SoC04 Tunaelekea wapi?

Tanzania Tuitakayo competition threads

BASSAM MAKACHA

New Member
Joined
Jan 9, 2024
Posts
1
Reaction score
0
TANZANIA TUITAKAYO.
Mazuri yajayo yataboresha maisha yetu na kutufanya tujivunie Kwa ukuaji wa uchumi na mabadiriko ya miundombinu .Tujiandae Kwa haya yafuatayo.

SEKTA YA AFYA.
Jitihada zake zinavutia sana naanza na pongezi.

Ugonjwa wa kifua kikuu"TB' huu ni ugonjwa hatari sana,unashambulia mapafu Kwa kasi kubwa sana.kikawaida vidonge vyake huwa ni vikubwa sana Kwa mtumiaji ,matumizi yake ni SIKU 180 sawa na vidonge 720 amabapo kidonge kimoja kina zaidi gram 11 na unatakiwa kumeza vinne Kwa SIKU mara moja tunachohitaji kuwe na chanjo maalumu kuepusha hili tatizo Kwa WATOTO wajao lakini pia Kwa kutambua ukubwa wa mabadiriko ya kutambua mabadiliko ya kisayansi tunahitaji dozi iliyoboreshwa ambayo matumizi yawe Kwa muda mfupi mgonjwa apone

Hii itachangia wagonjwa kutokatisha dozi kiukweli kiharisia dozi zilizopo sasa zinaumiza misuli ,zinachosha Kwa wingi wa siku na unywaji pia sharti ni gumu zaidi unahitajika unywe na kula Kwa kushiba sasa ndani ya miezi sita na Kwa hali ya maisha yakawaida ni vigumu kujimudu Kwa muda wote

Ongezeko la waganga wa dawa za asili.
Kumekuwa na ongezeko la watabibu wa dawa za asili lakini mashaka yetu makubwa hakuna chuo maalumu kinachotoa hawa watalamu na mbadala wake tunaona vyeti vilivyosajiliwa na baadhi yao wenye maduka wanalipa Kodi swali la msingi mafunzo wanapata wapi? Sote hatufahamu kiukweli kama tunawahitaji hawa watabibu wa dawa za asili lazima kijenge chuo mahsusi au wathibitishwe na watalamu waliothibitishwa na serikali. Hii huchangia kupungua Kwa matapeli pia Tiba za jadi hususani za Tanzania kutambulika kimataifa na nchi zote zilizoendelea kutumia Tiba zetu.

Wakata Vimeo au "vidaka"
Ni aibu Kwa nchi inayoendelea kutokuwa na watalamu na wabobozi katika hospitali za serikali na mbadala wake wakata Vimeo wa njia za jadi ambayo hawatambuliki kiserikali hawana vibali madhara yake watu wanakufa kiholela .kama tukishindwa kuwa na dawa maalumu ya kuyayusha hiko kimeo basi inatulazimu tuwe na madaktari bingwa wa ukataji.

MIUNDOMBINU.
Hapa ndo kwenye muonekano wa nchi na kutambua mandhari ya kuvutia .

Aina za mtindo wa ujenzi.
Kwa kutambua ubora wa viwanja vilivyopimwa na serikali pia tuwe na mipango mahsusi ya ujenzi wa kisasa Kwa kila eneo lililopimwa na serikali siyo tu kujenga hovyo .kila mnunuzi apewe ramani maalumu ramani mchanganyiko wenye mandhari mchanganyo ili achague MTINDO anao hitaji Hii itasaidia kuonyesha mazingira mazuri ya mji wa kisasa.

Maghorofa
Ghorofa nyingi za mijini ni za zamani sana zinahitaji marekebisho ya njia za maji na gesi za kuzima taharuki na hatari inapotokea lakini sehemu za mijini watu ni wengi hufanya shughuli tofauti tofauti hawa watu pindi inapotokea hatari huwa wa mwanzo kutoa msaada wa kwanza jamii inahitaji mafunzo mara Kwa mara njia za kutumia pindi tatizo linapotokea nini chakufanta .

Kwanini kivukoni kwenda kigamboni hakuna daraja mpaka sasa Kwa mtazamo kivuko huzalisha fedha nyingi na watu wengi hupita kwenda kufanya shughuli mchanganyo ni jambo la msingi kuwe na daraja la funga na fungua lenye mvuto wa kisasa italeta mtazamo mazuri sana

TEKNOLOJIA
Hapa ndo ilipo Dunia Kwa sasa. Shule zetu za misingi za serikali hakuna somo la vitendo la somo la teknolojia mpaka sasa ni aibu Kwa kupata vijana washindani na wabunifu wa kimataifa kiukweli inatupaswa kuwandaa watalamu wabobezi wa tehama kuanzia ngazi ya chini. Shule zetu za misingi za serikali ziwe na kompyuta anagalau somo hili Liwe kipaumbele lakini pia kuwe na televisheni itayo onyesha vipindi maalumu vya ukuaji wa teknolojia itasaidia kukuza ubongo na kufanya kuwa wepesi zaidi Kwa vijana wetu wajao.

Serikali iwe na email maalumu ambayo itatufanya sisi wananchi kutoa maoni,maovu na ushauri lengo kujenga nchi Kwa pamoja maana Mtindo wa barua ni WA muda Sana na huchochea rushwa na ni mgumu kuwafikia walengwa.

Ongezeko la wanahabari.
Ni muhimu kuundwa Kwa Sheria Kali Kwa wanahabari wasiokidhi vigezo vya watoahabari .lakini pia wanaotoa habari za upotoshaji na uchochezi washurutishwe kiukali zaidi.

SEKTA YA ELIMU.
Utandawazi na ukuaji wa kiswahili .bila shaka ni lugha inayokuwa Kwa kasi sana duniani,lugha pendwa zaidi ya Kiswahili lisiwe somo tu mashuleni na mazungumzo midomoni mwetu .kama tunahitaji lugha iwe kubwa zaidi kuwe na michakato ya midaharo ya mara Kwa mara Kwa ngazi ya awali mpaka juu yani kitaifa na kimataifa na zawadi kubwa ziwe za mvuto kwenye mashindano ya midaharo yatasaidia kukuza lugha pia kuketa morali Kwa wandishi na wazungumzaji kuongezeka Kwa lugha yetu pendwa ya kiswahili.
 
Upvote 2
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…