Tunakoelekea kuoga na Sabuni Pia tutaambiwa ni dhambi

Tunakoelekea kuoga na Sabuni Pia tutaambiwa ni dhambi

Bi zandile

JF-Expert Member
Joined
Sep 12, 2024
Posts
301
Reaction score
856
Baada ya Mchungaji Mch. Abiud Misholi Kutamka adharani kwamba ni Ushetani mkubwa Mlokole kushabikia mpira Mwimbaji wa nyimbo za injili na SHABIKI mkubwa wa Yanga African @Ann_annie kafunguka ya moyoni na kusema....

"Kuna Max Nzengeli na Kennedy Musonda wameokoka sasa na wanacheza mpira itakuwaje??

Mabasi yenyewe tunayopanda ni ya washirikina biashara nyingi tunakoenda kununua vitu wawekezaji ni hao hao washirikina, sadaka tunazotuma kwa wachungaji tumezipata kwa hao hao washirikina na cha ajabu wachungaji hawazikatai hizo sadaka ... Niseme tu ni Yesu tu anayetulinda".

Hivi ndivyo alivyofunguka mwimbaji wa gospel, nimemuelewa vizuri kabisa, ila mchungaji Misholi sijamuelewa kabisa.

Bila shaka tunakoelekea, hata kuoga na sabuni ya GSM tutakuja kuambiwa ni dhambi 🤔
 
Attachments

  • 1727939473700.jpg
    1727939473700.jpg
    207.6 KB · Views: 2
Hawa walokole au wanaojiita walokole wamepungukiwa akili, huwezi ukaokoka kabla haujafa.

Unakufa kwanza, unahukumiwa kwa kadiri ya matendo yako, ukipenya kwenda mbinguni hapo sasa ndiyo unakua umeokoka.

Naomba muwaambie wafanye matumizi mazuri ya hizo akili finyu, kama bado zipo

Andiko la nini hapo ni matumizi ya akili, unafikiri kila kitu utaandikiwa kwenye scriptures?

Sasa Mungu alikupa akili za kazi gani? kuvukia barabara na kwendea chooni?
Mk 16:16
Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa.

Unalionaje hilo andiko, lipo sawa na hoja yako?
 
Huyo Mchungaji Misholi yupo sahihi kabisa na kasema ukweli shida inakuwa ni kwa wapokeaji na ambao kilichosemwa kinawagusa lazima watafute kichaka cha kujifichia huyo aliyempinga kwa hoja dhaifu mkumbushe njia ya kwenda uzimani ni nyembamba sana na waipitao ni wachache kwa maana ya kwamba hiyo njia ina kujikana nafsi sana kwa kutoyapenda ya ulimwengu na kufuata amri, sheria na maagizo ya Mungu tu

Kinyume na hapo wewe hamia njia ya upotevuni huko wapo wengi ambao hawa hufanya wapendayo wao tu hawana amri sheria nk
 
Mk 16:16
Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa.

Unalionaje hilo andiko, lipo sawa na hoja yako?
Sikiliza ndugu, unaposoma Biblia hausomi andiko au mstari peke yake yaani independent or in isolation with the rest of the texts.

Msingi mzima wa maandiko yote ni tuishi hapa duniani na mwisho wa maisha yetu tutahukumiwa, yaani siku ya kiama na parapanda itapigwa na tutahukumiwa kwa kadiri ya matendo yetu. Hili jambo Yesu mwenyewe ameliongelea mara nyingi na liko wazi

Kama una amini kwenye hukumu ya mwisho, sasa dhana ya kuokoka ukiwa hai inatoka wapi? Kama utaenda kuhukumiwa kwa kadiri ya matendo yako mwisho wa maisha yako, unawezaje kusema umeokoka.

UMEOKOKA NA NINI KAMA UTAENDA KUHUKUMIWA NA PENGINE UKAKUTWA NA HATIA UKATUPWA MOTONI

Embu tumieni akili zenu vizuri
 
Hawa walokole au wanaojiita walokole wamepungukiwa akili, huwezi ukaokoka kabla haujafa.

Unakufa kwanza, unahukumiwa kwa kadiri ya matendo yako, ukipenya kwenda mbinguni hapo sasa ndiyo unakua umeokoka.

Naomba muwaambie wafanye matumizi mazuri ya hizo akili finyu, kama bado zipo
Waliteswa, wakafa, wakazikwa kisha wakafufuka pamoja na Kristo katika mauti yake.

Leo hii wako ndani ya Kristo. Na Kristo ameketi mbinguni kwa Mungu baba.
Maana yake wao wapo Mbinguni ndani ya Kristo, ndio maana ya Kuokolewa na Kristo.
 
Waliteswa, wakafa, wakazikwa kisha wakafufuka pamoja na Kristo katika mauti yake.

Leo hii wako ndani ya Kristo. Na Kristo ameketi mbinguni kwa Mungu baba.
Maana yake wao wapo Mbinguni pia ndani ya Kristo, ndio maana ya Kuokolewa na Kristo.
 
Huyo Mchungaji Misholi yupo sahihi kabisa na kasema ukweli shida inakuwa ni kwa wapokeaji
Kama yupo sahihi kwa nini hajawahi kukataa sadaka iliyotumwa kupitia ule mtandao wa washenzi Tigopesa or M-Pesa?

Wachungaji wapo speed kusambaza in public namba za kutuma sadaka ilhali watumaji ni hao hao mashrtani, upo wapi usahihi wa mchungaji?
 
Kama yupo sahihi kwa nini hajawahi kukataa sadaka iliyotumwa kupitia ule mtandao wa washenzi Tigopesa or M-Pesa?

Wachungaji wapo speed kusambaza in public namba za kutuma sadaka ilhali watumaji ni hao hao mashrtani, upo wapi usahihi wa Mchungaji
Kama yupo sahihi kwa nini hajawahi kukataa sadaka iliyotumwa kupitia ule mtandao wa washenzi Tigopesa or M-Pesa?

Wachungaji wapo speed kusambaza in public namba za kutuma sadaka ilhali watumaji ni hao hao mashrtani, upo wapi usahihi wa mchungaji?

Kwa hiyo arembe dhambi for the sake of offering hutaki kuambiwa ukweli baki kwako na sadaka yako hampendi kuambiwa dhambi ndiyo maana wanaibuka wachungaji wa comedy wa kuwafurahisha ili wawasindike motoni
 
Back
Top Bottom