The Father of All
JF-Expert Member
- Feb 26, 2012
- 11,099
- 13,709
Sina shaka na hili. Tanzania tuna tatizo. Tunafanya uchaguzi bila upinzani. Vyama CCM B vimewekwa baada ya kuhongwa ili kuhalalisha uongo.
Ni uchaguzi gani halali wa huru na haki bila Lissu? Ni uchaguzi gani ambapo hata baadhi ya wagombea walijiteua na kukataa hata taratibu za ndani ya chama chao? Ni uchaguzi gani huru ambapo kampeni zimejaa vitisho, rushwa, na kila aina ya uvunjaji amani?
Ni uchaguzi gani waweza kuwa uchaguzi wakati watu wanatekwa, kuuawa na kupotezwa huku viongozi wakiendelea na business as usual kana kwamba wahanga hawalindwi kikatiba? Je, kazi ya viongozi ni nini kama siyo kuhakikisha usalama wa raia na mali zao?
Je, wanamuongoza nani wakati hata nao wanahitaji kuongozwa? Tuache unafiki. Tuna mengi ya kujifunza toka Malawi juu ya namna ya kufanya uchaguzi huru na wa haki. Tunajifunza toka Madagascar kuwa wenye nchi wakiitaka hakuna wa kuwazuia.
Tunajifunza kuwa majeshi ya kweli ya wananchi husimama na wananchi na kupinga uovu. Ninapoandika, Kameruni kishaanza kuumana. Juzi, waliandamana na kuchoma majengo ya serikali na ya chama tawala wakimkataa Paul Biya, king'anganizi aliyehujumu nchi ile kwa zaidi ya miaka arobaini ukiachia mbali kuwa hana hata uwezo wa kujikuna wala kujua alipo.
Je, kama jamii, taifa, na watu, tena tunaodai tuna akili timamu, tunajifunza nini?