GUSSIE
JF-Expert Member
- Dec 2, 2014
- 3,880
- 11,134
Wanabodi, katika siku tatu hizi mfululizo kuna mambo mengi ya kisheria tumejifunza kama wana.
Ingawa Tundu Lissu anaweka mitego ili tujiingize kichwa kichwa halafu ije tuonekane ni nchi isiyofuata haki na demokrasia hivyo kutengwa.
Mosi, Kuandaa wanasheria bora wenye kusoma na kuelewa mambo kwa mapana kuanzia sheria zetu wenyewe za chama cha mapinduzi na za uchaguzi.
Mfano, Suala la Tume ya uchaguzi kumuita Tundu Lissu kwenye Tume ya maadili kupitia vyombo vya habari amelipangua vibaya mno kuwa lazima aitwe kwa maandishi na barua lazima apewe yeye, baadae Tume imebadili kauli kuwa watamtumia barua.
Pili, Suala la IGP Siro kumuita Polisi, Lissu ameeleza lazima aambiwe sababu na amevunja sheria ipi? Suala hili linaungwa mkono na maelfu ya wanasheria kwenye mitandao ya kijamii.
Ushauri kwa chama changu ni huu.
Mosi, Jeshi la polisi lisijiingize kwenye ishu za uchaguzi huu, Maelezo yote ya kumuita Tundu lissu Polisi yana tuma ujumbe kwa mataifa mengine na wananchi kuwa CCM tunabebwa na Polisi na Tume wakati kuna mikoa mingi ni ngome zetu wana CCM.
Pili, hata wanaCCM wameongea kauli tata juu ya lissu mfano anatumiwa na mabeberu, Mara Msukule lakini yeye akirusha mishale kwetu inauma sana tujifunze uvumilivu,Siasa ni utani na madongo kwa wagombea, kuna madongo yanauma na mengine yanafurahisha.
Wakati wa uchaguzi ndio wakati wa majungu na fitina na kuna watu wamezaliwa kufanya fitina na majungu ya kweli na uwongo
Mfano: Nape Nnauye alikuwa mtu wa majungu na fitina sana, Hivyo kila kauli kutoka kwa Dkt Slaa alijibu kwa majungu na fitina za kuuma na kupuliza.
Mwigulu Nchemba wa wakati huo alikuwa mtu wa kupika propaganda za uwongo na za kweli kuaminisha Chadema haifai.
Kuna mifano mingi sana hata Jakaya Kikwete alikuwa mtu wa kupiga mipasho fulani hivi ya Pwani, JK anakusema unaumia huku anacheka kwa kiswahili cha Pwani bila kutaja jina.
Tusiumie na Lissu yeye anatwanga live bila tafsida au kuchuja tumvumilie tu ndio uchaguzi huo.
Yote kwa yote somo la sheria hata sisi tusio wanasheria kuna kitu tunajifunza kwake mnyonge mnyongeni lakini kwenye ishu ya sheria jamaa ni mtaalamu na anasoma.
Kwa ufupi Tundu Lissu sio mvivu kusoma sheria zetu na historia yetu.
CCM tutashinda kwa mbinu za kisasa zaidi na zilizoboreshwa za kushawishi na kuonyesha yale tuliyoyafanya.