TUNAJIFUNZA NINI KUTOKA KWA MISRI

TUNAJIFUNZA NINI KUTOKA KWA MISRI

Aaron Arsenal

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2014
Posts
24,501
Reaction score
28,711
Misri wenyeji wa mashindayo ya AFCON mwaka huu na finalist wa AFCON2017 wamefurushwa kwenye nzunguko wa pili. Kocha mkuu wa timu hiyo Javier Agguire amesema wachezaji wa timu hiyo wasitupiwe lawama, kwani tatizo halikua kwao bali kwake. Amekubali kutupiwa lawama zote yeye.

Baada tu ya kutamka hivyo Rais wa chama cha soka cha Misri, Abou Rida akamfurusha kocha huyo. Kisha nae akasimama na kusema furushi la lawama halipaswi kubebwa na kocha Agguire peke yake. Bali hata yeye kama Rais wa EFA hakuwajibika ipasavyo kuhakikisha timu inashinda. Akaomba radhi na kujiuzulu.

Dakika chache baadae wajumbe wa kamati ya maandalizi ya timu hiyo kwenda AFCON nao wakajiuzulu. Wanasema furushi la lawama halipaswi kubebwa na kocha na Rais wa EFA peke yao. Na wao wanahusika. Wakaomba radhi na kung'atuka.

Hii ndio maana halisi ya uwajibikaji. Kila mtu katika nafasi yake anajihisi kuwa responsible bila kutafuta kisingizio. Na ndio maana wenzetu wanapiga hatua kubwa katika soka.

Hapa kwetu hali ni tofauti kabisa. Tumefurushwa AFCON kwa aibu kabisa na kuweka rekodi ya timu iliyofungwa magoli mengi zaidi kwenye michuano ya AFCON mwaka huu. Lakini hakuna anayetaka kuwajibika. Kila mtu anatafuta kichaka cha kujificha.

Amunike anasema tatizo sio lake ila ugeni wa mashindano. Anasahau kwamba Madagascar ni wageni kuliko sisi. Sisi tumeshiriki mara mbili. Madagascsr mara moja lakini wameongoza kundi lao na kuingia raundi ya pili. Madagascar haohao wageni kuliko sisi waliitandika timu kubwa kama Nigeria bila huruma. Sisi tunajificha kwenye kichaka cha ugeni.

Bashite anatupa lawama kwa Spika Ndugai na wabunge walioenda Misri. Bunge linasema tatizo ni Bashite. Bashite anasema tatizo ni Piere Liquid. Piere anasema Taifa Stars itabaki kuwa juu, itabaki kileleni. Ama kweli aliyetuloga alikufa na matunguli yake.!

kutoka kwa MALISA GJ
 
Tanzania hatuko serious na Mambo tuyafanyayo.

Kila kitu tunachukulia simple ndo maana hatufiki popote kimataifa
 
Back
Top Bottom