Nimelipia nguzo ili niwekewe Mita,mita pia nimelipa, nimekwamishwa na nguzo hakuna!
Mita zinazalishwa na kuagizwa toka nje,zipo za kutosha,shida nguzo,naambiwa Material hakuna,nina muda wa kusubiri mpaka siku Sitini!
Kama TANESCO hamna ufanisi katika kujua mahitaji yenu kwanini muendeleze Monopoly ya Supply ya nguzo, Kwanini msishughulike na Quality,tuwe na supply wengi wa nguzo moja kwa moja kwa Wateja?
Mteja akae gizani siku zote hizo kwa kushindwa ku project mahitaji yenu? Tunaomba elimu tulizopata na vyeo vitoe ufumbuzi wa shida za wananchi.
Mnakawaida ya kuja na majibu ya jumlajumla humu .hii ni real life experience niliyoshare
Habari ndugu mteja wetu,
Pole kwa usumbufu uliyotokea.
Kuhusu hoja yako ya kusubiri nguzo siku 60 wakati miti ipo kila Mkoa, naomba kufafanua kitaalamu kama ifuatavyo:
1. Kwanini nguzo inachelewa wakati mita ipo?
Siyo kila mti una sifa ya kuwa nguzo ya umeme, hizi nguzo unazoziona zinapitia mchakato hadi kuwa nguzo kamili ya kutumika kusambaza umeme. Ndiyo maana kuna miti maalum tunayotumia kutengenezea nguzo.
2. kwenye kuunganisha wateja kuna umbali unaozingatiwa na kila umbali kuna siku maalum za kuhakikisha mteja amefikiwa. Hata hivyo kama ikitokea tupo nje ya muda tunalazimika kukujulisha kama ipo changamoto inayopelekea taasisi kuchelewa na wala siyo adhabu kwa mteja wetu.
3.Kwanini hamuachi Monopoly ya nguzo?
Sheria ya Umeme Sura ya 131 inatupa TANESCO jukumu la usambazaji pekee ili kulinda usalama wa gridi ya Taifa.
Mtu binafsi anaweza kununua nguzo na kutumia mkandarasi kumjengea njia ya umeme lakini lazima Shirika lisimamie mchakato wote kwakua sio kila nguzo inafaa kwa kazi hiyo hivyo lazima kusimamia ubora (Quality) ili kuzuia madhara yanayoweza kutokea kama kuanguka kwa kuoza na kusababisha madhara, dhima ya kisheria ni ya TANESCO.
Hata hivyo kama taasisi tumejipanga kuhakikisha wateja wetu wanapata huduma kwa wakati ingawa hata gharama za kulipia kuunganisha umeme zilizopo sio gharama halisi kwakua bei hizo kwanza niza zamani sana lakini pia zililenga watu walio na kipato kidogo hivyo serikali kutambua hilo ikaona iweke bei ambayo mwananchi atachangia tu na wala sio bei halisi .
Mfano gharama ya kuunganisha umeme umbali wa meter 70 ambayo ni nguzo moja ni 516,000 wakati bei halisi ni 1,500,000.
Bei ya kuunganisha umeme umbali meter 30 ni Tzs 320,960 bei halidi ni Tzs 546,765
Asante.^FL