PROSPER 05
JF-Expert Member
- Oct 14, 2013
- 226
- 217
KUELEKEA fainali ya michuano ya Kombe la Mapinduzi keshokutwa Ijumaa, Kocha Msaidizi wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, Idd Nassor Cheche, ameweka wazi kuwa wanajua namna ya kuikabili Simba na kupata matokeo mazuri kwenye mchezo huo.
Cheche ametoa kauli hiyo kwenye mazoezi ya kwanza ya Azam FC jioni ya kujiandaa na mchezo huo, ambapo imeingia fainali baada ya kuichapa Taifa Jang’ombe bao 1-0, lililofungwa kwa shuti kali na kiungo Frank Domayo.
“Mchezo utakuwa mgumu, sisi tumewaona tokea mwanzo kwenye michuano hii na tunawajua tokea huko nyuma na mwalimu waliokuwa naye na sisi tulikuwa naye tunamjua na tunajua ni vitu gani tutafanya, hatuwezi kusema hivi sasa utakuja kuviona uwanjani wakati tunacheza kama tulivyowaahidia kwenye mechi na Yanga,” alisema Cheche wakati akizungumza na mtandao rasmi wa klabu www.azamfc.co.tz ... mwisho wa kunukuu
.........................................................................................................................
Nauona kwa Mbali Uzinduzi Mwingine wa Mtandao wa Kasi kwa Mnyama kwani Chama Langu la AZAM Ambao ni Mabingwa wa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA Kagame Cup) na Ngao ya Jamii, wametinga fainali ya michuano hiyo wakiwa na rekodi ya aina yake kwani ndio timu pekee ambayo haijafungwa bao lolote mpaka sasa ndani ya mechi nne ilizocheza ikiwa imefunga mabao sita.