Tunaamini katika kujiajiri lakini wakati huohuo tunawadharau wanaojiajiri

Tunaamini katika kujiajiri lakini wakati huohuo tunawadharau wanaojiajiri

Etugrul Bey

JF-Expert Member
Joined
Aug 6, 2020
Posts
6,514
Reaction score
15,247
Kutokana na uhaba wa ajira katika Zama hizi kumepelekea watu kuona umuhimu wa kujiajiri ili walau Maisha yaweze kusonga mbele, kwasababu uhitaji WA ajira ni mkubwa na nafasi zilizopo ni chache mno kuweza kukidhi mahitaji.

Kwahiyo namna pekee ya kutatua changamoto hii ni kutafuta njia mbadala ambayo itaweza kukidhi au kupunguza tatizo la ukosefu wa ajira nchini Kwa kuhamasisha watu waweze kujiajiri na kuendesha Maisha Yao.

Lakini Kwa masikito makubwa kabisa kuna matamshi ambayo huenda yanatolewa na wanasiasa ambao jamii ingetarajia kusikia wao ndio wakiwa WA Kwanza kuwapa vijana moyo WA kujiajiri katika shughuli halali na kujiingizia kipatao, lakini badala yake wao ndio WA Kwanza kuwakatisha vijana tamaa Kwa kuonyesha dharau Kwa kile vijana wanachofanya.

Hapa nazungumzia ajira ya bodaboda, hakuna asiyejua kwamba hii sekta hakika imewapa ajira vijana wengi Sana ambao hapo awali walikuwa vijiweni Bila chanzo chochote cha mapato,na kupelekea wengine kuingia katika shughuli haramu kama ujambazi,udokozi na wizi pamoja uhalifu mbali mbali.

Lakini kuja Kwa bodaboda na baada ya serikali kurasimisha hii biashara rasmi walau vijana wengi sasa Wana shughuli halali za kuwaingizia vipato na walau Maisha yanasonga japo sio Kwa asilimia mia moja.

Sasa kumeibuka kauli za kuwakatisha tamaa hawa vijana Kwa kudharau kazi Yao, na kuwafanya wajione duni Sana kitu ambacho si kizuri kabisa na hakina staha hata kidogo. Wewe kama Una shughuli nzuri zaidi ya kukuingizia kipato basi mshukuru Allah Kwa hiyo neema,lakini usione ajira ya bodaboda ni dhalili na haifai, kuna msemo unasema "kimfaacho mtu ni chake" kwahiyo kama wewe kwako unaona boda boda hailipi basi fahamu Kwa wahusika Maisha yanasonga mbele na wala hawaji kwako kukulilia shida.

Hata humu Jf kuna wapuuzi wachache huwa wanakandia ajira ya bodaboda na kusema sijui ni Laana kitu ambacho si kweli, na nimesikitishwa zaidi kusikia toka Kwa bodaboda mwenyewe akikiri kuwa hii kazi ni laana.

Huenda labda bodaboda WA sehemu Fulani wanatofautiana na WA sehemu nyingine, kuna kijana namfahamu kutoka mkoa wa Pwani alianza na bodaboda ya mkataba na kufanikiwa kumaliza na mpaka sasa anamiliki boda boda tatu (3) Kwa stahili hiyo hiyo,na yeye sasa ni boss kawapa vijana pikipiki mbili na yeye anakomaa na moja.

Ninachotaka kusema hapa, vijana wengi WA boda boda wanaendekeza Sana umalaya, kwasababu waendesha boda boda na wanawake ni damu damu,sasa kijana wa bodaboda akishakuwa na mashangazi wawili au watatu je unatarajia nini sasa, na wadada wanawapenda kwakuwa Kwanza watapanda boda boda bure na pili hawakosi buku mbili tatu Kwa hawa bodaboda, na kwakuwa Bida boda huwa anaombwa buku mbili mbili basi anaona kama hela ndogo Tu,lkn akija kupiga hesabu anajikuta anapoteza hela mingi Sana Bila kujua.

Kwahiyo Kwanza Boda boda wenyewe mbadilike mthamini ajira yenu na pili muache kuendekeza wanawake kwakufanya hivyo walau kipato mtakiona.

Na jamii iheshimu Ajira ya Boda boda kama inavyoheshimu ajira nyingine kwani hizo ni ajira na mwisho wa siku inaleta mkate ndani, kama wewe unaona ajira ya boda boda Kwa upande wako haikufai basi kausha Tu waache wenye kazi zao.

" Pili pili usiyo Ila je inakuwashia nini"


Ni hayo Tu!
 
Back
Top Bottom