mrdocumentor
Member
- Nov 27, 2021
- 45
- 56
Tanzania ni miongoni mwa nchi chache ambazo zimebarikiwa vijana wapambanaji sana.
Hii ndio nguvu kazi ya taifa na ndio chanzo halisi cha pato la taifa kutokana na jasho lao linalovuja kila uchwao.
Wapo vijana wakulima, wavuvi, wafanyabiashara, wapiga debe na wengine wengi.
Picha kutoka mtandaoni
Siku ya leo naomba tulitazame kundi moja tu. Kundi Hilo ni wafanyabiashara. Na si wafanyabiashara tu bali ni wafanyabiashara wadogo.
“Ndio ni wafanyabiashara wadogo”
“Hivi ni nani huyu mfanyabiashara mdogo?“
Mfanyabiashara mdogo ni mtu anaejishughulisha na kuuza na kununua bidhaa Kwa Lengo la kupata faida akiwa na mtaji mdogo.
Zipo tofauti za wataalamu na wasomi wengi juu ya kiwango sahihi ambacho kinaweza kutumika kama kipimo sahihi Cha kubaini kuwa yupi mfanyabiashara mdogo na yupi mfanyabiashara mkubwa
Lakini hilo mimi na wewe halituhusu tuwaachie wanazuoni Wenyewe waendelee kubishana wakifika muafaka watuletee jibu sahihi na sisi tutalipokea likiwa kama malighafi iliyochakatwa na Kuwa bidhaa safi tayari Kwa mtumiaji wa mwisho.
Hivi Tanzania ina hawa watu?
“Jibu ni ndio”
Kwa utafiti uliofanywa mwaka 2012 juu ya wafanyabiashara wadogo na wa kati wanaopatikana nchini ulibaini uwepo wa wamiliki wa biashara hizo milioni 2.75 na uwepo wa biashara milion 3.16 zikichangia 27% ya Pato la taifa na kuajiri Zaidi ya watu milion 5.2.
Lakini pia kutokana na ripoti ya Tanzania chamber of commerce, industry and agriculture walibaini kuwa 95% ya biashara za Tanzania ni ndogo ndogo wakati huo zikichangia 35% ya pato la taifa.
Richa ya takwimu hizo ambazo zinaonesha wazi kuwa kwa Tanzania kundi hili ni kubwa mno lakini bado watanzania wenyewe hatujalitendea haki kundi hili.
Yapo matatizo mengi Sana wanayopitia hawa watu mfano kukosa maeneo ya uhakika ya kufanyia biashara, kunyanyaswa na mengine mengi.
Lakini siku ya leo nitazungumzia tatizo moja tu.
“Ni lipi hilo tatizo?”
Kutokopesheka
Kwanza tujiulize kidogo
“Hivi ni kweli hawa watu hawakopesheki au hatujawashawishi kukopa?”
Inawezekana mtu akawa na shida kweli na akawa tayari kukopa ila kutokana na mazingira yaliyopo hayajamshawishi kufanya hivyo anaweza kuamua Kuendelea kuvumilia shida zake na asikope.
Vivyo hivyo kwa mfanyabiashara mdogo hawezi kukopa mtaji ikiwa mazingira si rafiki kwake.
Lakini mi nimegusia tu na hata sijatoa jibu la swali letu la msingi .
Kupata jibu la swali hilo tuangalie baadhi ya sababu zinazotajwa kuwa zinawafanya wafanyabiashara wadogo wakose mkopo.
Mara baada ya kuangalia sababu hizo kila mtu atapata jibu lake juu ya swali letu la msingi la kutaka kujua kuwa hawa wafanyabiashara wadogo hawakopesheki au hatujawashawishi kukopa?
Zifuatazo ni baadhi ya hizo sababu:-
Kukosa dhamana
Taasisi nyingi za fedha hapa nchini zimekuwa zikisisitiza zaidi kwenye suala zima la dhamana. Yaani Ili upate mkopo benki lazima uwe na kitu yaani mali ya kudumu na isiyohamishika.
picha kutoka mtandaoni
Kwa mujibu wa tafiti iliyofanywa na SIDO (Small Industry development organization) 2008 walibaini kuwa 92% ya vijana wanaomaliza shule wanaingia moja kwa moja kwenye kundi la wafanyabiashara wadogo. Kwa hali ya kawaida vijana wanaomaliza shule na kuingia mtaani hawawezi kuwa na hizo dhamana za kudumu kwa sababu wametumia muda wao mwingi shule na si katika Kutafuta mali na wanaingia mtaani Ili kuanza kuzitafuta hizo mali alafu wanakutana na iko kikwazo. Kwa hali hii kundi hili linakosa sifa ya kukopesheka.
Kutokuwa na tabia ya kutunza pesa katika njia sahihi yaani benki.
Wafanyabiashara hawa wadogo wanatoka kwenye jamii zetu ambazo zimekuwa zikiamini kuwa wanaopaswa kuwa na akaunti za benki ni wenye pesa nyingi pekee. Hivyo basi mawazo hayo wanapotoka nayo kwenye jamii wanapeleka pia kwenye taratibu za uendeshaji wa biashara zao na kutunza rekodi za biashara hizo kienyeji.
Kabla hatujawalaumu wafanyabiashara wadogo tuangalie hali ya umiliki wa akaunti za benki nchini kwa ujumla wake.
Hali ya watu kumiliki akaunti za benki nchini ni mbaya Sana. Takwimu za umiliki wa akaunti za benki nchini zilizotolewa na ofisi ya taifa ya takwimu (NBS) Katika ripoti yake ya utafiti wa mapato na matumizi ya kaya binafsi 2017/2018 ilibaini 12.3% tu ya kaya Tanzania bara ndizo zilizokuwa na walau mtu mmoja mwenye akaunti binafsi.
Picha kutoka mtandaoni
Vile vile ripoti imeonesha wananchi wengi wenye akaunti za benki wapo maeneo ya mjini Kwa 23% tofauti na vijijini ambapo 6.1% tu ndio Wana akaunti za benki.
Hapo nimejaribu kutoa picha ya hali Ilivyo kwa nchi nzima ili wote kwa pamoja tuone hali ya jamii yetu ilivyo nyuma kwenye suala hilo.
Kwa hali hii hamna taasisi yeyote ya fedha itakayokubali kutoa mtaji bila kuona Uhai wa biashara hiyo na Uhai wa biashara ni kuwa na rekodi za miamala ya mapato na matumizi ya biashara yako. Hii pia inatajwa kuwa ni sababu ya wao kutokopesheka.
Mchakato mrefu wa utoaji wa mkopo.
Hapa nitaangazia kwa pande mbili. Upande wa kwanza ni ule upande wa mkopo wa halmashauri na upande wa pili ni ule wa taasisi nyingine za fedha
Fungu la halmashauri
Fungu hili lipo lakini halionekani. Kama ambavyo viongozi wanasisitiza kuwa “Vijana mna fungu lenu halmashauri “
“Unafikiri kwanini halionekani?”
Sio kweli halionekani Ila vijana wanajua kuwa hadi ufaidike nalo unapoteza muda mwingi na unachokipata hakina thamani ya ule muda uliopoteza ndio maana vijana hawa wanaona hili fungu kama halipo . Tatizo hapa ni mchakato tu. Lakini fungu hili kweli lipo na mgawanyo wa hizo asilimia 10 ni kuwa 4% ni ya vikundi vya wanawake 4% ni ya vijana na 2% ni ya walemavu.
Mgawanyo wa asilimia hizo huwenda usiwe na tatizo sana ila shida inaanzia kwenye sifa za hicho kikundi hadi kiweze kufaidika ni sifa ambazo hadi kutimia ni mchakato mrefu mno ndo mana vijana wengi wanakata tamaa.
Picha kutoka policy forum journal
Taasisi za fedha
Taasisi hizi zimekuwa zikiwakatisha tamaa vijana wengi Kwa kuwa na mchakato mrefu Sana na vigezo vigumu ambavyo kwa mwananchi wa kawaida si rahisi kuvitimiza na hivyo kupelekea kukosa mtaji.
“Nawauliza tena!”
“Hawakopesheki au hatujawashawishi kukopa?”
Jitihada
Serikali ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania imefanya kazi kubwa sana katika kuhakikisha wafanyabiashara wadogo nchini wananufaika kwa kiasi kikubwa mno na kile wanachokitolea jasho kwa kuwawekea mazingira Salama ya wao kufanya kazi zao za kila siku.
Lakini pia serikali imejitahidi kuwaundia vyombo mbalimbali ambavyo vitawasaidia wao kuwasilisha mawazo yao kwa viongozi wao ambao watakuwa kama wawakilishi wao. Mfano Shirikisho la umoja wa Machinga (SHIUMA) pia SIDO (Small industries development organization) vyombo hivi vyote vipo kwa niaba ya wafanyabishara wadogo ili kusimamia masilahi yao.
Picha kutoka tovuti ya SIDO
Taasisi za fedha pia zimekuwa zikiwasogelea kwa Karibu mno wafanyabishara hawa ili kuhakikisha wanafahamu fursa ya wao kupata mtaji kutoka benki kwa mkopo.
Mfano hivi karibuni benki ya CRDB iliingia makubaliano na na benki ya maendeleo ya Afrika wenye thamani ya dola za kimarekani milioni 110 kwa ajili ya kuwezesha wajasiriamali nchini hususani wanawake.
Hizo ni baadhi tu ya jitihada ambazo serikali kwa kushirikiana na taasisi za fedha zimefanya na wanaendelea kuzifanya.
Nini kiboreshwe?
Elimu itolewe kwa Wafanyabiashara wadogo.
“Elimu hii itahusu nini?”
Elimu ninayozungumzia hapa si elimu ya kuwarudisha darasani ili warudi kukaririshwa mizigo tena , “Hapana”
Elimu inayotakiwa itolewe kwa vijana hawa ni kuwaelekeza ni kwa namna gani wanaweza kuwa na sifa za kukopesheka kwa sababu ni kweli pesa zipo na taasisi za fedha zipo tayari kuwakopesha ikiwa tu watakidhi vigezo . Sasa tatizo hapa ni Je, Nifanye nini ili niweze kufikia vigezo hivyo?
Hapa ndipo ambapo elimu inahitajika kutolewa kwa namna yeyote ile iwe kwa njia ya Semina, makongamano, warsha na njia nyingine Nyingi Lakini lengo kuu elimu ifike. Na ikiwa elimu itafika kwenye kundi hili kubwa basi sekta hii itasonga mbele na wahusika watafanya biashara kisasa zaidi.
Picha kutoka Ukurasa wa NBC
Tuandae Mazingira rafiki yatakayowashawishi wafanyabiashara wadogo wasihisi kupata mtaji ni bahati nasibu.
Kwa mazingira ambayo yapo kwa sasa kiufupi yanachukua mlolongo mrefu mno hapa nazungumzia pande zote yaani mkopo wa serikali na ule wa taasisi za fedha. Hivyo basi wafanyabishara na watoa mitaji wakae meza moja wajadili namna bora zaidi na ya haraka ambayo itawezesha pande zote mbili kunufaika na huduma ya kila mmoja (win-win situation) .
Tamati
Ikiwa sekta hii nyeti ina uwezo wa kuchangia hadi 30% ya pato la taifa na kuchangia ajira kwa kundi kubwa la vijana basi ni wazi kuwa hii sekta inapaswa kuchungwa sana na kuwekewa misingi mizuri na hatimae nchi yetu itapanda kiuchumi kupitia sekta hii.
Tuige mfano mzuri wa Malaysia.
Malaysia haikuwa juu sana kwenye hii sekta hapo mwanzo lakini kwa takwimu za muda mrefu kidogo 2016 zilionesha wafanyabiashara wadogo nchini humo walichangia 65% ya pato la taifa. Lakini pia sekta hii ilikadiriwa kuwa na uwezo wa kupanda mchango wake kwa pato la taifa kwa takribani 6% kwa mwaka. Piga hesabu toka hiyo 2016 imepita miaka mingapi na je, unafikiri hadi leo wapo wapi?
Picha kutoka mtandaoni
“Inawezekana”
Sio miujiza kikubwa ni uthubutu na utekelezaji wa yale maono yaliyopo kwenye makaratasi na midomoni mwa Watu.
Kuweka mipango ya muda mrefu au mfupi sio dhambi ila ni dhambi ikiwa mipango hiyo haitatekelezwa.
Ahsanteni.

Upvote
9