Tunaiomba Serikali itueleze hatma ya shamba la mifugo la Utegi

Koryo2

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2016
Posts
2,056
Reaction score
2,519
Sisi wananchi wa Vijiji sita vinavyozunguka shamba hilo tulipewa shamba hilo baada ya kukidhi masharti tuliopewa na Serikali.

(1) Sharti mojawapo ni kutolipwa fidia ya uhamisho kwa wananchi waliokuwa wanaishi katika shamba hilo.

(2) Kulipa kiasi cha Tshs.90,000,000 sharti lililotekelezwa na mwanachi kutoka familia ya vijiji hivyo. Serikali ilikuja baadaye kuwanyang'anya wananchi shamba lao bila maelezo ya msingi.

Wananchi wamezuiwa kulima katika shamba lao na hata kufanya shughuli zozote za maendeleo. Wameletwa maaskari katika shamba hilo na kwa kweli hakuna urafiki kati ya wananchi na hao maaskari na wanawatesa wananchi pindi hata ukikutwa katika shamba hilo.

Jambo hili ameelezwa Mhe. Mbunge na hakuna hatua iliyochukuliwa. Sisi wananchi wa Vijiji sita tunafahamu fika shamba ni la kwetu na mwafaka isipopatikana tutaenda Mahakamani hata ikipita miaka mia. Serikali turudishieni shamba letu.
 
Tatizo wategi na luos ni unafiq hapo wachache wakiitwa chemba haka soa hotel ya lakairo nakupewa posho imeisha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…