Tunaishi kuleee mbali nyuma, Wenzetu wanaishi kuleee mbali mbele.

Tunaishi kuleee mbali nyuma, Wenzetu wanaishi kuleee mbali mbele.

Nangu Nyau

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2022
Posts
5,015
Reaction score
14,139
Lazima tukubaliane tunafikiri na kuishi kizamani sana wakati wenzetu wanaishi na kufikiri miaka mingi mbele.
Haya yanayoendelea lazima tufahamu hakuna shida nyingine zaidi ya watu wenye uelewa mdogo kwenye mifumo na huku mitaani.

Maendeleo ni process na mipango mikali kuikamilisha hiyo process, hatuna process yeyote tuliyonayo practically baadala yake tunamipango mibovu kukamilisha kisichooneka, HATUNA TOFAUTI NA TIMU INAYOBUTUABUTUA UWANJANI ILI MPIRA UISHE.

Ifike mahala tukubaliane sasa, kama Taifa tunahitaji watu miongoni mwa watanzania nje ya mifumo inayotumika sasa kupata watu, Watanzania zaidi ya milioni 60 tukiweka ushindani na kutafuta "brains" (akili) tutazipata hata kama chache lakini zitatutoa na kuleta touch (mguso mpya). TUMEKWAMA tunakimbia kimbia hovyohovyo kama mwizi aliyekosa uelekeo, tunahitaji uelekeo na namna bora ya kuufuata huo uelekeo na sio kubahatishabahatisha.

Wazee wote mnaofikiri mlio kwenye mifumo, wanasiasa wenye akili timamu, viongozi wa dini nk tambueni mnakwenda kuwaacha vijana wenu utumwani maana huko mbele watakuwa wamezidiwa akili kila mahala kwa sababu ya ubinafsi wenu wakutokubali sasa Taifa linahitaji ushiriki wa watu wote kwenye kuliongoza na kuliendesha.

Mifumo mibovu wa kusajili watu kwenye taasisi mbalimbali, mashirika, vyama vya siasa, mashuleni, mavyuoni, taasisi nyeti nk umeacha "big brains" nyingi sana nje na matokeo yake umesajili vilaza aka vichwa vibovu vingi ambao wanakwamisha kila kitu ili waendelee kuwepo.

Nisiwachoshe sana, TUMEKWAMA SIO LEO TU, JANA, JUZI, JUZI KAZI, NA MAJUZI YALE ETI KWA KUAMINI TUNAWEZA HUKU SIO KWELI.
 
Back
Top Bottom