Tunakoelekea kuoga na Sabuni Pia tutaambiwa ni dhambi

Mungu baba,Mwana,Roho mtakatifu
 
nzengeli ni msabato, kwa habari ya wakatoliki, ni kweli hawaokoki, maria haokoi.
Yesu Anakuja na Wengine: Maria haokoi...

Wakatoliki:...
Nasadiki kwa Bwana mmoja Yesu Kristo, mwana wa pekee wa Mungu.
Aliyezaliwa kwa Baba tangu milele yote.
Mungu aliyetoka kwa Mungu,mwanga kwa mwanga,Mungu kweli kwa Mungu kweli.
Aliyezaliwa bila kuumbwa, mwenye umungu mmoja na Baba,
ambaye vitu vyote vimeumbwa naye.
Ameshuka toka mbinguni kwa ajili yetu sisi wanadamu na kwa ajili ya wokovu wetu.
 
Soma pia Yohana 14:26
 
Kama kuna Roho mtakatifu/Kristo mwingine unamsubiri unamaanisha lipi? Je hakuna Kristo ndani yako leo?

Huyo unayemsubiri akija, yuke uliyenaye siku zote ataenda wapi, ama aliyepo ni feki.
Roho mtakatifu ndiye kiongozi kwa Sasa,huyo Roho mtakatifu huyaabadilisha maisha,ndiyo maana unakuta dhamiri ya usitende baya linakujia ni kazi ya Roho mkuu!
 
kwa maoni yangu na matazamo wangu juu ya hili, kwanza lazima tukubaliane kuwa mpira wenyewe na asili yake haumpi Mungu utukufu, na maandiko yanasema fanyeni kila jambo kwa utukufu wa Mungu. Sasa kwenye huo mpira kuna ushirikina mkubwa wanaajiliwa waganga na mambo mengi ya kishirikina yanafanyika hayo hayampi Mungu utukufu

Pili mpira umejaa mambo ya kufuru, ufusika, pombe, lugha za matusi utazikuta uwanjani hayo hayampi Mungu utukufu

Sasa kama Mwana wa Mungu anapaswa kufanya mambo yanayompa Mungu utukufu akifanya hilo ambalo unaona kabisa kuna wengine walimiminiana risasi huko Russia, watu wana apa mpaka kuwatoa sadaka wake zao(kubet) sio sahihi.

Ukisimamia hoja ya wachungaji kupokea sadaka, wao wachungaji wanapokea tu lakini huwatolei wachungaji, ndio maana utatoa sadaka kwa wachungaji lakini utamuomba Mungu akubariki, maana yake hata sadaka zinamhusisha Mungu
 
Ukiwa mabanda ya mipira ndio utajua ushabiki wa mpira ni mpango wa shetani mabanda ya mipira yametawaliwa na lugha zilizokosa staha kitu kingine ushabiki wa mipira umeliingiza kundi kubwa la watu kuingia kwenye michezo ya kamari ushabiki wa mipira ni mpango wa shetani kuwa mshabiki wa timu Fulani unakuwa umeniunga katika ibada zao huko wanakotoaga makafara kabla ya msimu haujaanza
 
Kuna hasara nyingi unapata unapokunywa pombe kuliko faida, correction hakuna faida, kwann unachagua hasara?
Kwenye unywaji wa pombe andiko la Petro limejibu vyema kuwa pombe nyingi humuathiri mtu hivyo pombe ni kitu Cha tahadhari sio haramu
 
Mpira ni ibada na vilabu Ni madhehebu ambapo mtu akipenda kilabu Hicho hawezi hama.
Mfano umeamua kuwa Shetani Mwekundu bhasi milele wewe ni Shetani😁
Ahaa basi ngoja jioni nikaangalie YANGA kwa umakini,..nikimuona SHETANI naacha
kuiangalia🤣🤣
 
Hapa umedanganya.
 
Kama yupo sahihi kwa nini hajawahi kukataa sadaka iliyotumwa kupitia ule mtandao wa washenzi Tigopesa or M-Pesa?

Wachungaji wapo speed kusambaza in public namba za kutuma sadaka ilhali watumaji ni hao hao mashrtani, upo wapi usahihi wa mchungaji?
Sijui unabisha nini na hoja yako ni ipi? Maana naona unatoka kwenye mpira na sasa unaenda kwenye sadaka via Mpesa na Tigo pesa.
 
Mpira ni ibada na vilabu Ni madhehebu ambapo mtu akipenda kilabu Hicho hawezi hama.
Mfano umeamua kuwa Shetani Mwekundu bhasi milele wewe ni Shetani😁
Ni sahihi. Nakumbuka wakati nikiwa shabiki damudamu wa Chelsea na maono niliyoyaona ya lile Simba lililoshika mkuki kwenye logo ya Chelsea kama linatema moto hivi na uhalisia wake katika ulimwengu wa Roho.

Kwa jinsi ya kibinadamu ni ngumu kukubali ila ni kweli mpira ni chukizo. Hivi ushawahinjiuliza manembo na a.k.a ya majina yanamaanisha nini?

Timu inajiita red devil, dragon, blue satan n.k
 
Kristo atakuja mara ya pili kulichukua kanisa
 
Kama kuna Roho mtakatifu/Kristo mwingine unamsubiri unamaanisha lipi? Je hakuna Kristo ndani yako leo?

Huyo unayemsubiri akija, yuke uliyenaye siku zote ataenda wapi, ama aliyepo ni feki.
Ataondoka na huo ndio unyakuo wa kwanza, wawili watakuwa wamelala mmoja atwaliwa mmoja aachwa, wawili watakuwa shambani, mmoja atwaliwa mmoja aachwa
 
Mpira ni ushetani,

Man UTD Inaitwa timu ya Mashetani wekundu na nembo na picha za mashetani wameweka kabisa.

Chelsea ni timu ya Mashetani wa Bluu, na nembo na picha za mashetani wa Bluu zipo,

Sasa imeandikwa meditate the world of God day and night,

Sasa mlokole ulevi wake ameruhusiwa kulewa Kwa Roho MTAKATIFU, huo ulevi wa pombe au mpira wa nini?

Utakatifu ni kujiweka wakfu, kuwa special Kwa ajili ya kumtumikia Mungu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…