Tunaenda AFCON TFF Tafuteni kocha mwenye CV

Tunaenda AFCON TFF Tafuteni kocha mwenye CV

Tumeisha wajaribu sana hao wenye CV na bado mambo yalikuwa haya haya
Tumeifunga zambia kwao wakiwa na kocha mzoefu mno wa mpira Avram Grant
Nadhani huu wakati twende na kiemba na Julio wakiwa chini ya Moroko
Timu linacheza hovyo,kutwa kulinda,game za kirafiki na timu kubwa kupaki bus,cosafa na madagascar kupaki bus mpaka tufungwe ndiyo zianze pilika,hivi stars ya maximo ilikua ikicheza hivi!?
 
Hili lizanzibar lipuuzi tu.... Karia yupo kujikosha kwa bibi chura kiziwi takataka kabisa.
 
Tanzania hatujawahi kushinda mchezo wowote katika kushiriki kwetu afcon. Kwa ufupi nimiongoni mwa timu dhaifu sana katika mashindano ya AFCON zilizopita.

Pamoja na unyonge huo tunatakiwa kujitutumua kwenye maandalizi , TFF tafuteni mwalimu mwenye uwezo mkubwa na hili halihitaji kupepesa macho. Nchi inayoshika nafasi zaidi ya 110 haiwezi kutoa kocha mwenye mafanikio , nchi zinazotumia makocha wa nchi zao ninchi zenye mafanikio kimpira.

Kuhusu ligi namba 5 africa , hilo lisituponze kabisa , ukitaka kujua ubora wa ligi yetu ondoa Simba, Yanga, na singida big staa na timu zenye wachezaji wa kigeni kinachobaki ndio ligi yetu
NO REFORMS NO ELECTION
 
Tumeisha wajaribu sana hao wenye CV na bado mambo yalikuwa haya haya
Tumeifunga zambia kwao wakiwa na kocha mzoefu mno wa mpira Avram Grant
Nadhani huu wakati twende na kiemba na Julio wakiwa chini ya Moroko
Sipo kumuaribia mtu kibarua chake, lakini kwa Moroco mtanisamehe, hamna kocha mule.
Naungana na mdau, atafutwe kocha mwengine, sio huyo Moroco.
 
Kocha Morocco amefanikiwa kutengeneza timu inayojua kuzuia wanapoamua kulinda, hawafungwi kirahisi, anachotakiwa kufanya ni kujifunza kusoma mchezo kama Gamondi wa Yanga , kufanya subs za haraka bila kuangalia jina la mchezaji pia aweze kuwaaminisha wachezaji kuwa wana uwezo wa kushinda mechi yoyote , rejea mechi ya Zambia Afcon tuliongoza ila jamaa wakarudisha, ilikuwa ni makosa ya kocha kuacha kufanya subs za kuleta nguvu mpya uwanjani , hasa kuingiza viungo wakabaji, wachezaji wamechoka sote tunaona wamezidiwa yeye akaacha hao hao uwanjani, pia mechi na DR Congo tulizuia na jamaa wakachoka kushambulia tukawa na uwezo wa kufunga badala yake kwa uoga wa jina la DRC wachezaji wakawa wanapoteza muda kupasiana kwenye box yao hadi mpira ukaisha wakati ilitakiwa wapambane na hata kama wangefungwa potelea mbali, ilinichukiza sana nikasema hawa wachezaji hopeless kabisa badala ya kutafuta goli msonge mbele eti mnapoteza muda msifungwe wakati droo ilikuwa inawarudisha nyumbani, rubbish.

Morocco ni kocha mzuri sana anahitaji msaidizi wa kumsaidia kusoma mchezo haraka kama kocha Moalin msomali wa Yanga. Aende nae Afcon kupambana na asipaki basi acheze mpira liwalo na liwe, kufungwa tushazoea asiogope kufunguka inapobidi hasa mechi ya mwisho kufa kupona, bongo mpira umekua wakacheze wasiogope timu yoyote, uwezo wanao, mi nilitabiri wataenda Afcon nikaweka uzi humu jf na kweli wameenda sababu uwezo wanao
 
naunga mkono hoja huyo morroco,mgunda na julio hawana uwezo wa kufundisha taifa stars
Kwenye inshu ya tactical na technical organisation kwenye Mpira , ubunifu wa kocha hakuna kiti pale halafu huyu pia ana kaunzanzibar Fulani kwenye kuita na kupanga kikosi. Naunga mkono hoja 100%
 
Back
Top Bottom