Fascinating
Senior Member
- May 14, 2025
- 146
- 351
Kuna kauli moja imeibuka baada ya kilichotokea kipindi cha uchaguzi: “Tutalinda amani kwa gharama yoyote.” Imeanza kutumika kama wito wa wajibu wa kitaifa wa kuhakikisha nchi haianguki kwenye machafuko. Lakini ukiichunguza kwa makini, unagundua jambo la kusikitisha, gharama ambayo wengi wako tayari kulipa ni maisha ya raia wa kawaida. Risasi walizopigwa watu, kutekwa na kuuawa, au vifungo kwa wale wanaothubutu kuongea. Hiyo ndiyo gharama inayochukuliwa kuwa rahisi na inayoonekana inafaa kulipwa.
Swali ni kwamba, hiyo ndio gharama pekee inayoweza kulipwa? Je, hakuna gharama nyingine ambayo viongozi wanapaswa kuitafakari, ikiwemo ya wao wenyewe kuondoka madarakani au serikali kuwajibika kwa kuachia nafasi ya mabadiliko ya amani?
Hapa ndipo ninapoona matumizi mabaya ya kauli hii. Badala ya kuwa wito wa kujitolea kwa ajili ya nchi, imekuwa kisingizio cha ukandamizaji, ikiruhusu vurugu dhidi ya raia kwa jina la “amani.”
Kama gharama ya amani ni kuua, kuwapiga, kuwafunga raia, au kuwafanya waogope kila siku, je, hiyo ni amani ya kweli? Amani si kudhibiti watu wanyamaze. Amani ni hali ya kuishi bila woga, bila migogoro inayoweza kuepukika. Lakini mara nyingi, gharama ambayo haifikiriwi kabisa ni ile ambayo inawahusu watawala wenyewe. Rais anaweza kuondoka ikiwa amepoteza uhalali wa kuongoza. Serikali inaweza kuvunjika na kuunda mpango wa mpito wa wapatanishi. Chama tawala kinaweza kukubali kushindwa mapema kabla ya kuiingiza nchi kwenye vurugu. Jeshi linaweza kukataa kuwa zana ya kukandamiza raia na badala yake likawa mlinzi wa wananchi. Hizi ni gharama za heshima, za ujasiri, ambazo zingeokoa maisha na kuzuia nchi kuingia kwenye machafuko.
Historia inatupa mifano ya wazi ya jinsi gharama hizi za uwajibikaji zimefaulu. Wakati Yahya Jammeh alipokubali kuondoka madarakani huko Gambia mwaka 2017, aliruhusu nchi yake ipumue bila kuingia kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe. Alipofanya hivyo, alilipa gharama ya kuacha madaraka yake, lakini akaiokoa Gambia. Vivyo hivyo, Robert Mugabe mwaka 2017 alipokubali kuondolewa kwa amani baada ya shinikizo la wananchi na jeshi, Zimbabwe ilipata nafasi ya kujipanga upya bila damu kumwagika. Ufilipino mwaka 1986, Ferdinand Marcos alipokubali kwenda uhamishoni baada ya maandamano makubwa ya “People Power,” nchi ilipata uhuru bila mapigano makubwa.
Kuna upande mwingine wa sarafu. Ambapo viongozi walikataa kulipa gharama hiyo ya uwajibikaji na matokeo yake hayakuwa mazuri kwa ustawi wa nchi. Kwa mfano nchini Ivory Coast mwaka 2010, Laurent Gbagbo alipokataa kuondoka baada ya kushindwa uchaguzi, zaidi ya watu 3,000 walipoteza maisha, na nchi ikagawanyika kwa miaka mingi. Hili linatuonyesha kuwa kulinda amani kwa gharama yeyote sio tu kutumia nguvu dhidi ya raia bali pia kuona uwezekano wa kuachia madaraka ili kulinda mustakabali wa taifa.
Je, hawa viongozi wetu wako tayari kulipa gharama ya kweli ya amani, yaani, kuondoka madarakani kama hawakubaliki na wananchi? Au gharama pekee inayokubalika kwao bado ni damu ya raia, hofu kwa wananchi, na uharibifu wa nchi kwa ujumla? Amani ya kweli inahitaji ujasiri wa viongozi kuweka maslahi ya taifa mbele ya maslahi yao binafsi. Inahitaji wawe na uwezo wa kusema, “Tumeona dalili za machafuko. Badala ya kuua wananchi, sisi tunang'atuka.”
Tuache kugeuza kauli ya “amani kwa gharama yoyote” kuwa kisingizio cha mauaji, vifungo, na ukandamizaji. Iwe wito wa uwajibikaji, ambapo viongozi wanajitolea kuacha madaraka yao ili kuokoa nchi. Kwa sababu amani ya kweli haihitaji mazishi ya raia, inahitaji ujasiri wa watawala kujiweka chini ya maslahi ya taifa.
Hili si suala la upinzani au uenyekiti. Ni suala la maisha yetu, ya watoto wetu, na ya mustakabali wa nchi yetu. Je, unadhani gharama ya kweli ya amani inapaswa kuwa nini? Viongozi kuwajibika na kuondoka, au raia kuendelea kulipa kwa maisha yao?
Wakuu hebu tujadili jinsi ya kujenga amani ya kweli, ya heshima, na isiyohitaji damu.