Tunaiomba Serikali itupie macho vituo vya mafuta hapa nchini

Tunaiomba Serikali itupie macho vituo vya mafuta hapa nchini

Koryo2

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2016
Posts
2,056
Reaction score
2,519
Kwa siku za karibuni Serikali ilitangaza kushuka kwa bei ya nishati ya mafuta. Jambo hili lilifurahisha sana watumiaji wa nishati ya mafuta lakini liliwakasirisha sana wenye vituo vya mafuta.

Kwa sasajinsi inavyoonekana, wenye vituo vya mafuta kama vile wana mgomo baridi. Vituo vingi ukitaka kununua mafuta unaambiwa kuwa mafuta yamekwisha lakini wakati mafuta yakiuzwa kwa bei ya zamani yalikuwa hayakosekani kwenye vituo. Wengine wanasema kuwa wanayaficha wakitarajia Serikali itapandisha bei ya nishati kuanzia tarehe 1 Julai, 2020.

Kipaumbele cha mfanyabiashara ni kupata faida kubwa, hivyo tunaiomba Serikali itupie macho juu ya tatizo hili la ukosefu wa nishati ya mafuta.
 
Dawa ni moja tu, na wewe anzisha kituo cha mafuta halafu yafiche hadi julai 1, sawa?
 
Back
Top Bottom