Tunaishi duniani ili tufe

Tunaishi duniani ili tufe

BestOfMyKind

JF-Expert Member
Joined
Apr 26, 2012
Posts
1,350
Reaction score
1,464
Yaani kama una uhai leo jua utakuja kufa tu.
Kwahiyo punguza kuchakarika, kujivimbisha, kutukana watu.
Utakufa na hutokuwepo tena duniani.
Kiburi na majivuno yako yote hayatakua na maana na wala havitakuwepo duniani tena.
Umezaliwa ili uje ufe na hili haliepukiki.
 
Kwanini tunapambana kuishi kama tunaishi ili tufe ?

Why are dying to live, if we are just living to die ?
 
That's the philosophical dilemma, why do we struggle to live only to die in the end?
 
Fanya utafiti kujua kwanini tulikuja duniani, kuna sababu ya wewe kuwa hapo ulipo. Ila hiyo uliyosema sio sababu ya msingi
 
Sheria za maisha ni mbili tu

1.Survive
Hii ndio sheria ya msingi, hakikisha unakua "hai",
Kumbatia kitu chochote kinacho kuongezea "nafasi" ya kuishi

Mfano, chakula bora, Mazoezi, Usafi, Maarifa, Ku socialize na rafiki, etc.

Achana na vitu vinavyo kupunguzia nafasi ya kuishi kama Kuendesha gari ukiwa umelewa, utumiaji wa madawa ya kulevya, ugomvi, msongo wa mawazo, lishe duni, kutofanya mazoezi, huzuni, etc

2.Reproduce
Kwa sababu huwezi kua "hai" milele hata kama utazingatia yote hayo, kuna mda utazeeka

Kwa kuzaliana, "nature" inakupa nafasi ya kuingia kizazi kijacho, na kuhakikisha jamii ya binadamu inaendelea kuwepo.

Hakikisha unaacha. Watoto wa kutosha. (angalau kwanzia watatu)

Maisha hapa duniani yanataka hivyo tu,
Tazama hatua zote alizopiga binadamu, vumbuzi zote za sayansi na teknolojia lengo ni kuhakikisha tunaendelea ku survive na ku "reproduce"
 
"Zaeni mkaongezeke, mkaijaze nchi"
 
Mtu ameumbwa aishi milele. Maisha ya kukaa kwenye mwili huu yana kipindi chake, muda ukiisha mtu anauvaa mwili wa roho maana yake anaendelea ku-exist kwenye spiritual world. Mtu aliyemwamini Yesu anaendelea kuishi huko peponi (paradiso) japo duniani wanakuwa wanasema amekufa. Ambaye hakumwamini Yesu anaendelea kuishi kwenye eneo liitwalo kuzimu; lenye giza sana na mateso mengi(sio jehanamu lakini). Maana jehanamu ni baada ya hukumu ya mwisho.

Maisha ya milele na Yesu (kwenye mbingu mpya na nchi mpya) ama maisha ya milele na Shetani (kwenye lile ziwa liwakalo moto). Wakati wa kufanya uchaguzi ni sasa.

USHAURI: Amua kumpa Yesu maisha yako (KUOKOKA) ili awe ni Bwana na Mwokozi wa maisha yako hatimaye ukae naye milele. Huu ndio uzima wa milele.

On myself, "I AM A SPIRITUAL BEING WITH HUMAN EXPERIENCE".

YESU NI MWOKOZI.
 
Yaani kama una uhai leo jua utakuja kufa tu.
Kwahiyo punguza kuchakarika, kujivimbisha, kutukana watu.
Utakufa na hutokuwepo tena duniani.
Kiburi na majivuno yako yote hayatakua na maana na wala havitakuwepo duniani tena.
Umezaliwa ili uje ufe na hili haliepukiki.
Ili tuonje joto yajiwe
 
Fanya utafiti kujua kwanini tulikuja duniani, kuna sababu ya wewe kuwa hapo ulipo. Ila hiyo uliyosema sio sababu ya msingi
Utafiti umeshafanywa, kwa miaka zaidi ya 2000 binadamu wameishi na kufa. Katika kipindi chote cha milenia 2 hakuna aliyewahi kuishi bila kufa. End product ya maisha ni kifo.
If you live, you will die.
Mengine hayo ya ufufuo ni kujipa matumaini tu.
Ugunduzi wa ulimwengu na vilivyomo ( planetary discovery) unafifisha matumaini ya uwepo wa maisha baada ya kifo.
 
Yaani kama una uhai leo jua utakuja kufa tu.
Kwahiyo punguza kuchakarika, kujivimbisha, kutukana watu.
Utakufa na hutokuwepo tena duniani.
Kiburi na majivuno yako yote hayatakua na maana na wala havitakuwepo duniani tena.
Umezaliwa ili uje ufe na hili haliepukiki.
Mimi ninaishi ili nile.
 
Back
Top Bottom