Tunajifunza nini kutoka Honduras?

Tunajifunza nini kutoka Honduras?

Iga

Senior Member
Joined
Dec 17, 2007
Posts
112
Reaction score
6
Baada ya Rais Zelaya kukaidi amri ya Jaji Mkuu kwamba asiendeleze tamaa zake za kutaka kubadili katiba ili ajiruhusu kutawala Honduras kwa mwongo mwingine, Jaji Mkuu aliamru Jeshi limkamate na kumtia adabu.

Ninajiuliza hivi Tanzania na katiba yetu hii isiyo na kifungu inayoilinda dhidi ya Rais hakuna siku jamaa anaweza kukurupuka kwa kushawishiwa na wale wanaoneemeka na kuwepo kwake madarakani akaja akatengua kipengee cha miaka 5 mara mbili na kujiongezea mingine 5 au 10? Si ndio tabia ya viongozi wengi wa Kiafrika au sio?

Kwa hiyo ninapendekeza kwamba kazi za Jeshi letu pamoja na ilizo nazo sasa iwe ni kuhakikisha kuwa kila rais ajaye madarakani hata awahonge vipi haruhusiwi kutawala kwa zaidi ya miaka 10. Hili litatuepushia madhambi, balaaa na misukosuko mingi huko mbele ya safari.

Jamaa akichemsha tu awe ANAHONDURASIWA MARA MOJA!
 
History is full of lessons of dos and donts. But it is hard to grasp all the lessons. Hata hili nalo ni funzo kubwa
 
Wahonduras wanatufundisha kwamba katiba ya nchi ambayo ndio sheria mama iheshimiwe na kila mtu. yeyote atakayejaribu kuichezea kwa maslahi binafsi ashughulikiwe kikamilifu
 
Can't imagine TZ Jaji anaamurisha Rais akamatwe. Hii sheria inafaa iigwe TZ may be itapunguza nguvu na purukushani za viongozi wetu.

Natumaini ni funzo zuri kwa CCM na viongozi wake, na African politics kwa ujumla especially Bob!!!!!!!!!!!!!!!
 
Tanzanians need to grow up. Kila kitu kikitokea nje tujifunze nini? Hilo swali litakwisha lini? Do something or shut up.
 
Back
Top Bottom