Tunaelekea wapi jamani? Mfuko wa saruji(cement) umefikia Sh. 15,500/= Kigamboni

Bei ya cement siyo bei elekezi. Hili ni soko huria kama sufuria maana kwetu ni 18500 mfuko wa cement ni kawaida sana kwani lazima sote tujenge kwa cement, watajenga wenye uwezo wa kununua cement
 
Sijui kama umeelewa nilichosema nilimaanisha mchawi ni Serikali
Kabisa.dangote alitaka kuuza cement mpaka 5,.000 serikali wakamwambia hyo haiwezekani.serikali ndo inawapa jeuri twiga.
Hata mawakala wa cement wa twiga wanadharau sana.sababu wanajua Hakuna mpinzani.
sijui waziri wa viwanda anafanya kazi gani.
yaani ni upumbavu mtupu.
 
Sub sahara mentality ni kila mtu kumiliki nyumba nadhani ndo problem.Nliongea na wazungu nchi mbalimbali waliniambia Kwao kujenga sio kipaombele sababu rent na nyumba za kupanga ni simple.Hata Tanzania sio ghali.Tatizo mindset.
Unaongelea wenzako ambao walianza kujenga nyumba za maana B.C
Saa hizi ni lazima tu wapange watajenga wapi
Hapa Tanzania nyumba zimeanza kujengwa baada ya uhuru zenye kukidhi mahitaji mpaka uvutiwe ni chache na ni expensive kwa nini watu wasijenge!
 
Ndugu umewahi kufanya biashara yoyote japo ya Genge? Unajua biashara ni faida.? unajua majanga wanayofanyiwa wafanyabiashara mikodi isiyoeleweka?
Wanapanga faida,mtu anakwambia hapa tunakomaa kuuza 17,000 hata 18000 watanunua tu.
 
Wanapanga faida,mtu anakwambia hapa tunakomaa kuuza 17,000 hata 18000 watanunua tu.
....hapa mchawi ni serikali sio hao wauza cement maana wanafanya biashara kutokana na taratibu.zilizopo
 
....hapa mchawi ni serikali sio hao wauza cement maana wanafanya biashara kutokana na taratibu.zilizopo
Jana nimekwenda kununua cement Muuzaji anasema sina cement zote ni za order ila kama unaweza kulipia 16500 sawa unapata
Mwenzie akasema hapa kesho mkija nauza kuanzia 17,000 kwenda juu

Hizo ndiyo taratibu za uuzaji?!
Na ujue wameficha mzigo ili demand izidi wapange bei
 
Ndugu umewahi kufanya biashara yoyote japo ya Genge? Unajua biashara ni faida.? unajua majanga wanayofanyiwa wafanyabiashara mikodi isiyoeleweka?
Mkuu dolevaby mbona unanikosea heshima??Yaani jembe shambani??Kukujibu swali lako hivi unajua majukumu ya taasisi kama Ewura?? Production cost huwa zinakuwa considered wakati wanapokuwa wana regulate bei,muhimu kungekuwa na bei elekezi kama ilivyo fuel, bei ambayo inakuwa imefanyiwa tathmini yakina kwa kuangalia factors zote.
 
Niwie Radhi chief huenda sikueleweka nilimaanisha Taabu yote inaletwa na wafanya maamuzi wa kwa niaba ya wananchi Namaanisha Serikali hao wafanyabiashara wanafanya huo ujinga wakuumiza watu sababu hakuna wakuwaambia kitu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…