Hao waliokupa ushauri waulize wana watoto wangapi? Mtoto aendelee kunyonya tena bila shida yeyote. Mpe mama vyakula bora vya kutosha ili apate nguvu ya kulea viumbe vyote viwili. Mtoto anyonye mpaka wiki kama 5 kabla ya mama kujifungua.
Aachishwe ili maziwa ya mama yatengeneze kitu kinaitwa colostrum. Hii ni kinga ya huyo ajaye. Baada ya hapo mlishe mtoto wako vyakula vizuri. Maziwa ya kopo si mazuri kwani wengi wetu hata kuyatengeneza tayari kwa mtoto hatujui ndo maana watoto huharisha.
Pili, unataka watoto wangapi, zaa kila mwaka halafu funga kizazi namba yako ikitosha.
Mbona unavyomgegeda hukuomba ushauri?, kwanini hukuchukua tahadhari mapema? Mlishe mkeo vyakula bora tu hapo ili aimarike afya yake aweze kuhudumiaviumbe vyote viwili
Kiukweli nimefurahia sana ushauri wako, ila wengine nadhani wapo ili kuwakatisha wenzao tamaa, any way mungu akubariki sana ndg yangu!
Usiogope, Mimi Kama Mchungaji Knsn Kwetu hapa Ruaha Kilombero ilitokea iyo mwaka jana, mama mwenye mtoto wa miezi 3 akapata mimba, Akaenda Knsn Kuomba Ushauri na akafanyiwa huduma na akapewa agizo kuwa aendelee tu kumnyonyesha huyo mtoto bila tatzo.
Nna amefanya ivyo hadi mwisho hadi amejifungua na sasa ananyonyesha wote wawili, kwa iyo kama unaamin naomba nitumie namba yako ya cm nitawaombea na mama ataendelea kunyonyesha. usiogope mungu anawapenda.
Habari za ijumapili wakuu! Kwasasa tuna mtoto wa kike mwenye umri wa miezi saba, juzi mama mtoto wangu kafanya vipimo kakutwa na mimba ya wiki tatu, naombeni ushauri hasa namna ya kuhandle hali hii ili kulinda afya ya mwanangu anaenyonya. Mungu awabariki sana!