Tuna safari ndefu sana kuboresha huduma za afya

jimmyfoxxgongo

JF-Expert Member
Joined
Jan 23, 2013
Posts
5,352
Reaction score
9,329
Habari wanajamvi

Nchi yetu ni miongoni mwa mataifa yenye huduma mbovu za afya kupindukia

Nasema mbovu kupindukia kwa sababu nimekaa katika field hii kwa muda ingawa sio sana na kwa namna fulan nna uelewa na mambo mengi

Ili uboreshe huduma za afya kwa kiwango kikubwa ni lazima kwanza uboreshe PRIMARY HEALTH CARE kwa maana ya dispensaries au vituo vya afya vitoe huduma kwa hali nzuri to their limit hapa namaanisha kama wanatibu malaria watibu kwa usahihi sana

Namaanisha hv vituo vya afya vitoe huduma nzuri katika matibabu kulingana na hadhi yao

Lakin kwa bahati mbaya katika vituo hv hali haipo hiv.Huduma za vituo vya afya ni mbaya kuliko unavyofikiria

Taasis hizi( vituo vya afya) totally havina wataalam wa maabara kwa kiwango kikubwa wanaofanya kazi katika maabara za vituo hv ni attendant nurses.

Katika nchi kuna watu wengi wanaopoteza maisha sio kwa sababu tu siku zao zmefika ila ni kwa sababu ya huduma mbovu za afya huko mitaan hasa katika primary health cares.

Kitu kingine ni kukosekana kwa userious wa nchi yetu inawezekana vp nchi ina bodi za kumonitor taasis za afya kukawa na watu wanaofanya kazi wasio na taaluma au wasio na vibali.

Kwa mfano kwa Dar es salaam kuna vituo kibao vya afya ie dispensaries ambazo hazina usajili watu wanaofanya kazi kule sasa ni kichekesho.

Mfano wa pili ni katika jiji hili hili la Dar hospital kubwa zaidi ya 70% hazina sifa ya kuwa hospita plus wafanya kazi wake ni magumash na ndizo hospital ambazo mnaziamini sana.


Nawasilisha
 

Tunasitisha kuajiri mpaka tutakapomaliza swala ya uhakiki wa watumishi hewa.
 


Kwa sasa serikali haina uwezo wa kuboresha huduma za afya. Inashughulika na kuua demokrasia kwanza ikiwa ni sambaba na kuhamia dodoma. Hayo maswala ya Afya siyo kipaumbele chetu. Mkiendlea kulalamika, tunawakamta kwa uchochozi!.
 
Kwa sasa serikali haina uwezo wa kuboresha huduma za afya. Inashughulika na kuua demokrasia kwanza ikiwa ni sambaba na kuhamia dodoma. Hayo maswala ya Afya siyo kipaumbele chetu. Mkiendlea kulalamika, tunawakamta kwa uchochozi!.

Mkuu hili suala ni gumu sana serikali inapaswa kubebeshwa msalaba kwa sababu ya kushindwa kuwa na mifumo imara ya usimamizi
 
Mkuu hili suala ni gumu sana serikali inapaswa kubebeshwa msalaba kwa sababu ya kushindwa kuwa na mifumo imara ya usimamizi

Umesema kweli kiongozi. Tatizo ninadhani halianzii kwenye usimamizi. Linaanzia kwenye nia ya dhat ya kuinua ustawi wa Watanzania ambay inafuatiwa na mipango madhubuti yenye vipaumbele sahihii. Dhamira ya dhati haipo na ndiyo sababu utaona hata wabunge wao wako kichama zaidi. Wanakwenda bungeni kutetea chama badala ya wananchi. Wanapitisha budget ya ovyo haijawahi kutokea. Serikali inakosea hawana uwezo wa kuikosoa zaidi ya kujinafikisha. Wao wakiugua wanakimbizwa India kama Hindu Mandal.

Sisi tukiumwa tunakusanywa kama kuku mawodini ambako hata oxygen hakuna. Tunapukutika kama kuku wa kideli. Wakati huo huo serikali haina hata maono ya kuboresha uhai wetu, inajivalisha kinga sugu hata isikosolewe kusudi ifanye itakalo!.
Wakati tunakufa kwa kukosa oxygen na dawa mahospitalini, wao wanatumia mabilioni ya fedha kuhamia Dodoma.

Ni kweli kuhamia Dodoma kunaweza kuwa muhimu kwa maendeleo ya taifa. Lakini kuna uharaka wa namna hiyo? Kwamba inahamishwa serikali kwenye mazingira magumu kiuchumi namna hii, kwa budget ya dharura ambayo hata idhini ya bunge haina, ni kwa uharaka gani uliopo? Kuna vita kwamba tunahitaji kutunza serikali yetu mahala salama zaidi?

Kuna mwakani, mwaka keshokutwa, n.k. Kwa nini hili jambo liwe na uharaka bila kuzingatia maswala ya uhai wa Watanzania?

Nhi haiwezi kuongozwa kwa hisia za mtu mmoja. Hata watemi wa kale walikuwa na mabaraza ya wazee kuwasaidia katika maamuzi mbali mbali. Labda kwa sababu walikuwa wamesomea uongozi kwa uhalisia zaidi kuliko hawa wa mwendo kasi.

Usiku mwema.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…