Tumeshapiga kelele sana kuwa Nyakati zimefika sasa Tanzania ibadilike, tunaitaji kuwa na shirika la KIJASUSI lugha ngumu, au kwa lugha laini shirka la usalama wa Taifa. Kwa ukweli tulipofika tunahitaji shirika jipya la kisasa lenye watu wenye uwezo wa kuendana na kasi mpya ya dunia hii inayokimbia kwa kasi kubwa.
Ni wakati Mwafaka Watanzania wakamiliki shirka ambalo Watanzania watakuwa na taarifa kamili la kujua kazi za shirika lao ni zipi,lakini wasiojua linatekeleza kwa nani na muda gani.[kwa kuwa kazi za kijasusi ni kaziz za siri]. Ni vema sasa Watanzania wakawa na shirika ambalo watajua kuwa uarifu mkubwa,uhujumu wa uchumi, rushwa, uhaini na matendo amengineyo yote yanayohusu usalama wa raia na kama mmmoja mmoja au kundi au Taifa kwa ujumla una jicho la tatu ambalo kazi yake ni kukusanya profile za kila mmoja wetu.
Linatakiwa shirika lenye picha ya utaifa na sio picha ya chama au kikundi cha watu. Shirika ambalo watu wake wanakula yamini [Kiapo] kulilinda Taifa, watu wake, na Mali asili zake zote, wakati wowote na saa yoyote ile. Shirika ambalo walioajiliwa kwake wawe ni watu wenye uadilifu [integrite] na welevu [Intellegency] wa hali ya juu katika nyanja zifuatazao
1: Uchumi
Katika Nyanja hii ambayo kwa sasa ndio hujuma nyingi za kuatarisha usalama wa Taifa ziliko lala kwa kiwango kikubwa sana. Kulingana na dhama na nyakati za sasa.
- Tunahitaji walinzi waelevu wenye ufahamu mkubwa sana wa maswala ya uchumi ndani na Nje ya Nchi. Ambao watajua mbinu za kiarifu zenye nia ya kuhujumu Taifa kupitia sekta ya uchumi na wao pia kutoa ushauri makini ni kipi kifanyike kupambana na adui anaekuja kuhujumu Taifa kutoka ndani au nje ya Taifa.
- Tunahitaji wasomi na wanausalama waliofunzwa kupredict future ya uchumi kulingana na taarifa zao za kiusalama walizokusanya.
- Tunahitaji walinzi ambao dakika zote masikio yao na macho yao yanawaza na kuota mbinu na mikakati ya kutulinda sisi Watanzania na kuibua tafiti za kisasa yani za kitaalamu zaidi zitakazo wasaidia wao kujenga na kuunda maliasili watu kwenye sekta ya uchumi na kutoa taadhali ya tishio lolote linalotishia uvunjifu wa amani kupitia sekta ya uchumi.
- Tunahitaji shirika ambalo litawajibika kwa mujibu wa UKWELI [FACTS] na sio majungu ya nani anaogopeka Serikalini. Manake anaeogopeka leo Serikalini kesho anaweza kuwa ndiye adui number moja wa TAIFA.
Tufike sehemu tuseme basi kuwa TAIFA lahitaji mfumo wetu wa kisasa wenye kuzingatia mazingira ya kitanzania na uafrika. Watu watakao kuwa tayari kuunda mikakati ya kulisaidia TAIFA kuinuka kiuchumi. Watakaoibua na kubuni mbinu kuu za kuinua uchumi kupitia ushauri kwenye Serikali.
2: Ulinzi wa Taifa
Hapa tunahitaji aina mpya ya walinzi ambao watakuwa macho kulinda Taifa,watu wake, na mali zake. Hapa ni sehemu ambayo walinzi wake watakuwa na changamoto za kuahakikisha wanakusanya Taarifa za ulinzi ndani na Nje ya Nchi. Teknolojia imekuwa ulinzi kwa sasa unahitaji maarifa ya kutumia mitandao kutoa taarifa na kukusanya taarifa. Mbinu na mikakati yetu iwe ni ile ya kisasa yenye muda mkubwa wa kufikilia zaidi usalama wa TAIFA kwenye pande angle nyingi na sio angle ya ulinzi wa viongozi na bali ni TAIFa kwa ujumla wake.
3: Siasa
Tuwe na shirika linaloangalia siasa kama njia tu, na sio msingi imara wa kulinda TAIFA, wanausalama watakao kuwa makini kuona kofia ya siasa haizidi kofia ya nguvu ya umma au TAIFA. Ni wakati mwafaka wa kutambua NCHI ndio nguzo ya UTAIFA na sio siasa kuwa ndio UTAIFA wenyewe. Kusimamia Demokrasi kwa jicho la ndani na sio jicho la upendeleo wa kiitikadi bali kuongozwa na kusimamia maadilli ya NCHI dhidi ya siasa. Tunatakiwa Shirika ambalo alitatumika kwa faida ya chama, Mtu au kikundi cha watu bali ukweli Taifa lianitaji nini kutoka kwenye siasa.
4: Fedha
Ni wakati mwafaka wa kuwa na shirika lenye maarifa na mbinu zote zenye uwezo wa kubaini michezo mibaya dhidi ya TAIFa kupitia kofia ya kifedhaTaifa linaitaji watu wenye welevu kutambua hujum za kitaifa kwenye mazingira ya kifedha, mfano michezo hiyo ni kama Pesa halamu [Money Laundering], wizi, udanganyifu, utapeli na matumizi mabaya ya fedha ya umma kwenye wizara na mashirika ya umma na sehemu nyingine yeyote ile hata sekta binafsi ambako Serikali yetu ina interest zake.
5: Afya
Pia huku nako taifa laitaji watu makini kujua taarifa za kiafya za Taifa na watu wake, kuahakikisha uwepo wa Taarifa nyeti juu ya usalama wa watu wetu na mali ya asili yetu. Afya ni kitu cha msingi kwa mwanadamu yeyote yule. Hivyo ulizni wetu kama Taifa ni vyema pia tukazingatia AFYA. TAIFa lenye watu wagonjwa ni kuhatarisha amani na usalama wa TAIFA,
6: Elimu
Elimu ni siraha kubwa sana, ikitumika vizuri elimu uleta mapinduzi ya fikra, hivyo TAIFA linaitaji Wanausalama wabunifu na wenye maono kwenye sekta ya elimu. Watakaotoa mwongozo wa elimu sahihi itakayo tumika kujenga na kuinua Taifa.
7: Madini na Malia asili
Sekta hii kwa kuwa ni nyeti tunaitaji ulinzi makini na wenye upeo mkubwa,kupambanua maarifa na utekelezaji wenye kukinga,kujenga na kutetea malia ya asili ya TAIFA.
8: Sekta ya Utamaduni
Ni vyema ujio wa Shirika hilo ukaja na maarifa yenye kujenga na kutetea Utamaduni wa Mtanzania. Ni sehemu hizi ni mwanya kutumika vibaya kuhalibu jamii. Na hivyo shirika litakuwa ni jicho la jamii na jicho la jamii linaona mbali.