Tunajifunza nini kwa kijana Benjamin

Tunajifunza nini kwa kijana Benjamin

BilioneaPATIGOO

JF-Expert Member
Joined
Jun 23, 2012
Posts
12,320
Reaction score
11,327
Nimebahatika niseme hivyo kuangalia na kusikiliza interview aliyofanya Benjamin na Millard Ayo...nimesikia aibu sana..na laiti ningekua rais wa nchi hii sidhani kama ingepita siku mbili sijamuita huyu kijana aje anipe mawazo mapya ya kuwakwamua vijana zaidi ya laki kadhaa kama si milioni wasio na ajira na zaidi kuwalegezea masharti ya kufanya biashara ama kuendeleza idea zao za kuisaidia jamii inayowazunguka..

Kijana Benjamin anaipenda nchi yake ila sidhani kama anapewa ushirikiano wa kutosha ...just imagine anakaa na matajiri wa huko nje kwenye darasa moja maskin ya Mungu kila akikutana nao kitu cha kwanza ni neno "Tanzania" lakin majibu anayopewa inasadiki yanayoendelea nchini...na alijarib kujibu kitalaamu lakin ukweli ni kwamba wanaogopa kuja kuwekeza sababu ya mambo yanayoendelea kisiasa na kiuchumi..Sheria za kibiashara na kodi zinambana hata Yule kijana anayeanza biashara (start ups) ..

Benjamin anasema kuanzisha kampuni marekani haichukui zaidi ya dakika 30...je kwa hapa kwetu? (Msinijibu)
Ni Hali ya kushangaza sana ....Ghana tunaambiwa hivi sasa kwa wale wanaoanza biashara kuanza kulipa kodi ni after 7 years...je hapa kwetu (msinijibu)

Sasa wakati ule amekutana na Bill Gates akamwambia njoo uje ufanye kazi kwenye kampuni yangu ntakulipa milioni 400+ ... Benjamin kwa kujua anacho Fanya na kwa kujua he can make more that that money kiustaarabu akakataa (na bado naamin ana Namba ya simu ya Bill Gates and they still talk) tena akatolea mfano wa founders wa WhatsApp kwamba how rich they are now ..watu wakamuona mshamba wa mwisho kabisa hopeless..right now hadi sasa tangu ameanzisha app yake ambayo si lazima uwe na bundle kuitumia, amepata tuzo zaidi ya saba ..na ashaitwa na kampuni kubwa duniani aipeleke kwenye nchi zao ila maskin ya Mungu kakataa anasema anataka kwanza hapa kwetu ..unajiuliza hivi hapa kwetu mtu kama huyu anapata recognition gani kwa government?

Anamalizia kwa kusema ni imani yake kwamba kupitia yeye kuna mwingine atakuja na wengi watakuja kabadilisha jamii inayowazunguka ila kwa kuwekewa mazingira rafiki yasiyo ya kisiasa wala kichama ya kukamilisha ndoto hizo (kufanya biashara)
 
Ukisema tu BENJAMIN unakuwa hueleweki mauelezee kwa kumtaja kwa jina kamili BENJAMIN FERNANDES.
Anyway jamaa yupo Smart sana kichwani..nilipata mjua nilipokuwa Agape Television 2015/ (TING)
 
Tumejifunza kwamba tutafute pesa ili watoto wetu wasiteseke baadae, jamaa ana background nzuri kutoka kwa wazazi wake na ninahakika wanamsapoti.
 
Back
Top Bottom