Habari wana jukwaa,
Awali ya yote niombe kueleza kuwa huwa napenda kukosolewa kwa Hoja pale mtu atakaposema kuwa nimeongea sivyo au nimedanganya. Ninafahamu kuwa humu wamo ambao wameweka nia kwa ngazi ya ubunge na hivyo baadhi tayari wanafahamu kinachoendelea kuhusu nilichokiandika hapa chini.
Mimi ni miongoni mwa watu ambao wanatarajia kuingia katika kinyanganyiro cha ubunge kupitia Chama cha Mapinduzi katika uchaguzi ujao.
Tukiwa kabisa bado tuko katika hatua za awali za maandalizi ya uchukuaji wa fomu, yapo maelekezo ambayo yametolewa na uongozi ambayo yatapaswa kutekelezwa na wale wote waliotia nia au watakaoingia katika kinyanganyiro ndani ya chama.
Mojawapo ya maelekezo haya ni kwamba kila mwanachama atakeyechukua fomu ya kugombea ubunge, mbali na kulipia laki moja, pia atapaswa kulipia kiwango cha ziada kunzia laki tatu na kuendelea (pesa hii inatofautiana kulingana na eneo au Jimbo).
Tumejaribu kuhoji kwa Nini tulipie pesa ambayo haipo katika kanuni za chama, majibu tuliyoambiwa ni kwamba pesa hii haiwezi kuwekwa hadharani kwa mstakabari wa chama, na kwamba pesa Hizi zitatumika moja kwa moja katika kuendeshea mikutano ya wajumbe.
Sina nia mbaya na chama changu, lakini ni vyema kukawa na uwazi katika hili, kwani chama chetu ni chama ambacho kimejipambanua katika kupambana na ufisadi na rushwa, na hivi karibuni mambo Kama haya tumeyashuhudia katika vyama pinzani, na iweje leo yatokee katika chama chetu?
Ni Imani yangu kuwa TAKUKURU watafanyia kazi suala hili na watakuja na majibu sahihi.
Wasalaam.