Tuna mtoto wa miezi saba, mke wangu mjamzito. Ushauri pliiiz!

Tuna mtoto wa miezi saba, mke wangu mjamzito. Ushauri pliiiz!

Mwamgunda

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2012
Posts
247
Reaction score
48
Habari za Jumapili wakuu!

Kwasasa tuna mtoto wa kike mwenye umri wa miezi saba, juzi mama mtoto wangu kafanya vipimo kakutwa na mimba ya wiki tatu. Naombeni ushauri, hasa namna ya kuhandle hali hii ili kulinda afya ya mwanangu anaenyonya. Mungu awabariki sana!
 
Mbona unavyomgegeda hukuomba ushauri?, kwanini hukuchukua tahadhari mapema? Mlishe mkeo vyakula bora tu hapo ili aimarike afya yake aweze kuhudumiaviumbe vyote viwili
 
Kwa mtoto wa miez 7 haachishwe kunyonya mara moja then maziwa ya kopo.
 
Mwamgunda

Kwahyo uliendelea kumgegeda bila yeye kutumia uzazi wa mpango? (sindano au vidonge).. Huyo mkeo hana ndugu? Maana baada ya kujifungua kawaida anavutwa pembeni na kupewa mawaidha ya kujikinga. Mimi saivi najishindia tu...maana wife kachoma hiyo ya miezi 3...baasi raaaaha!
 
Last edited by a moderator:
Hamna tatizo hapo huyo first born wako muachishe then aanze kutumia vyakula vya formula
 
Hao waliokupa ushauri waulize wana watoto wangapi? Mtoto aendelee kunyonya tena bila shida yeyote. Mpe mama vyakula bora vya kutosha ili apate nguvu ya kulea viumbe vyote viwili. Mtoto anyonye mpaka wiki kama 5 kabla ya mama kujifungua.

Aachishwe ili maziwa ya mama yatengeneze kitu kinaitwa colostrum. Hii ni kinga ya huyo ajaye. Baada ya hapo mlishe mtoto wako vyakula vizuri. Maziwa ya kopo si mazuri kwani wengi wetu hata kuyatengeneza tayari kwa mtoto hatujui ndo maana watoto huharisha.
Pili, unataka watoto wangapi, zaa kila mwaka halafu funga kizazi namba yako ikitosha.
 
Kijana usihofu cha muhimu lishe mimi yalishanikuta Mtoto Ana miezi nane mimba tena, tukaenda kwa docta wa watoto akatushauri vizuri baada YA hapo mtoto alikuwa vizuri na mwingine akazaliwa bila tatizo leo ni wakubwa Hadi raha mmoja miaka 14 mwingine 13 na wana afya nzuri
 
Hao waliokupa ushauri waulize wana watoto wangapi? Mtoto aendelee kunyonya tena bila shida yeyote. Mpe mama vyakula bora vya kutosha ili apate nguvu ya kulea viumbe vyote viwili. Mtoto anyonye mpaka wiki kama 5 kabla ya mama kujifungua.

Aachishwe ili maziwa ya mama yatengeneze kitu kinaitwa colostrum. Hii ni kinga ya huyo ajaye. Baada ya hapo mlishe mtoto wako vyakula vizuri. Maziwa ya kopo si mazuri kwani wengi wetu hata kuyatengeneza tayari kwa mtoto hatujui ndo maana watoto huharisha.
Pili, unataka watoto wangapi, zaa kila mwaka halafu funga kizazi namba yako ikitosha.

Kiukweli nimefurahia sana ushauri wako, ila wengine nadhani wapo ili kuwakatisha wenzao tamaa. Anyway Mungu akubariki sana ndg yangu!
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Mbona unavyomgegeda hukuomba ushauri?, kwanini hukuchukua tahadhari mapema? Mlishe mkeo vyakula bora tu hapo ili aimarike afya yake aweze kuhudumiaviumbe vyote viwili

Si vyema kusema hivyo, haya mambo yanawatokea weng na si kwa kutaka.
 
Kiukweli nimefurahia sana ushauri wako, ila wengine nadhani wapo ili kuwakatisha wenzao tamaa, any way mungu akubariki sana ndg yangu!

Usitishwe na wanaosema bila kuwa na experience yeyote. Tunao watoto na tulijikuta ka weye lakini hatuku babaika. Mtunze mama vizuri tu wala hakuna madhara yeyote. Mbona mbuzi jike anakufa tunamnyonyesha mtoto kwa mbuzi mwingine. Ni mtu tena mamake.
 
Usiogope, Mimi Kama Mchungaji Knsn Kwetu hapa Ruaha Kilombero ilitokea iyo mwaka jana, mama mwenye mtoto wa miezi 3 akapata mimba, Akaenda Knsn Kuomba Ushauri Na akafanyiwa huduma na akapewa agizo kuwa aendelee tu kumnyonyesha huyo mtoto bila tatzo,

Na amefanya ivyo hadi mwisho hadi amejifungua na sasa ananyonyesha wote wawili, kwa iyo kama unaamin naomba nitumie namba yako ya cm nitawaombea na mama ataendelea kunyonyesha. usiogope mungu anawapenda.
 
Usiogope, Mimi Kama Mchungaji Knsn Kwetu hapa Ruaha Kilombero ilitokea iyo mwaka jana, mama mwenye mtoto wa miezi 3 akapata mimba, Akaenda Knsn Kuomba Ushauri na akafanyiwa huduma na akapewa agizo kuwa aendelee tu kumnyonyesha huyo mtoto bila tatzo.

Nna amefanya ivyo hadi mwisho hadi amejifungua na sasa ananyonyesha wote wawili, kwa iyo kama unaamin naomba nitumie namba yako ya cm nitawaombea na mama ataendelea kunyonyesha. usiogope mungu anawapenda.

Maombi hayabadili kitu chochote.
 
Yaan hii ndo stail ya siku hizi, mnazaa fasta then mnapumzika hata 5yrs mfanya maendeleo na kuanza kusomesha
Baada ya hapo ndo uzazi unaweza endelea, yaan hiyo safi sana
 
Mkuu hapo cha msingi ni lishe bora tu...kwa mama na mtoto...nadhalia ya kubemenda kitaalam haipo
 
Habari za ijumapili wakuu! Kwasasa tuna mtoto wa kike mwenye umri wa miezi saba, juzi mama mtoto wangu kafanya vipimo kakutwa na mimba ya wiki tatu, naombeni ushauri hasa namna ya kuhandle hali hii ili kulinda afya ya mwanangu anaenyonya. Mungu awabariki sana!

Mkuu,

Usiumize kichwa, acha stori za mtaani. Mimi ni shuhuda namba moja wa hiyo kitu, wakati mwanangu wa kwanza akiwa na miezi 6,waifu alishika ujauzito wa mwanetu wa pili. Tulichanganyikiwa kidogo lakini baaada ya kupata ushauri wa wataalam na kuufuata, leo hii tuna watoto wawili, yule wa kwanza wa kiume na huyu wa pili wa kike.

Mwanetu wa kwanza alinyonya kama kawaida hadi alipofikisha umri wa mwaka mmoja ndio tukamuachisha. Kitaalamu ni kwamba atleast huyo wa pili aachiwe ziwa miezi mitatu kabla. So,wanetu wapo na wana afya sana. Tatizo ni kwamba tu mimba imekuja pasipo matarajio hivyo mjiandae na malezi dabo dabo,lakini mengineyo yote shwari kabisa.
 
Hongera sana ndugu. Hizo ni challenge tu za maisha. Mpeleke mkeo clinic mapema sana ili mpate ushauri wa kitaalamu. Ila kiufupi hakuna kitu kama kubemenda. Mke ale vizuri na anyonyeshe mtoto hadi mwisho. Hao wanaoshangaa kwenye familia zetu wapo watu wamepishana umri mwaka mmoja, kwani ilitokeaje?

Kila la kheri
 
Wala usipanic. You are all gonna be okay.

First things first. Kumuachisha bi dada nyonyo. Na ku supplement nyonyo. Ushauri wa maziwa ya kopo nashindwa kukupa kwa sababu sijawahi kutumia ila msosi wa mtoto unatakiwa umtosheleze.

On the other hand kumnyonyesha mtoto si kumshibisha tu. Kuna psychological factor na inabidi bonding ya mama na mtoto izidi hasa kipindi hiki. Usipoelewa hapa utanijulisha.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Back
Top Bottom