Cha kujifunza hapa keangu ni kimoja tuu.
Ukoloni unarudi kwa kasi saaana, bahati mbaya unamshirikisha kijana msomi anayepumbazwa na imani ya kuwa wazungu wanamthamini kea itikadi zake.
Nimshukuru mbowe na jopo lake kwa ujumla, nilichokigundua kutoka kwake hasa tukijifunza na hili sakata la uganda, kuna vitu vingi vinaendelea ndani ya vyama vya siasa na mitizamo ya wanasiasa.
Kuna uwezekano mkubwa kuna nguvu kubwa ya kibepari inayojificha nyuma ya hivi vyama
Ndio Mbowe amejikuta akibalance kuna wanaomsukuma kufanya mbinu za vurugu kwa mgongo wa chama lakini yeye kasimama katikati kwa maslahi ya watanzania.
Nikichogundua ni kwmba mbowe amekwishaliona kuwa wapo watu wa mataifa ya nje kwa maslahi yao wanataka kuwatumia wao kuivuruga amani hii, lakini huyu mzee kaamua kutukingia kifua.
Matharani. Chukulia hili tukio la Uganda ukiwa na uhuru kichwani, wamefanya walichofanya na impact imetoka nje, wakizubaa hawa waganda tutawapa makazi ya wakimbizi hivi punde.
Lakini kwetu lilitokea la kijana wetu machachali na mjuzi wa siasa kupigwa risasi, lakini kwa upinzani imara ulio chini ya mbowe inaonyesha alikataa kata kata kulitumia kisiasa tofauti na wenzetu huko uganda.
Kwa sasa utaiona nguvu kubwa inayohitaji kulikuza hili swala nadhani si kwa maslah ya waganda, kuna watu wananufaika na hiki kitu.
Ni kweli tunahitaji demokrasia kwa kiasi kikubwa tu nadhani hili halina ubishi, katika hili najikuta nalitazama kwa kina kwani hii mifumo tunaiiga kwa wenzetu waliofanikiwa kama Marekani na nchi zingine.
Kinachonishangaza zaidi ni upotoshaji wa demokrasia yenyewe,
Matharani iangalie marekani ambayo ndio baba wa demokrasia
Nikivosikia
IMETHIBITIKA UCHAGUZI WAKE ULIKUWA NA DOSARI BAADA YA MSHIRIKA WAKE MKUU KUKIRI YA KUWA ILITUMIKA PESA KUWANYAMANZISHA WATU HASA WALE WACHEZA SENEMA ZA NGONO.
Hapa napo tunapaswa kujifunza nini??
Na katika uchaguzi huu huu wa marekani ulimpa Trump ushindi
Kulikuwa na tetesi kwamba urusi ameingiria mifumo ya uchaguzi ya marekani ili kuhakikisha Trump anashinda, lakini mpaka leo sijaona hashtags juu ya masuala haya.
Vipi huko hakuna wanaharakati??
Kama mti mbichi unatendwa hivyo, vipi kuhusu mti mkavu??
Nionavyo mimi, harakati za demokrasia zisizozingatia mifumo ya nchi husika kwa kutegemea kutizama mataifa makubwa yamefika wapi ni mwanzo mzuri kwa wazungu kurudi tena afrika kwa kishindo kikuu
TANZANIA KUANZIA UTAWALA MPAKA UPINZANI KUNA MISIMAMO IMARA NA ISIYOTETEREKA BADO.
NDIO MAANA MPAKA LEO LINAPOKUJA SWALA LA AMANI SI WAPINZANI WALA WATAWALA WANATOFAUTIANA.
UNAFIKI WA MKENYA
Haijasahaurika bado kwamba hata wao kuna mtu alisha likimbia taifa hilo kwa kuhofia usalama wake, hakuna hata mbunge mmoja aliyeandamana, leo wao wanakwenda kuandamana katika nchi ya watu kumtoa mtu kwenye vyombo halari vya taifa lao.
Wamesahau ya kuwa hata wao kuna watu wamepoteza maisha katika mchakato wa chaguzia zao ndani ya kipindi kifupi kilichopita, maisha ya wataalam wale si kitu, kubwa kwao ni bobi kuwafanya waandamane
Wamesahau hivi juzi raia wao walikuwa wanateseka kwa kukosekana kwa unga, matatizo hayo si ya kidemokrasia isipokuwa kuandamana.??
Hili taifa lisipoangaliwa kwanjicho la tatu, linaweza likawa ni wakala mzuri wa kuivuruga amani na wakala mzuri wa ujio wa mkoloni kwa mara ya pili
Niishie hapa uzi sio wangu niwape nafasi wengine
(Tundu Lissu)
Tunakukumbuka saana tena saana tumeona unafiki wa watu na tumejua jirani na watu wengine wanaotuzunguka ni watu wa aina gani
Mh. Mbowe najua unapitia wakati mgumu sana tena sana lakini upana wa kifua chako ulivyoyabeba matatizo ya wanainchi ndivo uatakavyobeba baraka zako kutoka kwa Muumba.
Kuna watu wanatamani leo hii ukitangaze chadema kama kikundi cha waasi ili muivuruge amani, lakini wewe umesimamia misingi na sheria.
CCM na nyinyi mkisikia miruzi mingi muwe mnageuka msipotee kama mbwa.
Haya yanayojiri nchi jirani embu chukueni tahadhari nchi yetu bado tunaipenda iwe katika amani
Najua hata nyinyi mnaumizwa vichwa na tuhuma mnazozibeba, lakini pia embu mtafuteni mchawi ni nani ili mtuweke huru na wasiwasi juu yenu.
Sent using
Jamii Forums mobile app