TUNAHITAJI parliamentary democracy (system ) sio kuendelea chini ya Presidential democracy (system )

Na kweli huu mfumo uliopo watawala wanaupenda sana na hawaoneshi hali ya kutaka kuuacha
 
Kuna mwamba alitoka bungeni akisema anaenda kuimarisha chama ambcho kilikuwa na zaidi ya 95% ya wabunge
 
Naunga mkono hoja, hii madaraka yote ya nchi kupewa rais ndio imechangia mifumo yote kuwa dhaifu, na kufanya kwa maagizo kutoka juu, kuliko kufuata katiba na sheria. Na ubovu unaongezeka maana rais hashitakiwi akiwa madarakani au ametoka.
 
Tatizo sio mfumo,
Nchi kama Marekani, South Korea na Brazil zinatumia Presidential system, na bado ni moja kati ya nchi zenye mafanikio makubwa zaidi duniani.

Haijalishi unatumia mfumo bora kiasi gani, as long as utahitaji watu kuuendesha au watu kama sehemu muhimu ya huo mfumo

Kama hao watu ni wendawazimu, mfumo mzima utaonekana wa kijinga.

Unaweza kuwa na hata mfumo wa ki dikteta na ukaonekana mzuri kama watu wanaounda huo mfumo wana maslahi mapana ya nchi kichwani na miyoni mwao.

Issue sio system, issue ni incompetent leaders wanaounda hio system, huwezi ongozwa na wajinga na mambo yakaenda sawa

Na wajinga hawa wapo vyama vyote.

Tatizo la hapa kwetu halijawahi kuwa chama, wala mfumo.
 
Naunga mkono hoja, hii madaraka yote ya nchi kupewa rais ndio imechangia mifumo yote kuwa dhaifu, na kufanya kwa maagizo kutoka juu, kuliko kufuata katiba na sheria. Na ubovu unaongezeka maana rais hashitakiwi akiwa madarakani au ametoka.
Kwetu Rais ni small god hagusiki hata kidogo
 
Yes, tunawatu wapuuzi katika system pia system ina ubovu mkubwa kwa uimara wa taifa nchi kama U.S.A mabunge yao yote yana nguvu kama ilivyo tu taasi ya Urais hakuna wa kumtawala mwenzake Presidential democracy ya U.S.A ni tofauti na ya hapa bongo
 
Kiongozi hili jambo ni muhimu sana na mimi naunga mkono hoja kwa kuwa Jambo lolote halitakalo Rais ndio linalazimishwa liwe hata kama halina maslahi kwa Taifa, kama hilivyo sasa Rais Samia anautaka mkataba wa Bandari kuliko Mtanzania yoyote yule, kumkosoa, Kuhoji au kumshauri ni uadui, sio sawa, nchi yetu sote lazima Rais ahojiwe.
 
Kwetu Rais ni small god hagusiki hata kidogo
Na kosa hili lilifanyika wakati wa Nyerere baada ya kutungwa katiba ya kumfurahisha na kuhakikishia anabaki madarakani atakavyo. Matokeo yake kwa sasa mifumo yote iko kumuogopa na kumsujudia rais. Kwa bahati mbaya sana, mfumo huu hautaweza kutoka kwa njia ya amani, bali machafuko ama mapinduzi ya kijeshi.
 
Yes, tawala zote zilizokuwa na madaraka ya Kimungu hapa dunia historia inatuelekeza kuwa hazikudodoka kwa amani bali fujo
 
Umesema point sn
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…