Tunajifunza nini kuhusu kutimuliwa kwa Jeanine Mabunda kama Spika wa Bunge la Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo?

Tunajifunza nini kuhusu kutimuliwa kwa Jeanine Mabunda kama Spika wa Bunge la Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo?

Sawa, Endelea itawezekana tu Mkiweza kuruhusu Mwenyekiti wa Chama chenu aache kuibadilisha katiba ili awe Mwenyekiti wa kudumu. Nyani kweli haoni kundule
Hivi unaweza kumlinganisha Mwenyekiti wetu na Mwenyekiti wenu?

Hivi wewe uliwahi kuona wapi ina-printiwa form moja tu ya kugombea Urais, kama kweli huyo Jiwe wenu anakubalika hapa nchini kama mnavyodai?
 
Hivi Spika wa Bunge aliapa kumtii Rais Magufuli au aliapa kuitii na kuiheshimu Katiba ya nchi?

Jibu utakalopata ndiyo argument yangu kuwa ni kwanini Spika Ndugai hatufai kwenye nafasi hiyo ya U-Spika na hivyo anapaswa ang'olewe
Utasubiri sana spika atolewe
 
Najifunza kuwa rais wa DRC naye anatamani udikteta. Ndiyo maana anataka kumweka soika atakayefuata maagizo yake.
 
Kwa Bunge la JMT usitarajie hilo kutokea. Badala yake Wabunge wanapigana vikumbo kujipendekeza Kwa Spika ili 'awaone'.
 
Nilichojifunza ni kuwa mfumo dume AFRICA una tabia mbaya wamemfukuza huyo spika sababu mwanamke kama ambavyo mfumo dume wa Chadema umewaonea kuwafukuza wabunge wanawake viti maalumu akina halima mdee na wenzie
 
Nilichojifunza ni kuwa mfumo dume AFRICA una tabia mbaya wamemfukuza huyo spika sababu mwanamke kama ambavyo mfumo dume wa Chadema umewaonea kuwafukuza wabunge wanawake viti maalumu akina halima mdee na wenzie
Duh.........

Mfumo dume tena??
 
Spika siyo kwamba anasusua kufuata kanuni sheria na miongozo...
Tatizo anaendekeza maagizo kutoja juu...




Cc: mahondaw
 
Usishangae sana, Sisi tupo kivyetu zaidi mkuu. Na hakuna wa kuuliza hivyo tuvumilie tu.
 
Tinachosema ni kuwa Spika Ndugai aliapa kuitii na kuiheshimu Katiba ya nchi, kabla hajaanza kutumikia madaraka hayo, ni kwanini basi anaikanyaga kanyaga Katiba hiyo kwa kutotaka kuitii Katiba hiyo inayomwambia kuwa mbunge yeyote anapovuliwa uanachama wake na chama kilichomdhamini ubunge wake, automatically anakuwa amevuliwa ubunge wake?
Mkuu wala usiwe na shaka malipo ni hapa hapa Duniani. Ndugai alishazoea kuwakemea na kuwanyanyasa Wabunge wa Upinzani hasa Chadema. Sasa wako wenyewe mle. Ataanza kuwanyanyasa wa chama chake mwenyewe. Kuna taarifa kwamba tayari yameshaibuka makundi mara baada ya kutangazwa Baraza la Mawaziri na pili tamko la Jiwe kuwa hatokubali Mgombea Urais 2025 awe aliyemzidi umri.

Haya makundi yamo mle Bungeni na wataanza kusodoana mle mle ndani na Spika hataweza kuwadhibiti jambo ambalo halitamfurahisha M/Kiti wao Taifa. Hivyo kuna uwezekano mkubwa kuwapo na Watakaotimuliwa kwenye chama. Muda utaongea.
 
Ila anachoongea huyu jamaa kina ukweli fulani,wapenda mabadiriko nchini hasa vyama vya siasa wasitegemee chochote kupitia mfumo huu wa utawala au bunge hili.

Ukimwangalia ndugai usoni amekaa kinafiki nafiki sawa na maneno yake

Yaani ukiambiwa ni msomi unaeza usikubali.
Kati ya viongozi utopolo tulionao nchi hii ndugai no,1. Yaani hata jiwe ana nafuu.

Huyu spika sijui familia yake ina hali gani kitabia!!.
Mke sijui anaishi nyumbani kwake au kwa wengine

TUNA SPIKA AU TUNA MAITI?
"Ukimwangalia ndugai usoni amekaa kinafiki nafiki sawa na maneno yake

Yaani ukiambiwa ni msomi unaeza usikubali".
Ndugu nguruka wa kig0ma ,Ndugai usomi ameupata wapi,lini na kutoka wapi!?
Bungeni leo nani ni msomi pale!?
Ndugai hata shule yake ya hovyo,huo usomi atautoa wapi?
Huwezi kuwa msomi halafu ukakubali "matumizi kinyume na maumbile".
 
K
Hapo jana ya tarehe 11/12/2020 tulipata taarifa kuwa Bunge la Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo limepiga kura ya kutokuwa na imani naye Spika wao wa Bunge, Jeanine Mabunda kwa namna anavyoliendesha Bunge hilo kwa upendeleo na kujiegemeza kwa Rais Mstaafu, Joseph Kabila, pamoja na chama chake.

Nchi yetu Tanzania tunajifunza nini kuhusu kutimuliwa kwa Spika huyo wa Bunge la Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo?

Ni dhahiri kuwa yapo mengi tunayoweza kujifunza kwa Bunge hilo jinsi lilivyosimamia kanuni zake na kumwona Spika huyo wa Bunge kuwa hafai na hivyo kumpigia kura za kukosa imani naye.

Hapa nchini kwetu tunaye Spika ambaye ameamua kuikanyaga kanyaga Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977
kwa kuwakumbatia wale wabunge wa viti maalum wa Chadema.

Ni sharti la kikatiba kuwa mbunge yeyote anapovuliwa uanachama wake na chama chake, basi hatua inayofuata ni kwa Spika kuiandikia barua Tume ya uchaguzi kuieleza kuwa nafasi hizo za ubunge ziko wazi, kwa hiyo ufanyike mchakato mwingine wa kuziziba nafasi hizo.

Tumepata taarifa toka kwa kiongozi wa Chadema, John Mrema, zilizothibitisha kuwa chama hicho kilishapeleka barua kwa Spika wa Bunge, Job Ndugai, tarehe 29/11/2020 kuhusu maamuzi ya Kamati Kuu ya Chadema, kuwavua uanachama wabunge hao akina Halima Mdee.

Swali tunalopaswa kumuuliza Spika Ndugai ni kwanini anashikwa na "kigugumizi" na hataki kutekeleza sharti hilo la kikatiba kwa kumwandikia barua Mkurugenzi wa Tume, kumjulisha kuhusu kupokea kwake barua hiyo ya Chadema?

Hivi kuna tofauti gani katika uendeshaji wa Bunge kati ya Spika Ndugai na mwenzake Jeanine Mabunda wa Congo aliyetimuliwa kazi kuhusu upendrleo wake kwa Rais mstaafu Joseph Kabila na Chama chake?

Hivi Spika Ndugai ambaye anaonyesha upendeleo wa wazi kabisa kwa Rais Magufuli na chama chake cha CCM, na kuikanyaga kanyaga Katiba ya nchi yetu ni kwanini basi Bunge la nchi yetu lisipange kupiga kura ya kumng'oa kwenye nafasi hiyo ya U-Spika?
Kwani anayetaarifiwa ni Spika au ni Tume iliyowateua!?
 
Yaani CHADEMA ni wajinga no offense, unategemea Ndugai aende dhidi ya matakwa ya CCM na Mwenyekiti wake, hivi unajua hata huyo Spika wa Congo ametimuliwa sababu ya kuwa upande tofauti na Rais wa nchi yake, mna ndoto za kitoto kama vile mpo katika fantasy world.
Wewe ndiyo una utoto kwa kuja na mifano isiyoendana na uovu wa Ndungai
 
Have understood only "Fantasy"
Yaani CHADEMA ni wajinga no offense, unategemea Ndugai aende dhidi ya matakwa ya CCM na Mwenyekiti wake, hivi unajua hata huyo Spika wa Congo ametimuliwa sababu ya kuwa upande tofauti na Rais wa nchi yake, mna ndoto za kitoto kama vile mpo katika fantasy world.
 
Spika siyo kwamba anasusua kufuata kanuni sheria na miongozo...
Tatizo anaendekeza maagizo kutoja juu...




Cc: mahondaw
Kama anafuata maagizo toka juu, bila kuzingatia Katiba ya nchi, basi ajue kuwa ipo siku hayo maagizo anayoyatekeleza yatakuja mtokea puani!
 
Kama anafuata maagizo toka juu, bila kuzingatia Katiba ya nchi, basi ajue kuwa ipo siku hayo maagizo anayoyatekeleza yatakuja mtokea puani!
Ipo siku yes... Ila hiyo ipo siku kwa katiba hii hii haiwezi kufikiwa...




Cc: mahondaw
 
Back
Top Bottom