Reluctance and incapability of small holder farmers to adaptation of new agricultural practices has nothing to do with extension officersThat’s is why we need professional help from agriculture higher education students to stay with farmers for three months in each year of their training. Giving support and advice on the right crops for the season and climate.
Asante kwa hoja nzuri.. shida sasa.. serikali inayotakiwa kubeba jukumu la kuleta mageuzi ndo haina dira wala mwelekeo.. wako bize na miswada uchwara kwa lengo moja, kuendelea kubaki madarakani kwa gharama yoyote ile. Mageuzi yanayohitajika ili kukipa kilimo hadhi yake ni yale yatakayotokana na utafiti, tena wa kina.. serikali iko bize na sera uchwara zinazovuruga moja kwa moja mwenendo wa masoko na mwishowe mkulima anazidi kuwa maskini hohe hahe.. Hakika sijaona watu wa ajabu kama wanasiasa wa Tanzania. Hata wale wasomi uchumia tumbo unawapa tabu sana, hawana mbinu wala namna ya kushauri ili nchi iondokane na jembe la mkono na kutegemea mvua.Ida si kubwa ya wa-Tanzania wanaishi kijijini, Hii ni takribani 70% ya wa-Tanzania. Hawa wanategemea kilimo ili kuendesha maisha yao. Bado jembe la mkono ndiyo nyenzo kubwa ya kutendeackazi.
Kama vijana wanakopeshwa bodaboda , haiwezekani wakopeshwe matrecta ya gharama nafuu?
View attachment 996957
Hili tractor ni moja ya matractor ya gharama nafuu ambalo kinaweza kufanya kazi mbalimbali kwa kubadilisha jembe kulimia au kuvunia.
Kwakweli jembe la mkono linakatisha tamaa katika mapinduzi ya kilimo. Unamwanbia kijana wa miaka 18 baada ya kumaliza darasa la 12 akashike jembe.
Asante kwa hoja nzuri.. shida sasa.. serikali inayotakiwa kubeba jukumu la kuleta mageuzi ndo haina dira wala mwelekeo.. wako bize na miswada uchwara kwa lengo moja, kuendelea kubaki madarakani kwa gharama yoyote ile. Mageuzi yanayohitajika ili kukipa kilimo hadhi yake ni yale yatakayotokana na utafiti, tena wa kina.. serikali iko bize na sera uchwara zinazovuruga moja kwa moja mwenendo wa masoko na mwishowe mkulima anazidi kuwa maskini hohe hahe.. Hakika sijaona watu wa ajabu kama wanasiasa wa Tanzania. Hata wale wasomi uchumia tumbo unawapa tabu sana, hawana mbinu wala namna ya kushauri ili nchi iondokane na jembe la mkono na kutegemea mvua.
Hebu fikiria ikiwa asilimia 50 tu ya watanzania millioni 55 ni watu wenye uwezo wa kufanyakazi maana yake unaongelea watu millioni 25. Katika hao, 70% ni wakulima, maana yake wakulima ni millioni 17.5. Cha kustaajabisha zaidi, wakulima millioni 17.5 wanashindwa kuzalisha chakula kwa ajili ya watu millioni 55, au kwa wastani mkulima mmoja anashindwa kuzalishachakula cha kuwatosha watu wanne.. Hapa kuna tatizo kubwa, ndio maana hoja ya mageuzi (reforms) ni muafaka kabisa. Wanasiasa hawawezi kufanya hesabu ndogotu kama hizo na kuona tatizo ili lifanyiwe utafiti wa kina
Safari bado ipo.. ufukara wa wakulima ndo furaha ya fisiyemu
We haveReluctance and incapability of small holder farmers to adaptation of new agricultural practices has nothing to do with extension officers
Sent using Jamii Forums mobile app
Upo sahihi, Jembe la mkono haliwezi kumkomboa mkulima. Hapo ndipo kulikuwa na udhaifu kwenye sera za Mwalimu Nyerere, kuna mengi mazuri alifanya kama kutufanya tuwe wamoja, kufuta ukabila, udini, kusaidia ukombozi wa Afrika nk.
Lakini kuwapeleka watu vijijini, kuwapa jembe kutegemea kwamba watajitegemea kwa ajiri ya jembe na mvua zisizotabirika, hapo alikosea.
Trekta, irrigation, protection of crops, masoko, barabara zinazopitika hata msimu wa mvua,viwanda vidogo vya kuprocess na kuyatunza mazao hapo bado tuna tatizo.
Vijana jifunzeni kufikiri kidogo, najua elimu yetu haichochei kufikiri, na inakandamiza fikra huru, lakini Nyerere hakufuta udini wala ukabila nchi hii. Pwani ya Afrika mashariki ilishakuwa civilised miaka mingi sana kabla nyerere hajazaliwa, na hapakuwa na ubaguzi wa kidini wala kikabila. Sitaki kuandika sana kwasababu hakuna muda.
Jiulize, kabla nyerere kabla hajaja darisalama, huku darisalama kulikuwa na udini au ukabila? Unawezaje kufuta kitu ambacho hakipo?
Nyerere kazaliwa musoma, kasoma Tabora kwa wanyamwezi. Jee amewahi kubaguliwa na wanyamwezi kwasababu yeye siyo mnyamwezi mwenzao?
Alipokuja pwani kapokelewa na wazalamu. Jee waliwahi kumbagua kwasababu yeye siyo mzalamu?
Kapokelewa na waislamu, jee waliwahi kumbagua kwasababu yeye siyo muislamu? Au alifuta udini na ukabila kabla hajaenda kusoma Tabora na kabla hajahamia pwani?
The moral of the story is.... Learn to think.