Tunahitaji a Surrogate Mother

Tunahitaji a Surrogate Mother

Eliphaz the Temanite

JF-Expert Member
Joined
Jan 19, 2010
Posts
3,018
Reaction score
1,151
Rafiki yangu aliyefunga ndoa mwaka 2006 amekuwa akijitahidi kupata mtoto bila mafanikio, Mke wake hubeba mimba kama kawaida na punde siku zinapokaribia kujifungua kiumbe hupoteza uhai! Amekwisha jaribu zaidi ya mara 3 bila mafanikio!

Uchunguzi wa hivi karibuni unaonyesha kuwa mke ana tatizo la kuwa na mfuko mdogo wa uzazi ambao hauwezi kusurport full growth ya mtoto.

Katika majadiriano likaja la kutafuta a surrogate mother! Si jambo baya na limekuwa linafanyika nchi za wenzetu, je kwetu kisheria linakubarika? Na kama linakubalika nani yuko tayari kuingia mkataba huu?

Lengo hasa la wanandoa hawa ni kupata mtoto anyetoka katika mauno yao! Nakaribisha ushauri, mawazo, na kama kuna binti ambaye yuko tayari kusurrogate kwa malipo na matunzo mpaka atakopo jifungua anakaribishwa
 
Hapo ndipo utaona sharia ya kuoa wake zaidi ya mmoja inavyonufaisha.
 
Hapo ndipo utaona sharia ya kuoa wake zaidi ya mmoja inavyonufaisha.

akili zengine bwana.
Kwa hiyo kungekuwa na wake wawili ndio huyu mke mwenye matatizo angepata mtoto wa maungo yake? Uwache pumba wakati mwingine, unajua fika madhila wanayopata wake wenza, hasa ikitokea amekuwa tasa kwa bahati mbaya!
 
Adha ni kwa wale wasiomuamini Mwenyeezi Mungu na sharia zake, mwanamke mwenye imani yake humuambia "mume wangu kaoe" uniletee watoto nilee. Tumewaona wengi tu wa namna hiyo.
 
Naomba kukuuliza; Hili ni tatizo pekee! Je hakuna uwezekano wa kumtoa mtoto kabla ya kufikia full term (C-se) ku- avoid hili kutokea?
 
Kwani lazima wafanyie Tanzania? Nadhani huku hakuna legal provision ya hypothesis hiyo.
 
Hhhmm sijui kama kwa bongo kuna mtu yuko tayari. Ila mnaweza mkapata. . . kama kuna pesa ndefu.
 
kwa bongo bado sana maana atakae patikana atakaba atafikiri yeye ndo mke halali
 
akili zengine bwana.
Kwa hiyo kungekuwa na wake wawili ndio huyu mke mwenye matatizo angepata mtoto wa maungo yake? Uwache pumba wakati mwingine, unajua fika madhila wanayopata wake wenza, hasa ikitokea amekuwa tasa kwa bahati mbaya!

Jamani FaizaFox kwa maelezo yake kasema amesoma madrasa tu! Siku hizi nimemuelewa sipati shida kuelewa majibu yake. Madhara ya Brain Wash.
 
nainua mkono hapa kitambaa cheupeeee
alama ya upendo hapa na si kusonkolana

back to topik!
Kwa kiswahili swahili, ngumu sana mtu kukuelewa.
 
mama wa kibongo ukimgongea deal la kuwa surrogate mother, basi ujue mkeo inabidi atafute kabisa sehemu ya kuhamia
 
Hapo ndipo utaona sharia ya kuoa wake zaidi ya mmoja inavyonufaisha.

wacha bwanaaa... Na je ka mwaaume ndo mwenye matatizo?
Tuache tabia za kushabikia udini kila pasipo na hoja za msingi
 
Back
Top Bottom