekelezwa. Hata hivyo, muda wa kumfikia kila mteja unaweza kutofautiana kulingana na hatua iliyofikiwa katika ombi lake.

TANESCO inaendelea kufanya jitihada za kuhakikisha wateja wanapatiwa huduma kwa kuzingatia taratibu zilizowekwa.

Asante. ^FL
 
Nimelipia nguzo ili niwekewe Mita,mita pia nimelipa, nimekwamishwa na nguzo hakuna!
Mita zinazalishwa na kuagizwa toka nje,zipo za kutosha,shida nguzo,naambiwa Material hakuna,nina muda wa kusubiri mpaka siku Sitini!

Kama TANESCO hamna ufanisi katika kujua mahitaji yenu kwanini muendeleze Monopoly ya Supply ya nguzo, Kwanini msishughulike na Quality,tuwe na supply wengi wa nguzo moja kwa moja kwa Wateja?

Mteja akae gizani siku zote hizo kwa kushindwa ku project mahitaji yenu? Tunaomba elimu tulizopata na vyeo vitoe ufumbuzi wa shida za wananchi.

Mnakawaida ya kuja na majibu ya jumlajumla humu .hii ni real life experience niliyoshare
Maajabu ya BONGO! Ni kama ukosefu wa maji wakati tuna aquifer kila kona NCHINI!
 
Cha ajabu miaka iliyopita eti walikua wanatoa nguzo SA tunalipishwa karibu nguzo moja Tsh 637,000 aisee wahuni sio watu nguzo zetu hizo hizo walikua wanatuuzia kwa bei ya kutoka nje na hakuna hata mmoja aliewajibika kwa huo wizi wa miaka yote.
Habari ndugu mteja, tunaomba kujua changamoto yako kwa msaada zaidi.

Huduma ya kuunganisha umeme ni huduma inayohitaji miundombinu na kadri umbali unavyokuwa mkubwa mahitaji ya vifaa pia yanatofautiana.

Hata hivyo hakuna wizi wowote, malipo yoyote unalipia kwa namba ya malipo yaani (control number).

Pia hakuna bei kama hiyo uliyotaja kwenye hoja yako.

Taarifa zangu zipo kwenye ansad za Bunge na watu walitimuliwa kazi kwa huo wizi labda kama umeingia kazini juzi..
 
Ila ni kama hata hizo siku 60 hazitimii mkuu
 
Nimelipia nguzo ili niwekewe Mita,mita pia nimelipa, nimekwamishwa na nguzo hakuna!
Mita zinazalishwa na kuagizwa toka nje,zipo za kutosha,shida nguzo,naambiwa Material hakuna,nina muda wa kusubiri mpaka siku Sitini!

Kama TANESCO hamna ufanisi katika kujua mahitaji yenu kwanini muendeleze Monopoly ya Supply ya nguzo, Kwanini msishughulike na Quality,tuwe na supply wengi wa nguzo moja kwa moja kwa Wateja?

Mteja akae gizani siku zote hizo kwa kushindwa ku project mahitaji yenu? Tunaomba elimu tulizopata na vyeo vitoe ufumbuzi wa shida za wananchi.

Mnakawaida ya kuja na majibu ya jumlajumla humu .hii ni real life experience niliyoshare
Habari ndugu mteja wetu,

Pole kwa usumbufu uliyotokea.

Kuhusu hoja yako ya kusubiri nguzo siku 60 wakati miti ipo kila Mkoa, naomba kufafanua kitaalamu kama ifuatavyo:

1. Kwanini nguzo inachelewa wakati mita ipo?
Siyo kila mti una sifa ya kuwa nguzo ya umeme, hizi nguzo unazoziona zinapitia mchakato hadi kuwa nguzo kamili ya kutumika kusambaza umeme. Ndiyo maana kuna miti maalum tunayotumia kutengenezea nguzo.

2. kwenye kuunganisha wateja kuna umbali unaozingatiwa na kila umbali kuna siku maalum za kuhakikisha mteja amefikiwa. Hata hivyo kama ikitokea tupo nje ya muda tunalazimika kukujulisha kama ipo changamoto inayopelekea taasisi kuchelewa na wala siyo adhabu kwa mteja wetu.

3.Kwanini hamuachi Monopoly ya nguzo?

Sheria ya Umeme Sura ya 131 inatupa TANESCO jukumu la usambazaji pekee ili kulinda usalama wa gridi ya Taifa.

Mtu binafsi anaweza kununua nguzo na kutumia mkandarasi kumjengea njia ya umeme lakini lazima Shirika lisimamie mchakato wote kwakua sio kila nguzo inafaa kwa kazi hiyo hivyo lazima kusimamia ubora (Quality) ili kuzuia madhara yanayoweza kutokea kama kuanguka kwa kuoza na kusababisha madhara, dhima ya kisheria ni ya TANESCO.

Hata hivyo kama taasisi tumejipanga kuhakikisha wateja wetu wanapata huduma kwa wakati ingawa hata gharama za kulipia kuunganisha umeme zilizopo sio gharama halisi kwakua bei hizo kwanza niza zamani sana lakini pia zililenga watu walio na kipato kidogo hivyo serikali kutambua hilo ikaona iweke bei ambayo mwananchi atachangia tu na wala sio bei halisi .
Mfano gharama ya kuunganisha umeme umbali wa meter 70 ambayo ni nguzo moja ni 516,000 wakati bei halisi ni 1,500,000.

Bei ya kuunganisha umeme umbali meter 30 ni Tzs 320,960 bei halidi ni Tzs 546,765

Asante.^FL
 
Back
Top Bottom