Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,843
- 31,057
Hapo jana ya tarehe 11/12/2020 tulipata taarifa kuwa Bunge la Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo limepiga kura ya kutokuwa na imani naye Spika wao wa Bunge, Jeanine Mabunda kwa namna anavyoliendesha Bunge hilo kwa upendeleo na kujiegemeza kwa Rais Mstaafu, Joseph Kabila, pamoja na chama chake.
Nchi yetu Tanzania tunajifunza nini kuhusu kutimuliwa kwa Spika huyo wa Bunge la Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo?
Ni dhahiri kuwa yapo mengi tunayoweza kujifunza kwa Bunge hilo jinsi lilivyosimamia kanuni zake na kumwona Spika huyo wa Bunge kuwa hafai na hivyo kumpigia kura za kukosa imani naye.
Hapa nchini kwetu tunaye Spika ambaye ameamua kuikanyaga kanyaga Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977
kwa kuwakumbatia wale wabunge wa viti maalum wa Chadema.
Ni sharti la kikatiba kuwa mbunge yeyote anapovuliwa uanachama wake na chama chake, basi hatua inayofuata ni kwa Spika kuiandikia barua Tume ya uchaguzi kuieleza kuwa nafasi hizo za ubunge ziko wazi, kwa hiyo ufanyike mchakato mwingine wa kuziziba nafasi hizo.
Tumepata taarifa toka kwa kiongozi wa Chadema, John Mrema, zilizothibitisha kuwa chama hicho kilishapeleka barua kwa Spika wa Bunge, Job Ndugai, tarehe 29/11/2020 kuhusu maamuzi ya Kamati Kuu ya Chadema, kuwavua uanachama wabunge hao akina Halima Mdee.
Swali tunalopaswa kumuuliza Spika Ndugai ni kwanini anashikwa na "kigugumizi" na hataki kutekeleza sharti hilo la kikatiba kwa kumwandikia barua Mkurugenzi wa Tume, kumjulisha kuhusu kupokea kwake barua hiyo ya Chadema?
Hivi kuna tofauti gani katika uendeshaji wa Bunge kati ya Spika Ndugai na mwenzake Jeanine Mabunda wa Congo aliyetimuliwa kazi kuhusu upendrleo wake kwa Rais mstaafu Joseph Kabila na Chama chake?
Hivi Spika Ndugai ambaye anaonyesha upendeleo wa wazi kabisa kwa Rais Magufuli na chama chake cha CCM, na kuikanyaga kanyaga Katiba ya nchi yetu ni kwanini basi Bunge la nchi yetu lisipange kupiga kura ya kumng'oa kwenye nafasi hiyo ya U-Spika?