Tunafanyaje kuhusu suala la Ushuru TRA?

Muda si mrefu nimetoka kuongea na TRA kupitia namba zao zile za huduma kwa mteja.

Muhusika ananiambia kuwa wao wameshaevaluate hiyo bei kwa flat rate wanayoitambua. Ikiwa ndogo zaidi ya ile waliyoipanga then wanachukua iliyopangwa ikiwa ni kubwa zaidi waliyoipanga wanachukua hiyo bei mpya uliyokuja nayo.

Upumbavu wa karne.

Ananiambia consideration ipo katika consumer goods nyingine but sio magari na mashine nyinginezo. Aisee nikakasirika sana. Nikamuuliza so hapa nani tunamuwajibisha akasema wabunge wenu wanaotunga Sheria. Wao ndio wanaomletea commissioner na serikali sheria wao ndio watunga sheria.

Commissioner na serikali wao wanadeal na maelekezo ya hizo sheria.

Jamani tuwe serious na watu wanaokwenda bungeni jamani.

Mabadiliko yanatakiwa kuanzia bungeni pale.
 
Magari ya serikali mengi ni chakavu pia alafu kama serikali zetu zingekuwa sikivu wangepunguza ushuru angalau Kwa 30% pengine nusu ya watanzania wangemiliki gari
 
Niliwahi uliza hili swala mahala. Inakuaje gari inachajiwa kodi zaidi ya bei ya kuinunulia wakati Tra hawajui kuitengeneza hata nut ya kwenye hiyo gari? Nikajibiwa lengo hasa ni ku control traffic jam, miundombinu yetu bado haiwezi kuruhusu kila raia kumiliki gari hivyo kodi kua juu kuna control idadi ya magari kuendana na miundombinu yetu.
 
Wao wame evaluate hio bei kwa vigezo gani? Bunge limewapa sheria ya ku evaluate kwa vigezo vipi? Huyo na wenzie ni clueless kwenye sector ya magari na bei zake.
 
Hoja dhaifu sana kwasababu watu wanakimbilia magari ya bei nafuu, traffic iko pale pale.
 
Sikubaliani na wewe mjumbe. Hebu nenda kwenye calculator ya TRA angalia kodi ya magari ya kuanzia miaka ya 2011 na kuendelea..kodi zake si za kitoto...Hawa TRA hawako kwa lengo la kumsaidia mnyonge.

Lakini bora gari chakavu la Japani kuliko haya machakavu tunayouziana wenyewe Kwa wenyewe..

Unanunua gari namba A, unajikuta wewe ni mmiliki wa 9, limegongwa gongwa na kupata ajali mara kadhaa..
Limenyooshwa limejaa puti kilo 35..[emoji15][emoji15][emoji15][emoji15][emoji15][emoji15][emoji15][emoji15][emoji15][emoji15][emoji15]
 
Nadhani nilishaiona hiyo comment yako.....
 
Wao wame evaluate hio bei kwa vigezo gani? Bunge limewapa sheria ya ku evaluate kwa vigezo vipi? Huyo na wenzie ni clueless kwenye sector ya magari na bei zake.
Nimemhoji yule dada wa huduma kwa mteja ameshindwa kunipa majibu ya kueleweka cha zaidi alikuwa anatoa majibu kama nesi wa muhimbili.
 
Eti puti kilo 35...[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Ndio maana magari haya yanakuwa yanakula sana mafuta sababu yana uzito wa puti [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Nani kakudanganya?
 
Roho inaniumaga sana kwenye Subaru Legacy BM9 au Forester SH9....lazima uache milioni 24,000,000 wakati gari umelinunha $4000
 
Wabunge hawatungi sheria. Serikali ndio wanaotunga sheria na kuzipeleka bungeni, wabunge kazi yao ni kuzipitisha kwa kura za ndioooo
 
SI kweli
 
Roho inaniumaga sana kwenye Subaru Legacy BM9 au Forester SH9....lazima uache milioni 24,000,000 wakati gari umelinunha $4000
Na Volkswagen jamaa wanapiga kodi ya kukomoa...
 
Wabunge hawatungi sheria
Serikali ndio wanaotunga sheria na kuzipeleka bungeni, wabunge kazi yao ni kuzipitisha kwa kura za ndioooo
Hapana serikali hawapeleki sheria bungeni, huwa wanapeleka mswaada ili ujadiliwe na ukishapitishwa ndipo unageuzwa kuwa sheria baada ya raisi kusign
 
Daaaaah umeongea kwa uchungu sana na ukweli mkuu,

Pole kwa iyo kadhia....Naunga hoja.
 
Mnapeleka std seven, tunategemea nini hapo kila jambo ndiyooooo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…