Baada ya Rais Zelaya kukaidi amri ya Jaji Mkuu kwamba asiendeleze tamaa zake za kutaka kubadili katiba ili ajiruhusu kutawala Honduras kwa mwongo mwingine, Jaji Mkuu aliamru Jeshi limkamate na kumtia adabu.
Ninajiuliza hivi Tanzania na katiba yetu hii isiyo na kifungu inayoilinda dhidi ya Rais hakuna siku jamaa anaweza kukurupuka kwa kushawishiwa na wale wanaoneemeka na kuwepo kwake madarakani akaja akatengua kipengee cha miaka 5 mara mbili na kujiongezea mingine 5 au 10? Si ndio tabia ya viongozi wengi wa Kiafrika au sio?
Kwa hiyo ninapendekeza kwamba kazi za Jeshi letu pamoja na ilizo nazo sasa iwe ni kuhakikisha kuwa kila rais ajaye madarakani hata awahonge vipi haruhusiwi kutawala kwa zaidi ya miaka 10. Hili litatuepushia madhambi, balaaa na misukosuko mingi huko mbele ya safari.
Jamaa akichemsha tu awe ANAHONDURASIWA MARA MOJA!