Tuna watoto 4, wote kwa operesheni, mimba ya 5 (na mke alishafunga kizazi)

Tuna watoto 4, wote kwa operesheni, mimba ya 5 (na mke alishafunga kizazi)

Kabla hujaamua pata ushauri wa madaktari bingwa zaidi pale muhimbili (Dr. Kamugisha, Dr. Thomas nk) Aghakhan (Dr. Kaguta, na wengineo,) kiufupi nenda kwa wataalamu wa kina mama,hao ndo wanaweza kukupa majibu sahihi zaidi.fanya hivo mapema mkuu!
 
Pole sana. Nashauri utafute second opinion hasa kwa daktari bingwa wa wanawake!
 
Habari wadau,
"mimi na mke wangu tuko kwenye ndoa mwaka wa 17 sasa na tumejaaliwa kupata watoto wanne wote wa kike. kutokana na uzazi wa mke wangu kujifungua kwa operesheni mara kwa mara madaktari hosp ya mwana nyamara walitushauri kuwa mke wangu afunge kizazi kwani mimba zaidi ya nne kwa operesheni itahatarisha uhai wake na mtoto pia endapo ataendelea kuzaa. kweli tulikaa na mke wangu japo tulitaka kuendelea kuzaa walau tupate mtoto wa kiume tukaona ni vizuri kufuata ushauri wa madaktari na kufanya kama walivyotushauri kwa kufunga kizazi.
mwezi na siku na kadhaa zilizopita mke wangu alijisikia vibaya atukutilia maanani sana japo dalili zilikuwa ni za ujauzito kwani tuna miaka minne toka alipojifungua na kufunga kizazi, lakini hali hiyo iliendelea mpaka tulipoenda hospitali na kugundulika ana ujauzito wa miezi 3 na manesi walisema tayari hiyo mimba ni kubwa na kutokana na mishono aliyoshonwa tayari ni tatizo na kwa kifupi haitawezekana kujifungua salama eidha mtoto afe mama apone au mama afe mtoto apone
nilipopata hizi habari nilishtuka na kuhuzunika sana.
nakuja mbele yenu wanajamvi mnipe ushauri mwenye uzoufu na masuala kama haya naamini kabisa inawezekana madaktari hawakufanya kazi yao ipasavyo katika kufunga kizazi lakini tayari tatizo limeshatokea, je tuuwe kiumbe au kilichopo tumboni au tufanyaje?"
ushauri tafadhari.

kwa kawaida ni mama kwanza .... ikitokea emergency akienda hospital yoyote wata save maisha ya mama kwanza
 
Pole sana mkuu.
Tafuta njia nyingine ya kuokoa Maisha ya wote,Huenda Mungu akukuwekea Mkono wake.
Kama ameweza kujifungua kwa Oparesheni zaidi ya 3 Na hii pia ataweza,Kwa kuzingatia Wataalam wa afya ya Uzazi mama na Mtoto.
 
pole sana mtoa mada, fata ushauri wa dakatari, inawezekana pia mtoto akazaliwa salama tu. kuua kiumbe kama wengi walivyoshauri naona kuna ugumu. pengine mungu amesikia kilio chenu cha mtoto wa kiume na ndio huyo amewapatia.
 
Mkuu wengi washakushauri kwamba okoa kwanza uhai wa mama ila pia nina imani kama ukipata hosp iliyotulia hasa nje ya nchi kama uwezo upo unaweza ukaokoa uhai wa wote wawili as long unapendelea sana mtoto wa kiume embu fanya ultra sound muone ni mtoto gani anatarajiwa? Ila kama itashindikana kupata hosp makini ama kwenda nje basi mama kwanza ila pia huyo dkt sio wa kumuacha bure aliyefunga kizazi inabidi atoe maelezo yanayoeleweka imekuwajekuwaje mimba imeingia
 
Mungu ni Mwema
Pole sana Mkuu,fuata ushauri wa Madaktari.
 
Noo nina mama yangu mdogo ana watoto watano wote kwa operation ww cha muhimu tafuta daktari bigwa wa kinamama awe karibu na mkeo atajifungua na wote wawili wataishi pole dn
 
Mkuu, haya mambo ya kubahatisha yatakuja kukuletea majuto makubwa huko mbele, ushauri umeshapewa na wataalam vipi tena unataka ushauri hatarishi pia uwemo? Nakushauri fanya haraka mharibu mimba ili kumuokoa mama, hizi habari sijui mtoto wa kike au wakiume hazina maana tena, mshukuru Mungu kwa watoto wanne uliowapata kwa maana wengine hata wakusingiziwa hatuna.
 
Pole sana. Hospitali/daktari aliyefanya opersheni ya kufunga mirija ya uzazi unaweza kumchukulia hatua za kisheria. Zipo rejea za kesi kama hiyo katika mahakama zetu au hata nchi jirani. Kama unazo doc au fanya namna upate kutoka hospitalini. Wasiliana na wanasheria kama uwashtaki uongozi wa hospitali(sahihi zaidi) au daktari aliyehusika.
. Kuhusu mama,pata ushauri kutoka kwa madaktari bingwa magonjwa ya wanawake.
 
Pole sana mkuu,,onana na madaktari Bingwa Achana nao hapo M/Nyamala.
 
Madaktari wameshakushauri,hebu harakisheni kuokoa afya ya huyo mama.
 
Pole sana.muhimu ni kutafuta ushaur wa kitaalamu hospital nyingine kubwa.na iman utapata tu ufumbuzi. Muombe sana Mungu atakusaidia.mimi wazaz wangu walinipata kwa njia kama iyo.ujauzito wangu uligundukila ukiwa na miezi 7.mama alikuwa anahisi ni uvimbe tu coz alishafunga kizazi.alipata ushaur mzuri hadi ni kazaliwa.tafuta ushaur wa haraka kwa madaktari bingwa then fanya watakavyokushauri.pole mno.ila inauma na kuvuruga akili ukijua hukupagwa kuzaliwa.
 
Umeishia mwananyamala tu??? unajipa conclusion nenda hosp kumbwa km muhimbili ikiwezekana hata nje uokoe maisha yao both.

On my opinion bora ufanye hivyo kuliko kukimbilia kama wengi wanavyokushauri uokoe mama tu. Kila mtoto ana riziki yake hujui Mungu kampangia nini huyo kijacho huo ni mtihani ndugu muombe na mshirikishe Mungu katika hili everything happens for a reason.
 
Back
Top Bottom