Tunakufa Kwa ajali Sometimes sababu Ya usalama Mdogo wa Magari yetu

Tunakufa Kwa ajali Sometimes sababu Ya usalama Mdogo wa Magari yetu

Umiliki wa magari kwa sasa ni hitaji Muhimu sana kwa maisha yetu.

Na ni ndoto ya kila mtu kuwa na gari kwa sasa, kijana wa kiume na wa kike ukimuuliza katika "To do Goal" yake Kununua gari ni moja ya Lengo lake.

Soko la magari mengi yanayoingia nchini ni kutoka Japan na ni gari zetu hizi za toyota, na ndio kiukweli tunazimudu kulingana na hali zetu...Sasa kuna haja hawa watu wakashauriwa huko Kwenye manufacturing industries angalau pamoja na yote Wazingatie usalama wa mtumiaji.

Gari ukipalamia mpapai Bampa nyang'anyang'a na wewe ni wa kulazwa...hapo usiombe ukagonga punda au ng'ombe basi ni kifo. Gari zetu nyingi ukishafika 80Kph uko kwenye hatari ya kufa endapo itatokea ajali ya ghafla..wajapan walichoweka ni Airbags tu, lakini umezungukwa na ma plastic tupu ambayo hayakupi usalama wowote.


Na huenda wakaendelea kutuletea mabox zaidi kwa bei nafuu miaka ijayo sababu ndiyo tunayataka. NAWASILISHA.
Mkuu kwa usalama zaidi kuna vifaru urusi unaweza kuagiza tu ukaendesha ili usife kwa ajali. Kama gari lazma iwekwe material laini yasiokuumiza wakati wa impact. Yani gari iharibike ila utoke salama ndio dhumuni la airbags na body laini.
 
Ni uongo ama ukweli mkuu? Maana uzi huu sio wa kuponda magari yajapani, ila ndo ukweli, mimi mwenyewe namiliki gari ya mjapan
Wewe endesha gari kwa akili usigonge mipapai. Acha ulevi!!!

Mtu anatanua kijinga akipewa kubwa anaanza kusema ni mipango ya Mungu. Hakuna Mungu anayekupangia ufe kizembe. Upuuzi wa kutanua hovyo ndo unawauwa vibaya huko highway
 
Hizo ni Crumple zones..zipo maalamu kwa ajili kupunguza impact ya accident kwa occupants na pedestrian..ndo maana gari safety ratings zake inapimwa kwa uwezo crumple zone ku absorb impact ya ajali huku impact energy isiwafikie occupants kwa ukubwa, lakini pia ikitokea imegonga pedestrian basi bumper la plastic liweze kupunguza impact ya ajili..


Na tambua ajali zote zinazotea si fault ya gari bali ni faults ya madereva (95%}
Dereva wa kibongo anawazaga kukimbia tu bila tahadhari.
 
Boss gari za zaman hata utengenezwaji wake ulikua ni bati ngumu nakupa mfano kifo cha marehem mgombea aliekua anagombea kipindi magu anaingia 2015 alipata ajali na corola na ilibilingita lakini ile gari ilivunjika vioo tu na marehem alikufa sabab hakufunga mkanda wwnzie wote walipona then chukulia picha ingekua mark x au crown au vits ingekuaje
Sasa. Marehem kwanini asifunge mkanda nae. Huoni alizembea mwenyewe
 
😄😄 Wana JF bana,wanapenda vitu vigumu vigumu Kama Ni sifa vile.

Wengine wanadhani kuweka ngao kwny Gari'kwa logic Ile ile ya kupenda vitu vigumu vigumu' Ni Salama Sana kwny Gari kuliko kutokuweka ngao.Hawajui hata zilishapigwa hesabu hapo na wataalam za namna Gari ikigongana/ikigonga inavyoweza ku-absorb hio shock,wao wanaweka ngao na ku-defy hesabu za wataalam na wakigongana inakua shughuli.

Swali linakuja Ni model gani tunazotumia hapa Tz za wajapan(tuchukulie mfano za Toyota) ambazo zimetengenezwa special kwa ajili ya Africa tu ili tujue haya magari tunayolalamikia sisi(waafrika) yanatumiwa na waafrika tu au na wajapan/Asia wanayatumia magari hayahaya?
Bongo mtu anataka gari ya million 15 impe safety ya gari ya million 150.
 
Naona unauchukulia poa mpapai...
So ukiwekewa china tupu ukimgonga boda inakuaje, au mtembea kwa miguu, au ukigongana na chums kingine
 
Na bado kuna mtu aliuliza kwanini mchina hatengenezi gari ndogo hizi za bei chee.
Yaani kuulizia kifo kwa ziraili.
Alijibiwa yapo ila ni ya umeme.
Sipati picha gari ya mchina ya kuchaji.
Aisee hapo utajikuta sebuleni kwa Mungu bila hodi
 
Mkuu kwa usalama zaidi kuna vifaru urusi unaweza kuagiza tu ukaendesha ili usife kwa ajali. Kama gari lazma iwekwe material laini yasiokuumiza wakati wa impact. Yani gari iharibike ila utoke salama ndio dhumuni la airbags na body laini.
Aisee Nimecheka sana😅😅😅,
Aagize kifaru tu Ukraina
 
Bongo mtu anataka gari ya million 15 impe safety ya gari ya million 150.
Exactly! Tena gari la miaka 30 iliyopita. Utasikia "Rav4 old model ni gari gumu sana". Sasa unataka gari gumu kwani unakwenda kuling'olesha visiki jamani?
 
Back
Top Bottom