Bugududu Sududu
JF-Expert Member
- Apr 19, 2014
- 600
- 700
Habarini wana jamvi,
Ujumbe kwa mkuu wa mkoa wa mwanza,mkurugenzi wa jiji pamoja na uongozi wote wa mkoa,Tatueni kero hii ya ukosekanaji wa mataa katika barabara ya makongoro kuelekea Airport awali kabla ya upanuzi barabara hii ilikuwa na taa baadhi ya sehemu.
Serikali ilipoa amua kuifanyia upanuzi kutokana na kauli ya Rais wa wakati ule JPM taa zile ziliondolewa kupisha upanuzi lakini jambo la ajabu ni kuwa barabara hii imekamilika toka mwaka 2017 na kuanza kutumika lakini hadi leo hii ni takribani miaka 4 taa za barabarani hazijafungwa.
Alipokuja Rais Mama Samia katika ufunguzi wa jengo la Benki kuu tawi la mwanza serikali ya mkoa iliingia gharama kufunga taa za LED 38W mbili kila nguzo kuanzia lilipojengo la CCM Mkoa hadi yalipo makutano ya barabara ya kuelekea mwaloni hii yote ni kumpiga mama changa la macho.
Juzi tumesikia waziri mkuu Mh kassimu majaliwa amekataa kufungua barabara ya nangulukuru huko Lindi barabara imekamilika lakini alikataa kwakuwa bado haijawekewa taa za barabarani.Sasa kwanini hapa barabara ilikabidhiwa bila kuwekwa taa na ikapokelewa?
Na Waziri mkuu Kassimu mjaliwa aliwahi kusema barabara zote zilizojengwa zina bajeti ya mradi wa taa za barabarani.
Hivyo sisi wakazi wa mwanza tunaiomba serikali pamoja na serikali ya mkoa kupitia upya na kuziangalia barabara zetu haswa barabara ya Nyerere, barabara ya kenyatta na barabara ya mkongoro ziwekewe upya mradi wa taa za barabarani hili pia litapunguza vitendo vya uhalifu kama vile ukabaji, uporaji na ajali za usiku zinazosababishwa na maruweruwe yanayotokana na taa za magari.
Serikali yetu sikivu tunaomba hili mliweke kwenye utekelezaji.
Asanteni.