Tunajua namna ya kupata matokeo dhidi ya Simba - Cheche

PROSPER 05

JF-Expert Member
Joined
Oct 14, 2013
Posts
226
Reaction score
217
KUELEKEA fainali ya michuano ya Kombe la Mapinduzi keshokutwa Ijumaa, Kocha Msaidizi wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, Idd Nassor Cheche, ameweka wazi kuwa wanajua namna ya kuikabili Simba na kupata matokeo mazuri kwenye mchezo huo.

Cheche ametoa kauli hiyo kwenye mazoezi ya kwanza ya Azam FC jioni ya kujiandaa na mchezo huo, ambapo imeingia fainali baada ya kuichapa Taifa Jang’ombe bao 1-0, lililofungwa kwa shuti kali na kiungo Frank Domayo.

“Mchezo utakuwa mgumu, sisi tumewaona tokea mwanzo kwenye michuano hii na tunawajua tokea huko nyuma na mwalimu waliokuwa naye na sisi tulikuwa naye tunamjua na tunajua ni vitu gani tutafanya, hatuwezi kusema hivi sasa utakuja kuviona uwanjani wakati tunacheza kama tulivyowaahidia kwenye mechi na Yanga,” alisema Cheche wakati akizungumza na mtandao rasmi wa klabu www.azamfc.co.tz ... mwisho wa kunukuu
.........................................................................................................................

Nauona kwa Mbali Uzinduzi Mwingine wa Mtandao wa Kasi kwa Mnyama kwani Chama Langu la AZAM Ambao ni Mabingwa wa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA Kagame Cup) na Ngao ya Jamii, wametinga fainali ya michuano hiyo wakiwa na rekodi ya aina yake kwani ndio timu pekee ambayo haijafungwa bao lolote mpaka sasa ndani ya mechi nne ilizocheza ikiwa imefunga mabao sita.
 
Huyu Cheche amekuaje siku hizi.. mbona huko nyuma hakua hivi? Baada ya kuwafunga Ndala naona kila siku yupo magazetini.. Kosa kubwa analolifanya ni kumfananisha Simba na Ndala. Hii itamgharimu.. Mnyama hatabiliki hata kidogo.. kwa maelezo zaidi amuulize Lwandamina.

NB; Cheche kuongea sana hakuwezi kukupa nafasi ya Ukocha Mkuu.. na uwe makini sana lasivyo kwa kipigo kizito tunachoenda kuwashushia leo.. hata hiyo nafasi ya ukocha msaidizi uliyopewa unaweza nyang'anywa.
 
Sisi tunasubiri mtu na binamu yake waucheze huo mpira.

Maneno mengi ya nini wakati dakika 90 zitaleta majibu?
Japo siku zote unaitia ugumu nira yako.. naamini leo utailainisha na kua upande wa mnyama ili uweze kupata burudani.. kitu ambacho kwa ndala ni nadra.
 
Japo siku zote unaitia ugumu nira yako.. naamini leo utailainisha na kua upande wa mnyama ili uweze kupata burudani.. kitu ambacho kwa ndala ni nadra.

Nipo njia panda Mkuu.

Katika hali ya kawaida ningependa mnyama alale mapema lakini vimatusi vya lambalamba juzi baada ya kubahatisha goli zake nne, vimeniacha hoi.

Yote kwa yote, bora Lambalamba ashinde leo maana kelele zake hazikawii kuisha. Fikiria "hotuba" ya Haji Manara mnyama akishinda !
 
Hahaha.. Mkuu kama unataka kujiongezea maumivu mshabikie lambalamba.. ila kama unataka furaha japo ya dk 90 kua upande wa mnyama
 
Hahaha.. Mkuu kama unataka kujiongezea maumivu mshabikie lambalamba.. ila kama unataka furaha japo ya dk 90 kua upande wa mnyama

Kumshabikia mnyama haiwezekana hata siku moja. Ngumu kumesa!
 
Ni Zamu ya Simba Leo Kuiita MApinduzi Cup "BONANZA"🙄🙄
 
Japo siku zote unaitia ugumu nira yako.. naamini leo utailainisha na kua upande wa mnyama ili uweze kupata burudani.. kitu ambacho kwa ndala ni nadra.
Mtani kwema ? sisi tunasubiri nani maneno yake yapo sahihi
 
Azam yupo kwajili ya kuwashikisha adabu watani wa Jadi ktk kombe hili, alianza na yanga na xx mnyama anarambishwa nae konii
 
Hahaha.. Mkuu kama unataka kujiongezea maumivu mshabikie lambalamba.. ila kama unataka furaha japo ya dk 90 kua upande wa mnyama
Niliandika baada ya dakika 90 tutajua kama ni iddi nassoro cheche beki wa zamani wa swaaleti (sigara )iliyokuwa imesheheni vipaji kama Joseph katuba, aziz nyoni njalambaya, kasongo athumani ,Peter lucas, mohomed khalfan kiumbe maarufu yasini,ladislaus shawa,mascut said aah kwanza nimejisumbua kuandika sembo atakuwa eneo korofi muda huu ila haidhuru akirudi atakutana nayo .
 
Ujue mikia ndio mmeisha jimaliza hapo hamta nyanyua kwepa mwaka huu kombe lenu ndio lilikuwa hilo mjue !
 
Watu tumelala vizuri kitaani utulivu...Santee azam
 
Ndugu zanguni hii kazi yenu nia yenu ni kunitafuta ubaya yaani kweli kwa haya yaliyo tokea jana khalafu leo mnanipa kazi ya kumtafuta sembo kwa kweli kama ni makusudi hapa mmeniweza na kazi yenu imenishinda na posho yenu narudisha.
 
Haha.. Sawa Mkuu nimekutana nayo.
 
Haha.. Sawa Mkuu nimekutana nayo.
Duh ! hatimae umejitokeza Shukran mtani maana mengi yametokea na namna ulivyo mnanga iddi nassoro cheche kitu ambacho hukujua cheche aliongea kama kocha na sembo aliongea kama kocha wa mikia humu jf
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…