Tunakosea wapi?

Tunakosea wapi?

Wekeza kwenye maadili ili kukwepa hao watoto mateja na machangudoa. Hao wazazi hawakuwa na elimu hii iliyopo kwenye mfumo rasmi,lakini walikuwa na elimu ya mazingira na maadili pia.
 
Wekeza kwenye maadili ili kukwepa hao watoto mateja na machangudoa. Hao wazazi hawakuwa na elimu hii iliyopo kwenye mfumo rasmi,lakini walikuwa na elimu ya mazingira na maadili pia.

Unamaana wazazi wa sasa hawana elimu ya mazingira na maadili?? Na je hili linaweza kuwa solution kwa kizazi chetu mkuu??

Cc Kingsmann
 
Afrika ilikua na tamaduni zake, tamaduni zilizotokana na fikra na maisha halisi ya mwafrika.

Elimu ya mzungu ikamfanya mwafrika kuidharau misingi ambayo kwayo afrika ilitengezwa, na kuona tamaduni ya mzungu ni bora zaidi.

Kudharau utamaduni wako ni sawa na kudharau fikra na maisha yako kwa ujumla, na huu ndio ugonjwa unaoisumbua afrika katika karne hii. (Mwafrika anajidharau na kuamini mzungu ndio mwelevu).

Tamaduni ndio inabeba maisha ya jamii nzima, kama jamii ya leo bado haijielewi utamaduni wake ni upi, lazima kizazi kiwe cha ajabu ajabu paka pale mwafrika atakapo acha kudharau fikra zake na kuunda utamaduni unaomfaa mwafrika.

Utamaduni imara uleta uchumi imara, siasa imara, na jamii inayojielewa. Kua na tamaduni za kuigilizia lazima mambo yote yawe magumashi.
 
Unamaana wazazi wa sasa hawana elimu ya mazingira na maadili?? Na je hili linaweza kuwa solution kwa kizazi chetu mkuu??

Cc Kingsmann
Pamoja na elimu uliyonayo simamia maadili kwa familia yako. Na ili uweze kusimamia maadili inakupasa uwe muadilifu wewe mwenyewe kwanza. Uwe na maadili mazuri wewe mzazi kabla haujamsimamia mwanao. Kama hautaki mwanao anyoe kiduku isiwe wewe mwenyewe unapiga viduku na kuvaa mlgezo (mfano).
 
Wakina Nyunyaa(Junior) wanadekezwa sana,malezi ya kimamtoni yanaharibu watoto,mtoto anachezea Tablet bado yuko kindergaten,akifika form one atakuwa na page Pornhub,au Badoo
 
Fake and fragile life ndo inawaua watoto wa kizazi hiki.

Ninaposema fake and fragile life namaanisha kila nyanja, mifumo mbalimbali ya maisha nk.

Mfano mdogo tuu, form four wa sasa wanaingia na calculator kwenye mitihani yao ya NECTA. Huyu mtoto utakuja kumlinganisha na mzazi wake ambaye calculator alikutana nayo chuo kweli?

Watoto wanazoea vitonga kuanzia nyumbani mpk nje, then tusitegemee wawe na high quality kama wazazi wao.

Cc Unforgetable
 
Pamoja na elimu uliyonayo simamia maadili kwa familia yako. Na ili uweze kusimamia maadili inakupasa uwe muadilifu wewe mwenyewe kwanza. Uwe na maadili mazuri wewe mzazi kabla haujamsimamia mwanao. Kama hautaki mwanao anyoe kiduku isiwe wewe mwenyewe unapiga viduku na kuvaa mlgezo (mfano).

Nimekwelewa mkuu

Cc Kingsmann
 
Back
Top Bottom