Tunaishukuru TBC kuonesha Kombe la Dunia 2022, lakini kulikuwa na mapungufu mengi

Kodi zetu zinatosha kuonyesha mechi zote bila kufirisika, Ni Kodi zetu haitoki mfukoni kwa mtu.
Mimi kwa ninavyofahamu DStv kwa kupitia channel Yao ya Supersport ndiyo walinunua haki za kurusha matangazo kwa nchi za Kusini mwa jangwa la Sahara.., then Channeli za Taifa kama Tbc kwa Tanzania na Kbc kwa Kenya walikua wanapewa mechi kadhaa tu za kuonyesha, so tusiwalaumu TBC sio kosa lao kuonyesha mechi 28 Mkuu
 
Tutafute Pesa!! TBC sio chanel ya michezo
Kwakweli, Bora wangeacha kama miaka yote. Iliwatibulia biashara DStv. Kuna siku unadhani mechi itaonyeshwa ukifungua channel ya TBC unakutana na habari ya Waziri Mkuu kamsimamisha Mkurugenzi Katavi, unasonya hadi basi.
 
Kodi zetu zinatosha kuonyesha mechi zote bila kufirisika, Ni Kodi zetu haitoki mfukoni kwa mtu.
Hizi ni Biashara za watu ndio maana TBC ikapewa mandate ya kuonyesha mechi 24 na sisi tuliolipa 56,000 ya compact DSTV tumeangalia zote 68.
Hamna habari ya Kodi hapa.
 
TBC ni chombo umma wa watanzania kinachoendeshwa kwa Kodi za watanzania wote. Ninamshukuru waziri mwenye dhamana ya michezo, waziri wa habari na mawasiliano na Mkurugenzi wa TBC kwa kuwafikiria matajiri wao (walipa Kodi) kuwaletea matangazo ya moja kwa moja kutoka Qatar, ahsanteni sana kwa kuwaza jambo hili. Labda shukrani nyingi zaidi ziende kwa Rais Dr. Samia kwa kuruhusu hili lifanyike kwa kutumia Kodi za wananchi, umeupiga mwingi kwakweli.

Lakini shughuli nzima ilikuwa na mapungufu yafuatayo.
1. Kukosekana kwa baadhi ya mechi. TBC haikuonyesha mechi zote, kama vile ilikuwa inatufanyia hisani TU watanzania kwa kutuchagulia mechi ipi tuangalie na ipi tusiangalie.

2. Kuchanganya channel ya matangazo ya taifa na michezo pamoja. Tulitegemea TBC ingekuwa na channel ya sports ili kuepuka kuchanganya matukio ya kitaifa na serikali na michezo.

3. Wachambuzi wa mpira hawakuwa na ubora. Wanaborongaboronga TU wakati hii ndiyo TV ambayo ingetakiwa na Quality wachambuzi.

4. Watangazaji wa mpira. Hawakuwa na mvuto zaidi ya kujua kiarabu TU. Hawavutii kuwasikiliza, unatamani waache kusimulia ili tuangalie TU wenyewe.

Ushauri: Sisi ndio wenye TBC, hivyo matangazo ya mpira lazima yawe ALL or NONE, sio vuguvugu kama vile. Bora muache kabisa ili watu wajioange kuliko vile. Chukueni wachambuzi ikiwezekana kutoka media nyingine binafsi. Kulikuwa na ugumu gani kutumia channel ya TBC2 au nyingine kwa michezo TU?

Ahsante ni TBC

Uliza kwanini ilikuwa hivyo sio unalalamika kama ma••ya aliyenyimwa chake
 
Fatilia Kwanza kwanini walionesha mechi 28, halafu kuwa na shukrani ,pili watangazaji hawakuwa na tatizo lolote ,ujuaji wenu ndio uliwafanya muone hawafai,

Kwa taarifa yako yule dogo Upete aliyekuwa anatangaza ana mix na kiarabu kapendwa Sana kuliko wajuaji wachache Kama wewe, na soon ataondoka TBC ,Azam media wameshaanza kumnyemelea
 
Sema tu ume-mind kwa sababu jamaa alikuwa anaongea kiarabu, ila angeongea kiingereza wala usingekuka kulalamika hapa.
 
Hizi ni Biashara za watu ndio maana TBC ikapewa mandate ya kuonyesha mechi 24 na sisi tuliolipa 56,000 ya compact DSTV tumeangalia zote 68.
Hamna habari ya Kodi hapa.
hizo 24 tumelipiwa na nani au tumepewa bure kama hisani? mbona hata hizo 24 kulikuwa na matangazo kibao ya kibiashara? Kusema hivo ni kuwadharau walipakodi na watoto wao na kukumbatia wakwepa kodi.
 
Uliza kwanini ilikuwa hivyo sio unalalamika kama ma••ya aliyenyimwa chake
wewe ndiye uliyetakiwa kutueleza kwanini ni mechi 24, kwani ni wachambuzi wabovu, ni kwanini ni watangazaji wa vile wanaoongeza kireno na kiarabu na wapiga kura (mabosi zake) sio mimi nikuulize kwanini ilikuwa vile. Kama ilikuwa ngumu si bora ungeacha kabisa iwe kama inavyokuwaga? Kitu cha serikali siku zote na mara zote lazima kiwe bora na madhubuti kuliko vitu vingine kwakuwa vitu vya serikali ni ALL or NONE, hakuna mitumba.
 
Sema tu ume-mind kwa sababu jamaa alikuwa anaongea kiarabu, ila angeongea kiingereza wala usingekuka kulalamika hapa.
Kaka Kiingereza ni letu yetu ya taifa, tunaizungumza na kuitumia kujifunzia tangu chekechea hadi hadi vyuo vikuu. Huna hoja hapo na wala siko huko kwakuwa hata mimi ni sheikh vilevile hivyo sina chuki na KIARABU, lakini je ni sahihi mtangazaji kwenda hewani kwa kiarabu kuwasialana na watanzania?
 
Fatilia Kwanza kwanini walionesha mechi 28, halafu kuwa na shukrani ,pili watangazaji hawakuwa na tatizo lolote ,ujuaji wenu ndio uliwafanya muone hawafai,

Kwa taarifa yako yule dogo Upete aliyekuwa anatangaza ana mix na kiarabu kapendwa Sana kuliko wajuaji wachache Kama wewe, na soon ataondoka TBC ,Azam media wameshaanza kumnyemelea
Hakuna shida yoyote kutangaza kiarabu kwenye media ya Azam lakini sio hii ya TBC ambayo ina sera ya kutumikia umma unaoongea kiswahili na kiingereza tu basi. Hata kama angeongea Kisukuma au Kikwere lingekiwa kosa pia.
 
Kwani unafikiri hao TBC ndio walikaa wakaamua waonyeshe hizo mechi 28?
 
Mimi kwa ninavyofahamu DStv kwa kupitia channel Yao ya Supersport ndiyo walinunua haki za kurusha matangazo kwa nchi za Kusini mwa jangwa la Sahara.., then Channeli za Taifa kama Tbc kwa Tanzania na Kbc kwa Kenya walikua wanapewa mechi kadhaa tu za kuonyesha, so tusiwalaumu TBC sio kosa lao kuonyesha mechi 28 Mkuu
sawa lakini je, walipakodi wanastahili hilo unalolisema, kwanini DStv wasipewe wao hizo 28 na wananchi wakapewa 64? na kwanini mabosi (wapiga kura na walipa kodi) hawakushirikishwa kwenye hilo, mbona kwenye tozo tunashirikishwa na tunalipa?
 
Kwani unafikiri hao TBC ndio walikaa wakaamua waonyeshe hizo mechi 28?
Ndio tuliowakabidhi waendeshe TBC kwa niaba yetu, kama kuna hela zaidi ingehitajika tulipe ili kuona mechi zote siwangetuambia sisi wenye visimbuzi vya taifa vya startime tulipe? mbona kodi na tozo tunalipa?
 
Tafuta hela tbc sio channel ya michezo over mmpewa hisan tu
 
hela ipo ndio maana nina bundle la kutosha kuwaambia ukweli. Kama tbc sio channel ya michezo hizo mechi 28 walionyesha kwa kupitia wapi? nani aliwadai waonyeshe kombe la dunia kumbe huwezi, huna channel ya mpira?. Ni heri wangeacha kabisa ili wananchi wajiandae kisaikolojia kama wanavyofanyaga miaka yote. baba huwezi kununua t-shirt tu kwa mtoto ambae hana nguo kabisa, yaani mtoto matako yako nje huku ukijisifu kuwa umenunua nguo kwa mtoto. Kama wangekuwa wakweli basi wangetoa orodha ya mechi watakazoonyesha na kuisambaza kwa wadau wafahamu mapema ni mechi ipi itaonyeshwa na ipi haitaonyeshwa kwenye mashindano kabla ya mashindano hayajaanza, hii ingewasaidia walipa kodi kuwa na mpango pia. Lakini nimeshuhudia watu wakisonya wakiwa wamekusanyika kuangalia mechi TBC mara wanaona matangazo mengine wasiyoyataka kwa muda ule. Na kuanza kufanya mipango ya kwenda sehemu nyingine wanakoonyesha, it was too late. Kuna watu wanashindwa kupanga kwaajili ya wananchi, matokeo yake wanaichonganisha serikali na wananchi wake.
 
Back
Top Bottom