Tunahitaji mwanasheria kutusaidia hili

Tunahitaji mwanasheria kutusaidia hili

wanatamani

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2011
Posts
415
Reaction score
145
HABARI WANA JAMVI
MIMI SI MTAALAMU WA SHERIA
NAOMBA KUJUA NINI SHERIA INASEMA MTU ANAPOAMUA KUJENGA KWENYE ENEO LAKO BILA MAKUBALIANO YEYOTE.

SISI FAMILIA, TUNA SHAMBA LETU JIRANI TUPO NA VIWANDA VYA MAFUTA, KUNA MUWEKEZAJI AMEJENGA KIWANDA NA KUPITISHA BOMBA LA MAFUTA KUPITIA KATIKATI YA ENEO LETU UREFU WA MITA HAMSINI 50 NA KUELEKEA ENEO JENGINE HUKO HATUJUI LABDA ANA MAKUBALIANO NAO SISI KAMA FAMILIA HATUJAWAHI KUKUTANA NAE KUFANYA MAKUBALIANO YEYOTE, JUU YA UWEKAJI WA BOMBA HILO AMEJIAMULIA MWENYEWE.

TUNAHITAJI MWANASHERIA ATAKAYEWEZA KUTUSIMAMIA MWANZO MWISHO ILI KULIPWA TUTAKACHO HITAJI.
MALIPO NI MAKUBALIANO BAADA KAZI KWA ANAYEONA ANALIWEZA HILI NA ANAHITAJI KUTUSAIDIA ANAKARIBISHWA

email: wanatamani@gmail.com mobile 0715 387545 PRIVATE RUKSA
 
hiyo ni civil wrong ndugu,inafall under tress pass to land,kwanza wataarifu nia na dhumuni lako ili wajue la kufanya,pili kama hamtofikia mwafaka utaenda mahakamani kufungua kesi ya madai ukiomba ulipwe fidia kutokana na kuingilia shamba lako,hasara uliyoipata na utakayoendelea kuipata nk. pia waweza omba injunction order mahakamani kuzuia ujenzi zaidi ktk shamba lako,,muhimu hati muhimu za umiliki wa shamba ziwepo ili kusaidia mtiririko wa kesi
 
Mkuu wanatamani,kama uko dar tuwasiliane. Jua ya kwamba,Wakili halipwi mwisho wa kesi. Hulipwa kabla na wakati wa kesi. Contigent fees are not allowed in our profession.
 
Last edited by a moderator:
Yawezekana pia kuna ndugu yenu kawazunguka kachukua cha juu katoa kibali bomba lipite.

Hizi mali za familia huwa zina mambo sana. Ulizaneni vizuri kabla hamjachukua hatua. Kama kosa limefanyika wadau juu washaeleza hatua za kuchukua
 
*Contingent*

And where exactly are they not allowed?

Ipo case law, ime set precedent kwamba malipo ya wakili yanayolpwa baada ya kesi na kutegemea maamuzi ya kesi hayakubaliki katika sheria zetu za bongo, kesi hiyo ni ya mkono dhidi ya mteja wake mmoja(sikumbuki jina) na pia citation yake sikumbuki uulizia utaipata.
 
Oh...kumbe bongo ndo hayaruhusiwi.....
 
Mkuu wanatamani,kama uko dar tuwasiliane. Jua ya kwamba,Wakili halipwi mwisho wa kesi. Hulipwa kabla na wakati wa kesi. Contigent fees are not allowed in our profession.

Are you sure? And are there not exemption to the general rule?
 
Last edited by a moderator:
Ipo case law, ime set precedent kwamba malipo ya wakili yanayolpwa baada ya kesi na kutegemea maamuzi ya kesi hayakubaliki katika sheria zetu za bongo, kesi hiyo ni ya mkono dhidi ya mteja wake mmoja(sikumbuki jina) na pia citation yake sikumbuki uulizia utaipata.

Pia citation siikumbukuki ila ni mkono vs Ladwa , ila zipo nyingine na pia Advocates Act ina kifungu kinachozungumzia hilo.
 
kwanza kabisa kabla sija ingia kwenye subject, naomba kikuelimishe kuwa kisheria hairuhusiwi mteja kukubaliana na mwanasheria kuwa atamlipa baada ya kesi,kama atashinda hii ni kwa kuwa kufanya hivyo kutamfanya mwanasheria awe na interest ktk kesi hiyo hivo kutumia njia yoyote ile ili ashinde akiogopa kutolipwa kama hato shinda. hivyo kama unataka mwanasheria sio habari ya kusubiri kesi iishe ndio umripe au makubaliane nini utamlipa. manakubaliana pesa utakayo mlipa kabla na utamlipa hata kama utashindwa kesi.refer the case of MKONO AND COMPANY ADVOCATES VS. LADWA.
 
nikija katika issue yenyewe, hiyo kweli ni tresspass to land , ambayo inaweza kuwa kosa la madai na ia jinai. hata hivyo kama uta institute kama jinai hakuna fidia utakayo pata. kinacho takiwa ni kufungua kesi ya madai under tresspass to land na kuiomba mahakama ulipwe fidia kutokana na hasara ulizo pata kwa ujenzi wa bomba hilo. hata ivyo ili uweze kulipwa fidia lazima uithibitishie mahakama kuwa kuna hasara ulipata. kesi hiyo ni rahisi sana kama una wakili na vithibitisho vya umiliki halali wa ardhi hiyo.
 
Mkuu wanatamani,kama uko dar tuwasiliane. Jua ya kwamba,Wakili halipwi mwisho wa kesi. Hulipwa kabla na wakati wa kesi. Contigent fees are not allowed in our profession.

Kiongoz sasa hapo kwa walala hoi si itakuwa tabu kidogo kupata haki, kama mtu huna kitu kwa wakati huo
 
Last edited by a moderator:
kwanza kabisa kabla sija ingia kwenye subject, naomba kikuelimishe kuwa kisheria hairuhusiwi mteja kukubaliana na mwanasheria kuwa atamlipa baada ya kesi,kama atashinda hii ni kwa kuwa kufanya hivyo kutamfanya mwanasheria awe na interest ktk kesi hiyo hivo kutumia njia yoyote ile ili ashinde akiogopa kutolipwa kama hato shinda. hivyo kama unataka mwanasheria sio habari ya kusubiri kesi iishe ndio umripe au makubaliane nini utamlipa. manakubaliana pesa utakayo mlipa kabla na utamlipa hata kama utashindwa kesi.refer the case of MKONO AND COMPANY ADVOCATES VS. LADWA.

Hiyo ni general principle lakini ukisoma court of Appeal Rules utagundua kuna exemption, kwa hiyo kama unataka kutoa elimu jaribu kugusa pande zote
 
*Contingent*

And where exactly are they not allowed?

Mimi kwa fikra zangu nahisi wewe jamaa umesoma LL.B maana kwenye mambo mengi yahisuyo sheria you are mostly there...i could be wrong...and right but not wrong and right at the sametime...
 
Mimi kwa fikra zangu nahisi wewe jamaa umesoma LL.B maana kwenye mambo mengi yahisuyo sheria you are mostly there...i could be wrong...and right but not wrong and right at the sametime...

Hahaaa yakhe mi mbeba maboksi tu.
 
Back
Top Bottom