Tunakosea wapi?

Tunakosea wapi?

Afrika ilikua na tamaduni zake, tamaduni zilizotokana na fikra na maisha halisi ya mwafrika.

Elimu ya mzungu ikamfanya mwafrika kuidharau misingi ambayo kwayo afrika ilitengezwa, na kuona tamaduni ya mzungu ni bora zaidi.

Kudharau utamaduni wako ni sawa na kudharau fikra na maisha yako kwa ujumla, na huu ndio ugonjwa unaoisumbua afrika katika karne hii. (Mwafrika anajidharau na kuamini mzungu ndio mwelevu).

Tamaduni ndio inabeba maisha ya jamii nzima, kama jamii ya leo bado haijielewi utamaduni wake ni upi, lazima kizazi kiwe cha ajabu ajabu paka pale mwafrika atakapo acha kudharau fikra zake na kuunda utamaduni unaomfaa mwafrika.

Utamaduni imara uleta uchumi imara, siasa imara, na jamii inayojielewa. Kua na tamaduni za kuigilizia lazima mambo yote yawe magumashi.

Asante kwa mchango wako

Cc Kingsmann
 
Nadhani mkanganyiko unatokea sababu malezi uliopewa na wazazi wako ni ngumu kuyaapply kwa watoto wako sababu ya utandawazi



Cc Kingsmann
Utandawazi una madhara makubwa zaidi kwa watu wasiojielewa, Wazungu hawajaathirika sana na tamaduni za kiafrika wanatuona kama jana yao. Sababu tunajitaidi kua kama wao, na sio kuendeleza tulichonacho.
 
Back
Top Bottom