Tunaiomba serikali utatuzi wa changamoto ya Daraja Lililopo Tabata Mwananchi/Kisiwani

Yofav

JF-Expert Member
Joined
Mar 12, 2021
Posts
4,236
Reaction score
7,583

Hizo ni baadhi ya picha za kabla ya mvua.
Baada ya mvua kidogo tuu matokeo ni haya hapa⬇️



Kinachouma na kusikitisha kabisa ni kwamba hili Daraja lipo karibu kabisa na office ya serikali za mitaa lakini viongozi wa hapo hawaoneshi kabisa kuoina issue hiyo kama changamoto licha ya kuwa imekuwa kero kwa wananchi wa eneo hilo kwa kuwabidi kuzungukia katika njia ya jirani ambayo ni maalumu kwaajili ya Tain/Rail way na hii ndiyo njia pekee ambapo wananchi wote waishio Tabata Kisiwani huitumia kuingia na kutokea mtaani.

Kwa akili zangu za haraka inaonekana sehwmu hii ingeshafanyiwa marekebisho ila ni dhahiri kwamba kuna viongozi wanaokwamisha hilo.

Ni aibu sana kuona sehemu ambayo ipo ndani ya wilaya ya Ilala kuwa ya hovyo namna hii huku ikihesabiwa kuwa ndani ya Jiji.

Naomba kero hii iwafikie viongozi husika wa eneo hili maana hata huyo mbunge toka achaguliwe inaonekana hamna kitu anachokifanya maana kama kweli anaelewa nini anafanya basi hili Daraja ambalo ndo kama mlango wa kuingia na kutokea kwa wananchi wake angeliacha katika hali hii hadi awamu inapinduka.

Shame.
 
Hii ndiyo Dsm, wenyewe wanajinasibu kuliita Jiji la 'maraha'
 
Raia unalipa kodi halafu unaiomba serikali? Endeleeni kufanya hivyo muone kama litatengenezwa. Wenzako wameagiza magari ya kifahari kwanza. Njia pekee ya kufanya ni kujiunga kwenye maandamano.
 
Kaka Viongozi wanaokalia viti ndo wanatuua kinomanoma
Raia unalipa kodi halafu unaiomba serikali? Endeleeni kufanya hivyo muone kama litatengenezwa. Wenzako wameagiza magari ya kifahari kwanza. Njia pekee ya kufanya ni kujiunga kwenye maandamano.
"The right cannot be given as a gift by the oppressor it must be demanded by the oppressed."
Martin Luther King Jr
 
Raia unalipa kodi halafu unaiomba serikali? Endeleeni kufanya hivyo muone kama litatengenezwa. Wenzako wameagiza magari ya kifahari kwanza. Njia pekee ya kufanya ni kujiunga kwenye maandamano.
Inabidi uiombe tu mkuu maana katika watu 100,000 unaweza kukuta mimi pekee yangu ndo nimekata tamaa na hali hiyo huku wengine wakiwa bado wana uvumilivu ndo maana wakakaa kimya.
 
Ifikie mahali watanzani tuache kulialia na kauli za tunaiomba serikali ili hali Serikali iliyopo imeshindwa kuongoza nchi alafu tena unaendelea kuiomba. Muhimu tuje na mbadala mwingine wa kuweza kutatua matatizo yetu ya ujinga na umaskini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…