Tunakuja Duniani tukiwa kamili; Kila kitu chetu kinakuwepo ndani yetu

Tunakuja Duniani tukiwa kamili; Kila kitu chetu kinakuwepo ndani yetu

Victor Mlaki

JF-Expert Member
Joined
May 1, 2016
Posts
5,628
Reaction score
6,411
Uumbaji una mengi ambayo yanaonekana kama yamejificha ila ndivyo yalivyo na mengine ukiyaongea unaweza ukaonekana kama hayawani hivi lakini ndivyo ilivyo. Leo napenda kuonesha namna tunavyoingia Duniani tukiwa kamili. Ninaposema kamili namaanisha kuwa tunazaliwa tukiwa tayari tumeshakamilika kwa kuwa na kila kitu katika maisha yetu. tunaouna kama wakati ujao na matokeo yake ni mambo yaliyopo ndani yetu.

Ukitaka kujiridhisha juu ya hili unaweza kutumia njia nyingi sana na zote zikakuonesha jibu lile lile kuwa tunakuja tukiwa na kila kitu chetu. Baadhi ya watu hali hii ya kuja na ukamilifu wa vitu huiita nyota ya mtu.

Wapo baadhi ya watu wanaoweza kutumia njia za sihiri na kuona vitu vya mtu na kuamua kuvivuruga. Hii inathibitisha kuwa hatuji Duniani hivi hivi tu ila tunakuja tukiwa na vitu vyetu. Hapa namaanisha kila kitu cha maisha yetu.

Biblia inaonesha kuwa " Mungu huutangaza mwisho tangu mwazo". Hapa tunapata picha ya kiakili kuwa uumbaji uliokamilishwa na Mungu umebeba kila kitu na Mungu hukiona kitu kabla ya mwisho wake.

Kabla mtu hajawa mtu anayeishi Duniani Mungu alishamuona mtu huyo akiwa kamili na hivyo tunapoanza kuishi haimaanishi ndiyo mwanzo wetu ila tulishaonwa na Mungu akaweka kila kitu tulichokuja nacho katika ukamilifu ndiyo akaona tunafaa kuja (kuzaliwa)

Wapo watu waliojaliwa nguvu uwezo wa kuona vitu vya watu na angalau kuwasaidia kuvitumia kwa faida ya kila mtu na kila kitu kwa sababu siri za uumbaji zinaonesha kuwa lengo la uumbaji limefungamana na nguvu ya upendo inayosukuma faida ya kusudi la uwepo wa mtu kwa kila mtu na kwa kila kitu.

Wapo wanaotumia sihiri kupata nguvu na uwezo wa kuona vitu vya wengine kwa nia ovu ya kuvuruga, hii ni kutokana na udhaifu wa kiakili wa mwanadamu unaozalisha chuki na ubinafsi na kusahau kila mtu ana kila kitu kwa faida ya kila mtu na kila kitu.

Hatukuja Duniani ili kutafuta vitu, ila tumekuja tukiwa tayari na vitu vyetu. Kwa mana nyingine vitu vyetu havipo nje yetu ila vipo ndani yetu. Kutafuta vitu vyetu nje yetu ni safari ngumu ya Mwanadamu iliyokosa uelekeo sahihi. Kwa mfano hujawahi kukaa na mtu ukisikia watu wakisema Mtu huyo ana bahati sana na wengine kupenda kuwa karibu naye?

Tunajifunza habari nyingi za watu waliotabiriwa kuzaliwa miaka mingi kabla ya kuzaliwa kwao na mambo watakayoyafanya na cha kustaajabisha ni tukio halisi la watu hao kuzaliwa kweli na kufanya hayo yaliyonenwa. Hii ni ishara tosha ya kutufanya angalau kuafiki kuwa kuna vitu hukamilika mahali fulani kabla ya kutokea katika ulimwengu wa vitu.

Napenda nikuongezee ujasiri kuwa katika maisha haya yapo mambo yako iliyokuwa nayo na utayafanya, hayapo mbali na wewe ila yapo ndani yako umekuja nayo na yalishaonekana na kukamilika ndiyo maana ukaja katika Dunia hii nzuri.

Usikate tamaa utendaji wa nguvu za kiumbaji haubanwi na muda, upo muda wako wa kufanya mambo yako. Ili mradi bado upo elewa yapo yako yaliyokamilika na utapaswa kuyafanya wewe tu na siyo mwingine.

Kuna wakati unaweza ukajisikia wivu na kutamani kuwa kama mwenzako na kusahau kuwa una vitu vyako vizuri tu ambavyo yeye hana. Ukitaka kushinda tabia hii ya wivu jizoeshe kukataa kiakili kwa kujilazimisha akili yako kukumbuka kuwa yapo mambo yako mazuri mno ambayo ni faida kwa kila mtu nakwa kila kitu.

Kumbuka mfano huu; Gari linapotengezwa kiwandani watengezaji huwa na picha kamili ya kiakili ya muundo mzima wa gari hilo na kazi zake na haliwezi likaingizwa sokoni kabla ya kukamilika na kuangaliwa kama linafaa au la!.Hii inaonesha kuwa unaponunua gari jipya haimaanishi ndiyo limeanza ila lilishaanza na lilishakamilika kabla ya kukufikia wewe. Rejea " Mungu huutangaza mwisho tangu mwanzo" ili kuona uumbaji ulivyo.

Hatukuzaliwa kuja kukata tamaa na kukatishana tamaa, naandika hapa ili angalau tujaribu kuangalia ndani yetu kuliko nje yetu na tukumbuke tulipokuja Duniani haukuwa mwanzo wetu ila tayari tulikuwa tumeshakamilika na tukaonekana tunafaa ndiyo maana tulizaliwa.

Wewe unayesoma uzi huu elewa kabisa kuwa ulishinda na ukaonekana unafaa ndiyo maana upo hapa .Upo kamili na una kila kitu chako. Umbali siyo kikwazo najua tumewasiliana.
 
Back
Top Bottom